Check out the new design

Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin * - Indise ng mga Salin


Salin ng mga Kahulugan Surah: Yā-Sīn   Ayah:

Yasin

يسٓ
Ya Sin.[1]
[1] Herufi hizi "Ya, Sin" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡحَكِيمِ
Kwa Haki ya Qur-ani yenye hekima!
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Juu ya njia iliyonyooka.
Ang mga Tafsir na Arabe:
تَنزِيلَ ٱلۡعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ
Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمۡ فَهُمۡ غَٰفِلُونَ
Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika.
Ang mga Tafsir na Arabe:
لَقَدۡ حَقَّ ٱلۡقَوۡلُ عَلَىٰٓ أَكۡثَرِهِمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّا جَعَلۡنَا فِيٓ أَعۡنَٰقِهِمۡ أَغۡلَٰلٗا فَهِيَ إِلَى ٱلۡأَذۡقَانِ فَهُم مُّقۡمَحُونَ
Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَجَعَلۡنَا مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ سَدّٗا وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ سَدّٗا فَأَغۡشَيۡنَٰهُمۡ فَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao. Na tumewafunika macho yao, kwa hivyo hawaoni.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَسَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ ءَأَنذَرۡتَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تُنذِرۡهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكۡرَ وَخَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِۖ فَبَشِّرۡهُ بِمَغۡفِرَةٖ وَأَجۡرٖ كَرِيمٍ
Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman (Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَنَكۡتُبُ مَا قَدَّمُواْ وَءَاثَٰرَهُمۡۚ وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ فِيٓ إِمَامٖ مُّبِينٖ
Hakika Sisi tunawafufua wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza, na wanayoyaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلًا أَصۡحَٰبَ ٱلۡقَرۡيَةِ إِذۡ جَآءَهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Na wapigie mfano wa wakazi wa mji walipojiwa na Mitume.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِذۡ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمُ ٱثۡنَيۡنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزۡنَا بِثَالِثٖ فَقَالُوٓاْ إِنَّآ إِلَيۡكُم مُّرۡسَلُونَ
Tulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: "Hakika sisi tumetumwa kwenu."
Ang mga Tafsir na Arabe:
قَالُواْ مَآ أَنتُمۡ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا وَمَآ أَنزَلَ ٱلرَّحۡمَٰنُ مِن شَيۡءٍ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا تَكۡذِبُونَ
Wakasema: "Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uongo tu."
Ang mga Tafsir na Arabe:
قَالُواْ رَبُّنَا يَعۡلَمُ إِنَّآ إِلَيۡكُمۡ لَمُرۡسَلُونَ
Wakasema: "Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu."
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَمَا عَلَيۡنَآ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
قَالُوٓاْ إِنَّا تَطَيَّرۡنَا بِكُمۡۖ لَئِن لَّمۡ تَنتَهُواْ لَنَرۡجُمَنَّكُمۡ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٞ
Wakasema: "Sisi tumeamua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu."
Ang mga Tafsir na Arabe:
قَالُواْ طَٰٓئِرُكُم مَّعَكُمۡ أَئِن ذُكِّرۡتُمۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ مُّسۡرِفُونَ
Wakasema: "Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka."
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَجَآءَ مِنۡ أَقۡصَا ٱلۡمَدِينَةِ رَجُلٞ يَسۡعَىٰ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱتَّبِعُواْ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: "Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa."
Ang mga Tafsir na Arabe:
ٱتَّبِعُواْ مَن لَّا يَسۡـَٔلُكُمۡ أَجۡرٗا وَهُم مُّهۡتَدُونَ
Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَمَالِيَ لَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِي فَطَرَنِي وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Na kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa?
Ang mga Tafsir na Arabe:
ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدۡنِ ٱلرَّحۡمَٰنُ بِضُرّٖ لَّا تُغۡنِ عَنِّي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَا يُنقِذُونِ
Je, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنِّيٓ إِذٗا لَّفِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٍ
Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنِّيٓ ءَامَنتُ بِرَبِّكُمۡ فَٱسۡمَعُونِ
Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!
Ang mga Tafsir na Arabe:
قِيلَ ٱدۡخُلِ ٱلۡجَنَّةَۖ قَالَ يَٰلَيۡتَ قَوۡمِي يَعۡلَمُونَ
Akaambiwa: "Ingia Peponi!" Akasema: "Laiti kuwa watu wangu wangelijua.
Ang mga Tafsir na Arabe:
بِمَا غَفَرَ لِي رَبِّي وَجَعَلَنِي مِنَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ
Jinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe, na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
۞ وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَىٰ قَوۡمِهِۦ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِن جُندٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ
Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِن كَانَتۡ إِلَّا صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَإِذَا هُمۡ خَٰمِدُونَ
Hakukuwa ila ukelele mmoja tu, na mara walizimwa!
