Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. [128]
[128] Na mwanamke akikhofia kuwa mumewe anapuuza mambo ya nyumbani au anayatupa, hayajali, wala hayashughulikii, basi hapana dhambi kwa wote hao wawili kutafuta njia za kusuluhiana kwa mapatano mema na kukurubiana. Na mwenye akili kati yao ni yule anaye anza kutaka masikizano. Na suluhu daima ina kheri, haina shari ndani yake. Linalo zuia masikizano ni kule kuwa kila mmoja kung'ang'ania haki yake kwa ukamilifu, na ugumu na uchoyo wa nafsi unapo wamiliki watu. Wala hapana njia ya kurejeza mapenzi ila mmojapo kati ya wawili kulegeza kamba. Na huyo ndiye mwema, mchamngu, mwenye kujihifadhi na dhulma. Na mwenye kutenda vitendo vyema na akamcha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu anayo khabari ya vitendo vyake, na atamlipa kwavyo.
Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu. [129]
[129] Kuwafanyia uadilifu wake kwa mapenzi ya daima yasiyo chafuliwa na udanganyifu, na kutendeana usawa katika mapenzi ikawa nipe nikupe, ni jambo lisilo wezekana kuwa. Kadhaalika haiwezi kuwepo usawa katika kuwapenda wake, ikiwa kuna zaidi kuliko mke mmoja. Walakini mkijitahidi, basi msimfanyie ujeuri mmoja wapo, mkamili upande mmoja, na mkamwacha mwengine si mke si mt'alaka. Yapasa mjitengeneze, na muendeshe nyumba zenu kwa wema si kwa ufisadi. Na mcheni Mwenyezi Mungu apate kughufirieni na akurehemuni. Ni shani yake kughufiria na kurehemu.
Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima. [130]
[130] Ikiwa suluhu haikumkinika na ikawa chuki (au karaha) imeshika nguvu zaidi, basi inalazimika kufarikiana. Na wakifarikiana Mwenyezi Mungu atawatosheleza kila mmoja wao kutokana na ukunjufu wa rehema yake na fadhila yake. Na riziki ziko katika mikono ya Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye hikima, na hupanga mambo yote kwa mipango yake.
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa. [131]
[131] Kiini cha Dini ni kumnyenyekea Mwenye kuumba ulimwengu, Mwenye utukufu na ukarimu, na kuukubali ufalme wake usio na ukomo. Kwani ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Na kwa huu Ufalme usio na ukomo amesema: Tumewausia watu wa dini zilizo toka mbinguni, katika Watu wa Kitabu na nyinyi Waislamu, mumkhofu Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na msiwe mnakufuru katika ibada yake, maana Yeye ndiye Mwenye utawala mkubwa kushinda wote. Hapana kitu kilicho toka nje ya utawala wake. Yeye ni Mkwasi, yaani mwenye kujitosha wala hakuhitajiini nyinyi. Juu ya hivyo Yeye anakuhimidini kwa imani yenu, kwani kwa kuwa Yeye ni Mwenye kujitosheleza mwenyewe, juu ya hivyo anasifu na kushukuru vitendo vyema vya waja wake.
Na ni vya Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi. [132]
[132] Kupanga kila kitu cha mbinguni na duniani ni kazi ya Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka. Yeye ndiye Mwenye madaraka, Mwenye kuendesha, Mwenye kupanga. Yatosha kuwa Yeye ndiye Mtawala aliye amrisha ulimwengu ukajipanga ulivyo jipanga, na akawaamrisha watu wamuabudu, na wamtegemezee Yeye mambo yao, na wamche Yeye.
Akitaka atakuondoeni, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hayo. [133]
[133] Hakika nyinyi enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mko chini ya ufalme wa Mwenyezi Mungu Mwenye uweza na Mwenye nguvu. Akipenda atakufisheni na alete wengine kabisa. Na Yeye Mwingi wa Utukufu ni Muweza wa hayo, na Muweza wa kila kitu.
Anaye taka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona. [134]
[134] Na watu, pindi wakitafuta neema za dunia zilizo halali kwa njia ya haki iliyo nyooka sawa, basi hakika Mwenyezi Mungu atawapa neema za duniani na Akhera; kwani Yeye ndiye aliye miliki neema zote mbili.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".