Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli.
Mwenyezi Mungu ameumba katika kila namna ya nyama hoa dume na jike. Hizo basi ni namna nane. Kondoo namna mbili, mbuzi namna mbili. (ngamia na ng'ombe wametajwa katika Aya inayo fuata.) Ewe Muhammad! Waambie washirikina kukanya hayo waliyo yaharimisha: Nini sababu ya kuharimisha katika hawa kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa madume? Au kwa kuwa ni kuwa matumboni ya mama zao? Hayo hayawezi kuwa hivyo, kwa sababu nyinyi hamkuharimisha watoto waliomo tumboni kabisa!! Nambieni kwa mategemeo baraabara, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika kuhalalisha na kuharimisha.
.Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu.
Na Mwenyezi Mungu ameumba ngamia namna mbili, dume na jike, na ng'ombe namna mbili mbili vile vile. Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanya: Nini sababu ya kuwaharimisha hao mlio harimisha kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa wao ni madume? Sivyo hivyo; kwa sababu pengine mnahalalisha madume! Au ni kwa kuwa majike? Pia sio hivyo, kwa sababu mnahalalisha majike wakati mwingine! Au kwa kuwa wana watoto matumboni mwao? Pia sio hivyo, kwa sababu hamkuharimisha watoto walio matumboni daima. Nanyi mnadai kuwa kuharimisha huku kunatokana na Mwenyezi Mungu! Nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuharimisheni haya na mkamsikia makatazo yake? Kabisa hayo hayakuwa. Wacheni mlio nayo; kwani hiyo ni dhulma. Na hapana mwenye kudhulumu zaidi kuliko mwenye kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu, akamnasibisha nayo mambo yasiyo toka kwake, wala hayana tegemeo lolote la ki-ilimu la kutegemea, bali huyo anataka kuwapotosha watu tu! Mwenyezi Mungu hawawafikishi wenye kudhulumu wakikhiari njia ya upotovu.
Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ewe Nabii! Sema: Hivi sasa sipati katika panapo toka mambo ya kuhalalisha na kuharimisha katika niliyo funuliwa mimi wahyi juu ya chakula kilicho harimishwa kula mlaji, isipo kuwa kitu hicho kiwe ni nyamafu, kimekufa na hakikuchinjwa kwa njia za sharia; au damu inayo tiririka, au nyama ya nguruwe - kwani hivyo vilivyo tajwa vinadhuru, na vichafu, havijuzu kula. Na pia katika vitu vilivyo harimishwa kula vinavyo toka katika itikadi sahihi, kwa kuwa wakati wa kuchinjwa lilitajwa jina lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu, kama sanamu au muabudiwa mwenginewe! Juu ya hivyo mwenye kulazimika kwa dharura kula kitu katika hivi vilivyo harimishwa, bila ya kuwa anatafuta utamu tu wa kula, na bila ya kupita mpaka wa ile dharura, basi huyo hana dhambi. Kwa sababu Mola wako Mlezi ni Mwenye kughufiria, na Mwenye kurehemu.
Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli.
Basi hivi ndivyo tulivyo kuharimishieni nyinyi. Na Mayahudi tuliwaharimishia nyama na shahamu na kila kitu cha wenye makucha katika wanyama, kama ngamia na wanyama wawindao. Na katika ng'ombe na mbuzi na kondoo tuliwaharimishia shahamu yake tu, ila shahamu ya mgongoni, au iliyoko matumboni, au iliyo changanyika na mafupa. Na kuharimishwa huku kulikuwa kwa ajili ya kuwatesa tu kwa ajili ya dhulma zao, na kuziachisha nafsi zao waweze kujilinda na matamanio. Na hakika Sisi tunasema kweli katika maneno yetu yote, na miongoni ya hayo ni khabari hii.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
ಹುಡುಕಾಟದ ಫಲಿತಾಂಶಗಳು:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".