Check out the new design

แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - ศูนย์การแปลรุว๊าด * - สารบัญ​คำแปล


แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: An-Nahl   อายะฮ์:
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمۡ سَكَنٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ بُيُوتٗا تَسۡتَخِفُّونَهَا يَوۡمَ ظَعۡنِكُمۡ وَيَوۡمَ إِقَامَتِكُمۡ وَمِنۡ أَصۡوَافِهَا وَأَوۡبَارِهَا وَأَشۡعَارِهَآ أَثَٰثٗا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ
Na Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amewajaalia ni kutokana na ngozi za wanyama, nyumba mnazoziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلٗا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡجِبَالِ أَكۡنَٰنٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلۡحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأۡسَكُمۡۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡلِمُونَ
Na Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba, na amewafanyia maskani milimani, na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto, na nguo za kuwakinga katika vita vyenu. Ndivyo hivyo anawatimizia neema zake ili mpate kujisalimisha kwake.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَإِنَّمَا عَلَيۡكَ ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Kwa hivyo, wakikengeuka, basi lililo juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi tu.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَعۡرِفُونَ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكۡثَرُهُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ
Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ
Na siku tutakapomtoa shahidi kutoka katika kila umma, kisha hawataruhusiwa wale waliokufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلۡعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ
Na wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, hawatapunguziwa adhabu hiyo, wala hawatapewa muhula.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ شُرَكَآءَهُمۡ قَالُواْ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدۡعُواْ مِن دُونِكَۖ فَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلَ إِنَّكُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na wale walioshirikisha watakapowaona hao waliowashirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako. Lakini hao watawatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo!
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَأَلۡقَوۡاْ إِلَى ٱللَّهِ يَوۡمَئِذٍ ٱلسَّلَمَۖ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Na siku hiyo watasalimu amri mbele ya Mwenyezi Mungu, na yatapotea yale waliyokuwa wakiyazua.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
 
แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: An-Nahl
สารบัญสูเราะฮ์ หมายเลข​หน้า​
 
แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - ศูนย์การแปลรุว๊าด - สารบัญ​คำแปล

แปลโดยทีมงานศูนย์แปลรุว๊าด ร่วมกับสมาคมการเผยแพร่ศาสนาอิสลามที่รอบวะฮ์ และสมาคมบริการเนื้อหาอิสลามด้วยภาษาต่าง ๆ

ปิด