Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa madai yao tu. Na wanyama hawa imeharimishwa migongo yao kupandwa. Na wanyama wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao. Wanamzulia uwongo tu Mwenyezi Mungu. Atawalipa kwa hayo wanayo mzulia.
Na katika mawazo yao ni kusema kwao: Ngamia hawa, na ng'ombe hawa, na mbuzi na kondoo hawa, na mazao haya ya mimea, ni marfuku. Hayali mtu ila wamtakaye katika utumishi wa masanamu. Hayo ni kwa madai yao ya uwongo, wala hayatokani na Mwenyezi Mungu. Na pia husema: Ngamia hawa wameharimishwa migongo yao, basi hapana ruhusa mtu kuwapanda. Nao juu ya hao hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wanapo wachinja hao ngamia, na ng'ombe, na mbuzi na kondoo. Na hayo ni kwa kule kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ushirikina wao. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa adhabu huko Akhera kwa sababu ya uzushi wao, na kuharimisha kwao vitu ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuharimisha.
Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni kwa ajili ya wanaume wetu tu, na wameharimishwa kwa wake zetu. Lakini ikiwa nyamafu basi wanashirikiana. Mwenyezi Mungu atawalipa kwa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hikima, Mwenye kujua.
Na katika mawazo yao ya uwongo hawa washirikina ni kuwa wanasema: Viliomo matumboni mwa wanyama walio watenga, walio zuwiwa wasichinjwe wala wasipandwe - viliomo matumboni mwao, yaani watoto, wanafaa kuliwa na wanaume, na haramu kwa wanawake. Na juu ya hivyo akizaliwa naye kesha kufa wote wanashirikiana wanakula! Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa kwa uwongo wao walio mzulia kwa kitendo chao. Kwani wanadai kuwa kuharimishwa huku kunatokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu, na ni Mwenye hikima. Vitendo vyake vyote ni kwa mujibu wa hikima. Naye atawalipa wenye dhambi kwa dhambi zao.
Hakika wamekhasirika wale ambao wamewauwa watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua, na wakaharimisha alivyo waruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu. Hakika wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Hakika wamekhasiri hao walio wauwa watoto wao kwa ujinga na kwa mawazo ya uwongo, bila ya kujua nini matokeo ya kitendo chao, wala sababu yake; na wakajiharimishia nafsi zao riziki alizo waruzuku Mwenyezi Mungu katika mimea, na wanyama, huku wakimzulia Mwenyezi Mungu kwa kudai kuwa ni Yeye ndiye aliye harimisha. Na hakika wamejitenga mbali na Haki kwa sababu hiyo. Na kwa sababu ya uzushi huu hawakuwa katika wanao sifika kwa uwongofu.
Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.
Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye umba bustani za matunda. Ipo miti inayo pandwa na kuegemezwa juu ya chanja, na ipo isiyo hitajia chanja. Na ameumba mitende, na mimea mingine inayo toa matunda yanayo khitalifiana kwa rangi, na utamu, na sura, na harufu na mengineyo. Na ameumba mizaituni, na makomamanga (makudhumani), yenye kushabihiana katika baadhi ya sifa zake, na isiyo shabihiana, ijapo kuwa udongo huenda ukawa ule ule, na yote ikawa inanyweshwa na maji yale yale. Basi kuleni matunda yake mkipenda, na toeni sadaka yake yanapo wiva na kuyachuma. Wala msifanye fujo katika kula, mkajidhuru wenyewe, na mkawadhuru mafakiri katika kuwanyima haki yao. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watumiao kwa fujo, katika mwendo wao na vitendo vyao.
Na katika wanyama amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu dhaahiri.
Na Mwenyezi Mungu ameumba katika nyama hoa, nao ni ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, wale wanao beba mizigo yenu, na wale ambao katika sufi yao na manyoya yao na nyewele zao mnatoa matandiko. Na hiyo ni riziki aliyo kujaalieni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni alicho kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msimfuate Shetani na marafiki zake katika kuzua vya halali na haramu, kama walivyo kuwa wakifanya watu wa Jahiliya! Hakika Shetani hakutakiini kheri, kwa sababu yeye ni adui yenu, mwenye uadui dhaahiri.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
ಹುಡುಕಾಟದ ಫಲಿತಾಂಶಗಳು:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".