Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាស្ហស្ហ៊ូអារ៉ក   អាយ៉ាត់:
فَلَمَّا تَرَٰٓءَا ٱلۡجَمۡعَانِ قَالَ أَصۡحَٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدۡرَكُونَ
Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
Walipo onana makundi mawili, watu wa Musa walisema: Hakika Firauni na watu wake watatupata. Basi tutaangamia.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ كَلَّآۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهۡدِينِ
(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!
Musa akasema: Hakika mimi ninao uangalizi wa Mwenyezi Mungu unao nifuata kwa kunihifadhi. Na Yeye ataniongoza kwenye Njia ya uwokovu. Amesema hayo ili awatuze kuwa watasalimika, na iwe mbali na mawazo yao fikra ya kutisha kwamba takuja patikana. .
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡبَحۡرَۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرۡقٖ كَٱلطَّوۡدِ ٱلۡعَظِيمِ
Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.
Tukamuamrisha Musa kwa wahyi, ufunuo, aipige bahari kwa fimbo yake. Ikapasuka bahari njia kumi na mbili kwa mujibu wa idadi ya mataifa ya Wana wa Israili. Kila njia katika hizo njia ilikuwa na kizuizi cha maji yaliyo nyanyuka kama mlima ulio simama imara.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَأَزۡلَفۡنَا ثَمَّ ٱلۡأٓخَرِينَ
Na tukawajongeza hapo wale wengine.
Tukawajongeza Firauni na kaumu yake mpaka wakaingia kwenye zile njia nyuma ya Musa na kaumu yake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَأَنجَيۡنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ
Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
Tukamwokoa Musa na walio kuwa pamoja naye kwa hifadhi ya bahari nayo imeshikamana, mpaka wakamalizika kuvuka.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ
Kisha tukawazamisha hao wengine.
Kisha tukamzamisha Firauni pamoja na walio kuwa pamoja naye kwa kuwafudikiza kwa maji pale walipo wafuata.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini.
Hakika katika vituko hivi vya ajabu vya kiungu pana funzo la kuzingatia kwa atakaye kunafiika. Lakini watu wengi si wenye kusadiki.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
Hakika Muumba wako na Mlezi wako ndiye huyo Mwenye nguvu katika kuwaadhibu wanao kanusha, Mwenye kuwaneemesha kwa rehema Waumini.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ إِبۡرَٰهِيمَ
Na wasomee khabari za Ibrahim.
Ewe Mtume! Na wasomee makafiri hadithi ya Ibrahim , Alayhi Ssalaam.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَا تَعۡبُدُونَ
Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
Alipo mwambia baba yake: Mnaabudu kitu gani hichi, ambacho hakifai kuabudiwa? Anakusudia kwa hayo kuyakebehi masanamu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُواْ نَعۡبُدُ أَصۡنَامٗا فَنَظَلُّ لَهَا عَٰكِفِينَ
Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.
Wakasema kujibu kwa njia ya kujitapa: Tunaabudu masanamu, nasi tunadumu daima dawamu tukiyaabudu, kwa kuyaadhimisha na kuyatukuza!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ هَلۡ يَسۡمَعُونَكُمۡ إِذۡ تَدۡعُونَ
Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
Ibrahim akasema: Kwani yanasikia madua yenu? Au yanakuitikieni mnapo yaomba? Kwa hayo anakusudia kuwanabihisha upotovu wa mwendo wao.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
أَوۡ يَنفَعُونَكُمۡ أَوۡ يَضُرُّونَ
Au yanakufaeni, au yanakudhuruni?
Au yanakuleteeni manufaa mnapo yat'ii? Au yanakupatilizeni kwa madhara mkiyaasi?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُواْ بَلۡ وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفۡعَلُونَ
Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.
Wakasema: Hawafanyi lolote katika hayo. Lakini sisi tumewakuta baba zetu wakiyaabudu mfano wa ibada yetu. Basi sisi tukawafwata kwa waliyo kuwa wakiyafanya.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ أَفَرَءَيۡتُم مَّا كُنتُمۡ تَعۡبُدُونَ
Je! Mmewaona hawa mnao waabudu-
Ibrahim akasema kwa kuwasusuika: Je! Mlifikiri hata mkalijua jambo lolote lilio kupelekeeni kudumu na kuyaabudu hayo masanamu?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلۡأَقۡدَمُونَ
Nyinyi na baba zenu wa zamani?
Nyinyi na baba zenu wa zamani - ati haya yanastahiki kuabudiwa au la? Lau mngeli zingatia mngeli jua kuwa hakika nyinyi mko katika upotovu ulio wazi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَإِنَّهُمۡ عَدُوّٞ لِّيٓ إِلَّا رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Kwani hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni maaadui kwangu mimi na kwenu. Basi mimi siwaabudu hao. Lakini ninaye muabudu na najijongeza kwake ni Muumba wa walimwengu wote, na Mwenye kumiliki mambo yao, na Mwenye kuwalinda.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ٱلَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهۡدِينِ
Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa,
Ambae ndiye aliye nizua kabla sijawa chochote akaniumba kwa bora ya umbo, na akanitunukia uwongofu wa kunifikishia kwenye mafanikio yangu ya duniani na Akhera.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِي هُوَ يُطۡعِمُنِي وَيَسۡقِينِ
Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.
Na Yeye ndiye aliye nineemesha kwa vyakula na vinywaji, na akaniwezesha kuvipata na kunafiika kwavyo, ili kuhifadhi uhai wangu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ
Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.
Na yakinishukia maradhi ni Yeye ndiye anaye niponesha, kwa kunisahilishia sababu za kupona na kuniwezesha kuzipata.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحۡيِينِ
Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.
Na Yeye ndiye atanifisha ikifika ajali yangu, na tena atanihuisha mara nyengine kwa ajili ya hisabu na malipo.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِيٓ أَطۡمَعُ أَن يَغۡفِرَ لِي خَطِيٓـَٔتِي يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo.
Na Yeye ndiye ninaye mtumai kunighufiria na kuyasemehe makosa yangu madogo madogo ya kujikwaa duniani, utapo fika wakati wa hisabu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
رَبِّ هَبۡ لِي حُكۡمٗا وَأَلۡحِقۡنِي بِٱلصَّٰلِحِينَ
Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema.
Ibrahim a.s. akasema kwa kuomba: Mola wangu Mlezi! Nitunukie ukamilifu wa ilimu na vitendo, ili nipate kustahili kuubeba Ujumbe wako na hukummu kwa waja wako, na niwezeshe niungane pamoja na kundi la watendao wema.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាស្ហស្ហ៊ូអារ៉ក
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