Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាស្ហស្ហ៊ូអារ៉ក   អាយ៉ាត់:
مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يُمَتَّعُونَ
Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?.
Kustarehe kwao kwa umri mrefu na maisha mema hakutowakinga hata chembe na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani adhabu ya Mwenyezi Mungu itakuja tu, kama si leo kesho. Wala hapana kheri katika neema ambayo khatima yake ni adhabu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ
Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji.
Na mwendo wetu kwa kaumu zote ni kuwa hatuuteketezi umma ila baada ya kuwatumia Mitume wa kuwaonya kwa kufuata hoja,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ذِكۡرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
Wakumbuke na wazingatie. Wala si shani yetu kudhulumu hata tuuadhibu umma kabla ya kuwaletea Mtume.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَمَا تَنَزَّلَتۡ بِهِ ٱلشَّيَٰطِينُ
Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo,
Qur'ani inakataa waliyo yasema makafiri wa Makka ya kwamba Muhammad anafuata majini, nao ndio wanampa Qur'ani. Qur'ani inasema: Mashetani hawakuiteremsha hii Qur'ani.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَمَا يَنۢبَغِي لَهُمۡ وَمَا يَسۡتَطِيعُونَ
Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
Wala haiwafalii wao kuiteremsha, na hawawezi kufanya hivyo.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِنَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّمۡعِ لَمَعۡزُولُونَ
Hakika hao wametengwa na kusikia.
Kwani hao hakika wanazuiwa wasiisikie Qur'ani pale inapo funuliwa kwa Muhammad s.a.w.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلۡمُعَذَّبِينَ
Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa.
Basi wewe muelekee Mwenyezi Mungu ukiendelea na usafi wako wa ibada, wala usishughulike na fisadi za madai ya washirikina na mwendo wao muovu. Na hivi kutakiwa Mtume s.a.w. awe na ikhlasi ya namna hii ni wito kwa jamii ya watu waliomo katika umma wake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَأَنذِرۡ عَشِيرَتَكَ ٱلۡأَقۡرَبِينَ
Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
Watie khofu ya adhabu ya shirki na maasi walio karibu nawe katika jamaa zako.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini.
Na kuwa mpole kwa wanao itikia wito wako wa Imani.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَإِنۡ عَصَوۡكَ فَقُلۡ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تَعۡمَلُونَ
Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda.
Pindi wakikuasi na wasikufuate basi jitenge nao, na jitenge na vitendo vyao vya ushirikina na maasi yote.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ
Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
Na tegemeza mambo yako kwa Mwenye nguvu, Mwenye uweza wa kuwatenda nguvu adui zako kwa utukufu wake, na kukunusuru wewe na kumnusuru kila mwenye kufanya a'mali yake kwa usafi wa niya.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ٱلَّذِي يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ
Ambaye anakuona unapo simama,
Ambaye anakuona pale unapo simama kwa ibada za usiku na vitendo vyote vya kheri.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَتَقَلُّبَكَ فِي ٱلسَّٰجِدِينَ
Na mageuko yako kati ya wanao sujudu.
Na anaona mwendo wako kati ya wanao sali, kwa kusimama, na kukaa, na kurukuu na kusujudu, pale unapo waongoza katika Swala.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
Hakika Yeye Subhanahu ndiye Mwenye kusikia dua zako na dhikri zako, ndiye Mjuzi wa kujua niya yako na vitendo vyako. Ni kama kwamba Subhanahu anamwambia: Usichukue taklifu kubwa bila ya kiasi katika mashaka ya ibada, kwani uyatendayo yote nayaona na nayasikia Mimi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
هَلۡ أُنَبِّئُكُمۡ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَٰطِينُ
Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani?
Washirikina walisema: Mashetani ndio wanamsomea Qur'ani Muhammad. Qur'ani ikawajibu: Nikupeni khabari watu gani Mashetani ndio wanawateremkia, na wakawashawishi?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٖ
Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
Wanamteremkia kila mwenye kubeba dhambi za namna mbaya kabisa za uwongo, na madhambi ya kuchusha kabisa. Nao ni hao makohani mafisadi ambao tabia zao na tabia za Mashetani ni jinsi moja na zimewafikiana.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
يُلۡقُونَ ٱلسَّمۡعَ وَأَكۡثَرُهُمۡ كَٰذِبُونَ
Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo.
Hao hutega masikio yao kwa Mashetani, na kwao wakapata mambo ya dhana dhana tu. Na wengi wao ni waongo, na huzidisha tena juu ya kauli walizo zipata kwa Mashetani.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلۡغَاوُۥنَ
Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata.
Makafiri wanasema: Hii Qur'ani ni mashairi, na Muhammad ni mtungaji mashairi. Mwenyezi Mungu ameyavunja haya kwa kuthibitisha kuwa hakika Qur'ani imejaa hikima na hukumu. Mpango wake unapingana na mpango wa mashairi ambao unategemea juu ya kweli na uwongo. Na amebainisha kwamba hali ya Muhammad s.a.w. inapingana na hali ya watungaji mashairi. Yeye anasema kwa hikima, wao wanasema kwa udanganyifu. Na hii ndiyo hali ya wengi katika watungaji mashairi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
أَلَمۡ تَرَ أَنَّهُمۡ فِي كُلِّ وَادٖ يَهِيمُونَ
Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?
Kwani huwaoni vile wanavyo tangatanga katika mabonde ya maneno wala hawaongoki kwenye Haki?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَأَنَّهُمۡ يَقُولُونَ مَا لَا يَفۡعَلُونَ
Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?
Na kwamba wao husema kwa ndimi zao wasio yaambatisha na vitendo vyao?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَذَكَرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا وَٱنتَصَرُواْ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْۗ وَسَيَعۡلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ أَيَّ مُنقَلَبٖ يَنقَلِبُونَ
Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.
Lakini walio hidika kwa hidaya ya Mwenyezi Mungu, na wakatenda mema mpaka zikatua katika nafsi zao sifa bora, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi mpaka ikathibiti khofu katika nyoyo zao, hawa basi huyafanya mashairi kama dawa ilio sibu kwa ugonjwa wake. Na hupambana kwa ajili ya kuiwania Dini yao na kusimamisha Haki, inapo kuwa Haki inafanyiwa jeuri. Na walio dhulumu nafsi zao kwa shirki na kumkejeli Mtume kwa mashairi, watatafuta wapi pa kuikimbia shari na hilaki wanayo iendea.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាស្ហស្ហ៊ូអារ៉ក
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