《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 瓦格尔   段:

Surat Al-Waqi'ah

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Kitakaposimama Kiyama.
阿拉伯语经注:
لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ
Hakutakuwa na yoyote mwenye kukanusha kusimama kwake.
阿拉伯语经注:
خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ
Ni chenye kuwainamisha chini maadui wa Mwenyezi Mungu ndani ya Moto na ni chenye kuwainua juu Peponi wale wenye kumtegemea.
阿拉伯语经注:
إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا
Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.
阿拉伯语经注:
وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا
Na yakamumunyuliwa majabali mmumunyuo wa kina.
阿拉伯语经注:
فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا
Yakawa vumbi lenye kuruka angani lililosukumwa na upepo.
阿拉伯语经注:
وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ
Na mkawa, enyi viumbe, makundi matatu:
阿拉伯语经注:
فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Kundi la watu wa upande wa kulia, wenye daraja kubwa. Ni kikubwa kilioje cheo chao!
阿拉伯语经注:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Kuna na kundi la watu wa upande wa kushoto, wenye daraja duni. Ni mbaya iliyoje hali yao!
阿拉伯语经注:
وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ
Na wale waliotangulia mbele kwenye kheri duniani ndio wenye kutangulia mbele kwenye daraja za juu huko Akhera.
阿拉伯语经注:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Wao ndio walioletwa karibu kwa Mwenyezi Mungu,
阿拉伯语经注:
فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Mola wao Atawatia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe.
阿拉伯语经注:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Watayaingia watu wengi watu wa mwanzo wa ummah huu, na ummah wengineo wasiokuwa wao,
阿拉伯语经注:
وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
na wachache miongoni mwa watu mwisho wa ummah huu,
阿拉伯语经注:
عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ
wakiwa juu ya vitanda vilivyofumwa kwa dhahabu,
阿拉伯语经注:
مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ
na wakiwa katika hali ya kuvitegemea na huku wanaelekeana na kukutana.
阿拉伯语经注:
يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ
Wanawazunguka wao kuwatumikia watumishi vijana wasiozeeka wala kufa,
阿拉伯语经注:
بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ
wakiwa na vikombe, mabirika na gilasi kutoka kwenye chemchemi ya pombe yenye kupita ndani ya Pepo,
阿拉伯语经注:
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ
na hawaumwi na vichwa kutokana nayo wala hawarukwi na akili.
阿拉伯语经注:
وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
Na watawazunguka wao watumishi vijana na kila kitu wanachokichagua miongoni mwa matunda,
阿拉伯语经注:
وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
nyama ya ndege ambayo nafsi zao inavutika nayo.
阿拉伯语经注:
وَحُورٌ عِينٞ
Na watakuwa na wanawake wenye macho makubwa kama kwamba wao,
阿拉伯语经注:
كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ
kwa usafi wao na uzuri wao, ni lulu iliyohifadhiwa ndani ya mashaza yake,
阿拉伯语经注:
جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
hali hayo yakiwa ni malipo yao kwa yale waliokuwa wakiyafanya duniani.
阿拉伯语经注:
لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا
Hawatasikia humo Peponi ubatilifu wala yale ya kuwatia madhambini kuyasikia,
阿拉伯语经注:
إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا
isipokuwa maneno yasiyokuwa na kasoro hizi na kusalimiana wao kwa wao.
阿拉伯语经注:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ
Na watu wa upande wa kulia,
阿拉伯语经注:
فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ
ni kikubwa kilioje cheo chao na malipo yao!
阿拉伯语经注:
وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ
Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na ndizi zilizopandana na kupangika,
阿拉伯语经注:
وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ
kila ndizi juu ya nyingine, na vivuli vya daima visivyoondoka,
阿拉伯语经注:
وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ
na maji yanayotembea yasiyokatika,
阿拉伯语经注:
وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ
na matunda mengi
阿拉伯语经注:
لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ
yasiyomalizika wala kuwaishia wala hakuna kizuizi chochote kinachowazuia wao kuyafikia,
阿拉伯语经注:
وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ
na matandiko yaliyoinuliwa juu ya vitanda.
阿拉伯语经注:
إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ
Sisi tumewaumba wanawake wa watu wa Peponi umbile ambalo silo lile umbile lililokuwa duniani, umbile lililokamilika lisilokubali kutoweka,
阿拉伯语经注:
فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا
na tumewafanya ni wanawali wenye kujipendekeza kwa waume zao,
阿拉伯语经注:
عُرُبًا أَتۡرَابٗا
hali ya kuwa ni marika na wao kimiaka.
阿拉伯语经注:
لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Tumewaumbia wanawake hao watu wa upande wa kulia.
阿拉伯语经注:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Nao ni kundi la watu wengi wa mwanzo
阿拉伯语经注:
وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
na kundi la watu wengi wa mwisho.
阿拉伯语经注:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ
Na watu wa upande wa kushoto, ni mbaya iliyoje hali yao na malipo yao!