Ang mga Tafsir na Arabe:
يَٰحَسۡرَةً عَلَى ٱلۡعِبَادِۚ مَا يَأۡتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ
Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.
Ang mga Tafsir na Arabe:
أَلَمۡ يَرَوۡاْ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ أَنَّهُمۡ إِلَيۡهِمۡ لَا يَرۡجِعُونَ
Je, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَإِن كُلّٞ لَّمَّا جَمِيعٞ لَّدَيۡنَا مُحۡضَرُونَ
Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَءَايَةٞ لَّهُمُ ٱلۡأَرۡضُ ٱلۡمَيۡتَةُ أَحۡيَيۡنَٰهَا وَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهَا حَبّٗا فَمِنۡهُ يَأۡكُلُونَ
Na Ishara hiyo kwao ni ardhi iliyokufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo!
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَجَعَلۡنَا فِيهَا جَنَّٰتٖ مِّن نَّخِيلٖ وَأَعۡنَٰبٖ وَفَجَّرۡنَا فِيهَا مِنَ ٱلۡعُيُونِ
Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemichemi ndani yake.
Ang mga Tafsir na Arabe:
لِيَأۡكُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦ وَمَا عَمِلَتۡهُ أَيۡدِيهِمۡۚ أَفَلَا يَشۡكُرُونَ
Ili wale katika matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru?
Ang mga Tafsir na Arabe:
سُبۡحَٰنَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡأَزۡوَٰجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلۡأَرۡضُ وَمِنۡ أَنفُسِهِمۡ وَمِمَّا لَا يَعۡلَمُونَ
Ametakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyovijua.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَءَايَةٞ لَّهُمُ ٱلَّيۡلُ نَسۡلَخُ مِنۡهُ ٱلنَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظۡلِمُونَ
Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱلشَّمۡسُ تَجۡرِي لِمُسۡتَقَرّٖ لَّهَاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱلۡقَمَرَ قَدَّرۡنَٰهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَٱلۡعُرۡجُونِ ٱلۡقَدِيمِ
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe.
Ang mga Tafsir na Arabe:
لَا ٱلشَّمۡسُ يَنۢبَغِي لَهَآ أَن تُدۡرِكَ ٱلۡقَمَرَ وَلَا ٱلَّيۡلُ سَابِقُ ٱلنَّهَارِۚ وَكُلّٞ فِي فَلَكٖ يَسۡبَحُونَ
Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَءَايَةٞ لَّهُمۡ أَنَّا حَمَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُمۡ فِي ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ
Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuria zao katika jahazi lililosheheni.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَخَلَقۡنَا لَهُم مِّن مِّثۡلِهِۦ مَا يَرۡكَبُونَ
Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَإِن نَّشَأۡ نُغۡرِقۡهُمۡ فَلَا صَرِيخَ لَهُمۡ وَلَا هُمۡ يُنقَذُونَ
Na tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِلَّا رَحۡمَةٗ مِّنَّا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٖ
Isipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُواْ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيكُمۡ وَمَا خَلۡفَكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na wanapoambiwa: Jilindeni kutokana na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَمَا تَأۡتِيهِم مِّنۡ ءَايَةٖ مِّنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِمۡ إِلَّا كَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ
Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa wao huwa ni wenye kuipa mgongo.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ أَنفِقُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَنُطۡعِمُ مَن لَّوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ أَطۡعَمَهُۥٓ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Na wanapoambiwa: Toeni katika aliyokupeni Mwenyezi Mungu, wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi hammo isipokuwa katika upotofu ulio dhahiri.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?
Ang mga Tafsir na Arabe:
مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ تَأۡخُذُهُمۡ وَهُمۡ يَخِصِّمُونَ
Hawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana.
Ang mga Tafsir na Arabe:
فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ تَوۡصِيَةٗ وَلَآ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمۡ يَرۡجِعُونَ
Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ يَنسِلُونَ
Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا مَنۢ بَعَثَنَا مِن مَّرۡقَدِنَاۜۗ هَٰذَا مَا وَعَدَ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَصَدَقَ ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Watasema: Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِن كَانَتۡ إِلَّا صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَإِذَا هُمۡ جَمِيعٞ لَّدَيۡنَا مُحۡضَرُونَ
Haitakuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
فَٱلۡيَوۡمَ لَا تُظۡلَمُ نَفۡسٞ شَيۡـٔٗا وَلَا تُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ ٱلۡيَوۡمَ فِي شُغُلٖ فَٰكِهُونَ
Hakika watu wa Bustani ya mbinguni leo wamo shughulini, wamefurahi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
هُمۡ وَأَزۡوَٰجُهُمۡ فِي ظِلَٰلٍ عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ
Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya kifahari.
Ang mga Tafsir na Arabe:
لَهُمۡ فِيهَا فَٰكِهَةٞ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ
Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka.
Ang mga Tafsir na Arabe:
