Check out the new design

แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - ศูนย์การแปลรุว๊าด * - สารบัญ​คำแปล


แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Al-A‘rāf   อายะฮ์:
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمۡنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمۡ تَغۡفِرۡ لَنَا وَتَرۡحَمۡنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Wakasema: Mola wetu Mlezi! Tumezidhulumu nafsi zetu, na kama hutatufutia dhambi na ukaturehemu, hakika tutakuwa katika waliohasirika.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ
Akasema: Teremkeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Nanyi katika ardhi mtakuwa na makao na starehe mpaka ufike muda.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قَالَ فِيهَا تَحۡيَوۡنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنۡهَا تُخۡرَجُونَ
Akasema: Humo mtakuwa hai, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ قَدۡ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمۡ لِبَاسٗا يُوَٰرِي سَوۡءَٰتِكُمۡ وَرِيشٗاۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقۡوَىٰ ذَٰلِكَ خَيۡرٞۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Enyi wanadamu! Hakika tumewateremshia vazi la kuficha tupu zenu, na vazi la pambo. Na vazi la uchamungu, hilo ndilo bora zaidi. Hilo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili mpate kukumbuka.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٰتِهِمَآۚ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Enyi wanadamu! Kamwe Shetani asiwafitini kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani lile, akawavua vazi lao ili awaonyeshe tupu zao. Hakika yeye anawaona yeye na kabila yake kwa namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wasaidizi wa wale wasioamini.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
وَإِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةٗ قَالُواْ وَجَدۡنَا عَلَيۡهَآ ءَابَآءَنَا وَٱللَّهُ أَمَرَنَا بِهَاۗ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na wanapofanya uchafu, husema: Tuliwakuta baba zetu juu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uchafu. Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua?
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ
Sema: Mola wangu Mlezi ameamrisha uadilifu, na zielekezeni nyuso zenu kila mnaposujudu, na muombeni Yeye kwa kumfanyia yeye tu Dini. Kama alivyowaanzisha, ndivyo mtakavyorudi.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلضَّلَٰلَةُۚ إِنَّهُمُ ٱتَّخَذُواْ ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُم مُّهۡتَدُونَ
Kundi moja ameliongoa, na kundi jingine limethibitikiwa na upotovu. Kwa hakika hao waliwafanya mashetani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka.
ตัฟสีรต่างๆ​ ภาษาอาหรับ:
 
แปลความหมาย​ สูเราะฮ์: Al-A‘rāf
สารบัญสูเราะฮ์ หมายเลข​หน้า​
 
แปล​ความหมาย​อัลกุรอาน​ - คำแปลภาษาสวาฮิลี - ศูนย์การแปลรุว๊าด - สารบัญ​คำแปล

แปลโดยทีมงานศูนย์แปลรุว๊าด ร่วมกับสมาคมการเผยแพร่ศาสนาอิสลามที่รอบวะฮ์ และสมาคมบริการเนื้อหาอิสลามด้วยภาษาต่าง ๆ

ปิด