Check out the new design

ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ಅಬ್ದುಲ್ಲಾ ಮುಹಮ್ಮದ್ ಮತ್ತು ನಾಸಿರ್ ಖಮೀಸ್ * - ಅನುವಾದಗಳ ವಿಷಯಸೂಚಿ


ಅರ್ಥಗಳ ಅನುವಾದ ಅಧ್ಯಾಯ: ಅನ್ನಹ್ಲ್   ಶ್ಲೋಕ:
وَأَلۡقَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَأَنۡهَٰرٗا وَسُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Na Ameyakitisha kwenye ardhi majabali ya kuithibitisha ili isije ikawayumbisha nyinyi, na Ameiweka humo mito ili mpate kunywa maji yake, na Amefanya humo njia nyingi ili mpate kuongoka kwa njia hizo kuzifikia sehemu mnazozikusudia.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَعَلَٰمَٰتٖۚ وَبِٱلنَّجۡمِ هُمۡ يَهۡتَدُونَ
Na kwenye hiyo ardhi Ameweka alama ambazo kwa alama hizo mnajielekeza njia kipindi cha mchana, kama alivyoziweka nyota ili kujiongoza kwa nyota hizo kipindi cha usiku.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
أَفَمَن يَخۡلُقُ كَمَن لَّا يَخۡلُقُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Basi mnamfanya Mwenyezi Mungu Ambaye Anaviumba vitu hivyi na vinginevyo, katika kustahiki Kwake kuabudiwa Peke Yake, ni kama waungu wanaodaiwa ambao hawaumbi chochote? Basi hamukumbuki utukufu wa Mwenyezi Mungu mkamuabudu Yeye Peke Yake?
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na mkijaribu kuzidhibiti neema za Mwenyezi Mungu kwenu, ili mjue idadi yake, hamuwezi kuzidhibiti kwa wingi wake na utafauti wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, ni Mwenye huruma kwenu, kwani Anasamehe kasoro zenu za kutotekeleza ushukuru wa neema, wala Hazikati kwenu, kwa kukiuka kwenu mipaka, wala Hawaharakishii mateso.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَ
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kila aina ya upungufu, Anayajua matendo yenu yote, sawasawa yale mnayoyaficha ndani ya nafsi zenu kati ya hayo na yale mnayoyafanya waziwazi mbele ya wengine, na Atawalipa kwayo.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخۡلُقُونَ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Na wale waungu ambao washirikina wanawaabudu hawaumbi chochote hata kama ni kidogo vipi. Hao ni viumbe ambazo washirikina wamevitengeneza kwa mikono yao. Vipi basi wataviabudu?
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
أَمۡوَٰتٌ غَيۡرُ أَحۡيَآءٖۖ وَمَا يَشۡعُرُونَ أَيَّانَ يُبۡعَثُونَ
Wote hao ni visiki, havina uhai, wala hawajui wakati ambao Mwenyezi Mungu Atawafufua wale wanaowaabudu. Na waungu hao pamoja na wanaowaabudu wote watatupwa Motoni Siku ya Kiyama.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٞ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ
Mola wenu Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa Peke Yake. Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Mmoja Peke Yake, hivyo basi wale wasioamini kufufuliwa, nyoyo zao ni zenye kuukanusha upweke Wake, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kutoogopa mateso Yake. Kwa hivyo, wao wana ujeuri wa kutoikubali haki na kukataa kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡتَكۡبِرِينَ
Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu Anayajua wanayoyaficha ya itikadi, maneno na vitendo, na wanayoyaonyesha waziwazi katika hayo, na Atawalipa kwa hayo. Kwa kweli Yeye, Aliyeshinda na kutukuka, Hawapendi wanaofanya ujeuri wa kukataa kumuabudu na kumtii, na Atawalipa kwa hilo.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمۡ قَالُوٓاْ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Na pindi wanapoulizwa, hawa washirikina, kuhusu yale yaliyoteremshiwa Nabii Muhammad, rehema za Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wanasema kwa urongo na uzushi, «Hakuleta isipokuwa visa vya waliotangulia na porojo zao.»
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
لِيَحۡمِلُوٓاْ أَوۡزَارَهُمۡ كَامِلَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَمِنۡ أَوۡزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۗ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ
Mwisho wao utakuwa ni kuzibeba dhambi zao kamili Siku ya Kiyama, hawatasamehewa chochote, na watazibeba dhambi za wale waliowadanganya ili kuwaepusha na Uislamu, bila ya kupunguziwa dhambi zao. Jueni mtanabahi, ni ubaya ulioje wa dhambi watakazozibeba!
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
قَدۡ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنۡيَٰنَهُم مِّنَ ٱلۡقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّقۡفُ مِن فَوۡقِهِمۡ وَأَتَىٰهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ
Kabla ya washirikina hawa, makafiri waliwafanyia vitimbi Mitume wao, na kuifanyia vitimbi haki waliokuja nayo. Hapo amri ya Mwenyezi Mungu ililijia jengo lao kutoka kwenye asili yake na msingi wake, na sakafu ikawaangukia, na maangamivu yakawajia kwenye sehemu ambazo walijimakini kuwa ni za amani, kutoka mahali wasipodhania kuwa maangamivu yatawajia kutoka hapo.
ಅರಬ್ಬಿ ವ್ಯಾಖ್ಯಾನಗಳು:
 
ಅರ್ಥಗಳ ಅನುವಾದ ಅಧ್ಯಾಯ: ಅನ್ನಹ್ಲ್
ಅಧ್ಯಾಯಗಳ ವಿಷಯಸೂಚಿ ಪುಟ ಸಂಖ್ಯೆ
 
ಪವಿತ್ರ ಕುರ್‌ಆನ್ ಅರ್ಥಾನುವಾದ - ಸ್ವಾಹಿಲಿ ಅನುವಾದ - ಅಬ್ದುಲ್ಲಾ ಮುಹಮ್ಮದ್ ಮತ್ತು ನಾಸಿರ್ ಖಮೀಸ್ - ಅನುವಾದಗಳ ವಿಷಯಸೂಚಿ

ಅನುವಾದ - ಡಾ. ಅಬ್ದುಲ್ಲಾ ಮುಹಮ್ಮದ್ ಅಬೂಬಕರ್ ಮತ್ತು ಶೈಖ್ ನಾಸಿರ್ ಖಮೀಸ್

ಮುಚ್ಚಿ