prev

AlHujurat

next

1 : 49

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُقَدِّمُواْ بَيۡنَ يَدَيِ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٞ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake msiamue jambo la Sheria za Dini yenu kinyume cha maamuzi ya Allah Mtukufu na Mtume Wake, mkaingia kwenye uzushi. Na muogopeni Allah Mtukufu katika maneno yenu na vitendo vyenu, isije amri ya Allah Mtukufu na Mtume Wake ikaendewa kinyume. Hakika Allah Mtukufu ni Msikizi wa maneno yenu, ni Mjuzi wa nia zenu na vitendo vyenu. Hapa pana onyo kwa Waumini wasifanye uzushi katika Dini au kuleta sheria ambazo Allah Mtukufu Hakuziruhusu. info
التفاسير: |

2 : 49

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَرۡفَعُوٓاْ أَصۡوَٰتَكُمۡ فَوۡقَ صَوۡتِ ٱلنَّبِيِّ وَلَا تَجۡهَرُواْ لَهُۥ بِٱلۡقَوۡلِ كَجَهۡرِ بَعۡضِكُمۡ لِبَعۡضٍ أَن تَحۡبَطَ أَعۡمَٰلُكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تَشۡعُرُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, msiinue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii mnaposema naye, wala msipige kelele mnapomuita kama mnavyopigiana kelele nyinyi kwa nyinyi, na ongeeni naye kwa namna tafauti ya vile mnavyoongea na wengine, kama alivyokuwa tafauti na wengine kwa kuteuliwa kuubeba ujumbe wa Mola Wake, ulazima wa kumuamini, kumpenda, kumtii na kumfuata kwa kuogopa yasitenguke matendo yenu mema bila nyinyi kufahamu wala kulihisi hilo. info
التفاسير: |

3 : 49

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَغُضُّونَ أَصۡوَٰتَهُمۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ٱمۡتَحَنَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡ لِلتَّقۡوَىٰۚ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٌ عَظِيمٌ

Hakika wale wanaoziteremsha sauti zao chini mbele ya Mtume wa Allah Mtukufu, hao ni wale ambao Allah Mtukufu Amewatahini nyoyo zao na akazitia uchamungu, watapata msamaha wa dhambi zao kutoka kwa Mola wao na malipo mema mengi, nayo ni Pepo. info
التفاسير: |

4 : 49

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُنَادُونَكَ مِن وَرَآءِ ٱلۡحُجُرَٰتِ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡقِلُونَ

Hakika wale wanaokuita, (ewe Nabii), nyuma ya vyumba vyako kwa sauti ya juu, wengi wao hawana akili ya kuwapelekea kuwa na adabu nzuri pamoja na Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kumheshimu. info
التفاسير: |
prev

AlHujurat

next
:
0:00 0:00