Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye huamrisha machafu na maovu. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingeli takasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [21]
[21] Enyi mlio amini! Hifadhini nafsi zenu kwa Imani. Wala msimfuate Shetani anaye kuvutieni kwenda tangaza uchafu na maasi baina yenu. Na mwenye kumfuata Shetani basi huyo amekwisha a'si, kwani Shetani anaamrisha madhambi makubwa makubwa na maasi mabaya. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake kwenu kwa kubainisha hukumu na kukubali toba ya wenye kuasi asinget'ahirika hata mmoja wenu na uchafu wa maasi. Lakini Mwenyezi Mungu anamsafisha mwenye kumuelekea Yeye kwa kumwezesha kuwa mbali na maasi, au kwa kumsamehe kwa kutubu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia kila kauli, Mwenye kujua kila kitu, na atakulipeni kwayo.
Na wale katika nyinyi wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa jamaa zao na masikini na walio hama kwa Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wasamehe, na waachilie mbali. Je! Nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [22]
[22] Wala wasiape wema wenu wenye nafasi kuwa watazuia kuwafanyia hisani jamaa zao na masikini na walio hama makwao katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wengineo kwa sababu za kibinafsi, kama vile kuwa wamewatendea uovu fulani. Lakini inatakikana wawasamehe na wayaachilie mbali makosa yao. Na ikiwa mnapenda Mwenyezi Mungu akusameheni maovu yenu basi wafanyieni wanao kufanyieni mabaya mfano wa anavyo kufanyieni nyinyi Mola wenu Mlezi. Na fuateni mwendo wake kwani Yeye ni Mkunjufu wa kusamehe na kurehemu. Aya hii imeteremka pale Abu Bakar r.a. alipo apa kumkatia msaada jamaa yake Mist'ah bin Uthaathah hapo alipo ingia Mist'ah katika uzushi alio zuliwa bibi Aisha r.a.
Hakika wanao wasingizia wanawake, wanao jihishimu, walio ghafilika, Waumini, wamelaaniwa duniani na Akhera, nao watapata adhabu kubwa. [23]
[23] Hakika hao wanao wasingizia wanawake wema walio safi, ambao hawadhaniwi hayo, bali wao kwa kumshughulikia Mwenyezi Mungu hata wameghafilika na hayo wanayo singiziwa, Mwenyezi Mungu atawatenga mbali na rehema yake katika dunia na Akhera, na watapata adhabu kubwa ikiwa hawatotubu.
Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyatenda. [24]
[24] Adhabu hiyo itakuwa Siku ya Kiyama ambapo itakuwa hapana njia ya kuikataa. Bali waliyo yatenda yatathibiti juu yao, kwa kuwa zitawashuhudia ndimi zao, na mikono yao, na miguu yao, kwa madhambi yote waliyo yatenda. Na hayo ni kwa kudhihiri athari ya vitendo vyao juu ya viungo hivyo, au kwa kutamkishwa na Mwenyezi Mungu ambaye anatamkisha kila kitu.
Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa sawa sawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki Iliyo Wazi. [25]
[25] Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu iliyo kwisha hukumiwa wapewe kwa ukamilifu wake bila ya upungufu. Na hapo wataujua kwa ujuzi wa yakini Ungu wa Mwenyezi Mungu na hukumu za Sharia yake, na ukweli wa ahadi yake na kitisho chake. Kwani yote hayo yatakuwa wazi hayana kificho.
Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Hao wameepushwa na hayo wanayo yasema; wao watapata msamaha na riziki ya ukarimu. [26]
[26] Wanawake waovu ni wa wanaume waovu, na wanaume waovu ni wa wanawake waovu. Na kadhaalika wanawake wema ni wa wanaume wema, na wanaume wema ni wa wanawake wema. Basi yamkini vipi kuwepo uwovu katika wema ulio hifadhiwa nao ni mke wa mwema muaminifu Mtume Mtukufu s.a.w.? Na wema hawa wamehifadhika na tuhuma wanazo wasingizia hao waovu. Na wao wana maghfira ya Mwenyezi Mungu kwa vijidhambi vidogo vidogo ambavyo mwanaadamu hakosekani kuwa navyo. Na watapata ukarimu mkubwa wa kupata neema za Peponi.
Enyi mlio amini! Msiingie nyumba zisio nyumba zenu mpaka mwombe ruhusa, na mwatolee salamu wenyewe. Hayo ni bora kwenu mpate kukumbuka. [27]
[27] Enyi mlio amini! Msiingie katika nyumba zisio kuwa zenu ila baada ya kutaka idhini kwa wakaazi wake na mkaruhusiwa kuingia, na baada ya kuwatolea salamu wakaazi wake - na salamu ni bora kwenu kuliko kuingia tu bila ya kutoa salamu. Na Mwenyezi Mungu amekuwekeeni sharia hii ili mpate kunasihika na muifuate.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".