سَلَٰمٞ قَوۡلٗا مِّن رَّبّٖ رَّحِيمٖ
"Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱمۡتَٰزُواْ ٱلۡيَوۡمَ أَيُّهَا ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Na enyi wakosefu! Jitengeni leo!
Ang mga Tafsir na Arabe:
۞ أَلَمۡ أَعۡهَدۡ إِلَيۡكُمۡ يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعۡبُدُواْ ٱلشَّيۡطَٰنَۖ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ
Je, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَأَنِ ٱعۡبُدُونِيۚ هَٰذَا صِرَٰطٞ مُّسۡتَقِيمٞ
Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia iliyonyooka.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَلَقَدۡ أَضَلَّ مِنكُمۡ جِبِلّٗا كَثِيرًاۖ أَفَلَمۡ تَكُونُواْ تَعۡقِلُونَ
Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri?
Ang mga Tafsir na Arabe:
هَٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِي كُنتُمۡ تُوعَدُونَ
Hii basi ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
ٱصۡلَوۡهَا ٱلۡيَوۡمَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ
Ingieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.
Ang mga Tafsir na Arabe:
ٱلۡيَوۡمَ نَخۡتِمُ عَلَىٰٓ أَفۡوَٰهِهِمۡ وَتُكَلِّمُنَآ أَيۡدِيهِمۡ وَتَشۡهَدُ أَرۡجُلُهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَلَوۡ نَشَآءُ لَطَمَسۡنَا عَلَىٰٓ أَعۡيُنِهِمۡ فَٱسۡتَبَقُواْ ٱلصِّرَٰطَ فَأَنَّىٰ يُبۡصِرُونَ
Na tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje?
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَلَوۡ نَشَآءُ لَمَسَخۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمۡ فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مُضِيّٗا وَلَا يَرۡجِعُونَ
Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَكِّسۡهُ فِي ٱلۡخَلۡقِۚ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ
Na tunayemzeesha, tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je, hawazingatii?
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَمَا عَلَّمۡنَٰهُ ٱلشِّعۡرَ وَمَا يَنۢبَغِي لَهُۥٓۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ وَقُرۡءَانٞ مُّبِينٞ
Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu isipokuwa ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha.
Ang mga Tafsir na Arabe:
لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيّٗا وَيَحِقَّ ٱلۡقَوۡلُ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.
Ang mga Tafsir na Arabe:
أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّا خَلَقۡنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتۡ أَيۡدِينَآ أَنۡعَٰمٗا فَهُمۡ لَهَا مَٰلِكُونَ
Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَذَلَّلۡنَٰهَا لَهُمۡ فَمِنۡهَا رَكُوبُهُمۡ وَمِنۡهَا يَأۡكُلُونَ
Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala.
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَلَهُمۡ فِيهَا مَنَٰفِعُ وَمَشَارِبُۚ أَفَلَا يَشۡكُرُونَ
Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةٗ لَّعَلَّهُمۡ يُنصَرُونَ
Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa!
Ang mga Tafsir na Arabe:
لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَهُمۡ وَهُمۡ لَهُمۡ جُندٞ مُّحۡضَرُونَ
Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakaohudhurishwa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
فَلَا يَحۡزُنكَ قَوۡلُهُمۡۘ إِنَّا نَعۡلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعۡلِنُونَ
Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha.
Ang mga Tafsir na Arabe:
أَوَلَمۡ يَرَ ٱلۡإِنسَٰنُ أَنَّا خَلَقۡنَٰهُ مِن نُّطۡفَةٖ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٞ مُّبِينٞ
Kwani mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiyo amekuwa ndiye mgomvi wa dhahiri!
Ang mga Tafsir na Arabe:
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلٗا وَنَسِيَ خَلۡقَهُۥۖ قَالَ مَن يُحۡيِ ٱلۡعِظَٰمَ وَهِيَ رَمِيمٞ
Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?
Ang mga Tafsir na Arabe:
قُلۡ يُحۡيِيهَا ٱلَّذِيٓ أَنشَأَهَآ أَوَّلَ مَرَّةٖۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلۡقٍ عَلِيمٌ
Sema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.
Ang mga Tafsir na Arabe:
ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلشَّجَرِ ٱلۡأَخۡضَرِ نَارٗا فَإِذَآ أَنتُم مِّنۡهُ تُوقِدُونَ
Aliyekujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.
Ang mga Tafsir na Arabe:
أَوَلَيۡسَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يَخۡلُقَ مِثۡلَهُمۚ بَلَىٰ وَهُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ
Kwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi mno.
Ang mga Tafsir na Arabe:
إِنَّمَآ أَمۡرُهُۥٓ إِذَآ أَرَادَ شَيۡـًٔا أَن يَقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Hakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
فَسُبۡحَٰنَ ٱلَّذِي بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيۡءٖ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ
Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.
Ang mga Tafsir na Arabe:
 
Salin ng mga Kahulugan Surah: Yā-Sīn
Indise ng mga Surah Numero ng Pahina
 
Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin - Indise ng mga Salin

Isinalin ito ng isang pangkat ng Sentro ng Rowad sa Pagsasalin sa pakikipagtulungan ng Samahan ng Da‘wah sa Rabwah at Samahan ng Paglilingkod sa Nilalamang Islāmiko sa mga Wika.

Isara