阿拉伯语经注:
فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ
Watakuwa kwenye upepo ulio moto utokanao na joto la Moto wa Jahanamu utakaozuia pumzi zao, na maji moto yanayochemka,
阿拉伯语经注:
وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ
na kivuli cha moshi mweusi sana,
阿拉伯语经注:
لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ
usio na mashukio baridi wala mandhari mazuri.
阿拉伯语经注:
إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ
Kwani wao walikuwa duniani wakijistarehesha kwa vitu vya haramu wakijiepusha na yale ambayo Mitume walikuja nayo.
阿拉伯语经注:
وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ
Na walikuwa wamesimama wima katika kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumshirikisha na kumuasi, na hawakuwa na nia ya kutubia kwa hayo.
阿拉伯语经注:
وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Na walikuwa wakisema hali ya kukanusha Ufufuzi, «Je hivi sisi tutafufuliwa tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa?» Maneno yao hayo yanaonesha kuwa wao walikuwa wakiliona jambo hili la kufufuliwa kuwa liko mbali na ukweli na wakilikanusha.
阿拉伯语经注:
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
«Je tutafufuliwa sisi na hali baba zetu waliotangulia wamekuwa mchanga uliotapakaa kwenye ardhi?»
阿拉伯语经注:
قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ
Sema uwaambie, «Hakika wa mwanzo na wa mwisho miongoni mwa binadamu
阿拉伯语经注:
لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
watakusanywa katika Siku iliyowekewa wakati maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama.
阿拉伯语经注:
ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ
«Kisha nyinyi, enyi mliopotea njia ya uongofu mnaokanusha onyo la Mwenyezi Mungu na agizo Lake,
阿拉伯语经注:
لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ
ni wenye kula kutokana na mti wa zaqqūm,
阿拉伯语经注:
فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ
nao ni katika miti mibaya zaidi, na ni wenye kujaza matumbo yenu kutokana nao kwa sababu ya ukali wa njaa,
阿拉伯语经注:
فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ
na ni wenye kunywa juu yake maji yaliyo moto hadi ya mwisho, yasiyomaliza kiu.
阿拉伯语经注:
فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ
Mtayanywa maji hayo kwa wingi kama vile ngamia wenye kiu wasioshiba maji kwa ugonjwa uliowapata.»
阿拉伯语经注:
هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Adhabu hii watakayoipata ndiyo zawadi Aliyowaandalia Siku ya Kiyama. Katika haya kuna kuwalaumu na kuwacheza shere.
阿拉伯语经注:
نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ
Sisi tumewaumba, enyi watu, na hamkuwa kitu chochote. Basi si msadiki kuwa kuna kufufuliwa?
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ
Mnayaonaje maji ya manii mnayoyatupa ndani ya vizazi vya wake zenu,
阿拉伯语经注:
ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
je nyinyi ndio mnaomuumba mwanadamu kutokana na hayo au ni sisi ndio wenye kuumba?
阿拉伯语经注:
نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Sisi tumekadiria kifo kwenu,
阿拉伯语经注:
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ
na sisi si wenye kushindwa kubadilisha umbo lenu Siku ya Kiyama na kuwaumba kwa sifa na namna msizozijua.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ
Na hakika mlijua kuwa Mwenyezi Mungu Aliwaumba uumbaji wa kwanza na hamkuwa kitu chochote. Basi si mkumbuke uweza wa Mwenyezi Mungu wa kuwaumba mara nyingine?
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ
Mnazionaje mbegu mnazozipanda?
阿拉伯语经注:
ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ
Je ni nyinyi mnaoziotesha kutoka ardhini? Sisi ndio tuaozituliza na kuziotesha ardhini.
阿拉伯语经注:
لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ
Lau tungalitaka tungaliifanya mimea inayotokana na mbegu hizo kuwa mapepe, haimkiniki kunufaika nayo kwa kula,
阿拉伯语经注:
إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ
mkawa mnaona ajabu kwa kilichoshukia mimea yenu na mnasema, «Sisi tumepata hasara na ni wenye kuungulika.
阿拉伯语经注:
بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ
Bali sisi tumekoseshwa riziki.»
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ
Mnayaonaje maji mnayokunywa ili mhuike kwayo?
阿拉伯语经注:
ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ
Je ni nyinyi mliyoyateremsha kutoka kwenye mawingu hadi kwenye kituo cha ardhi au ni sisi tuliyoyateremsha ili kuwarehemu nyinyi?
阿拉伯语经注:
لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ
Lau tungalitaka tungaliyafanya maji haya yawe na chumvi sana, ikiwa haiwezekani kunufaika nayo kwa kunywa wala kwa mimea. Basi si mumshukuru Mola wenu kwa kuteremsha maji tamu kwa kuwanufaisha nyinyi.
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ
Mnaouonaje moto mnaouwasha?
阿拉伯语经注:
ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ
Je ni nyinyi mlioufanya mti wake, unaozalisha moto kwa kukwaruzwa, upatikane au ni sisi tulioufanya upatikane?
阿拉伯语经注:
نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ
Sisi tumeufanya moto wenu mnaouwasha ni ukumbusho kwenu wa Moto wa Jahanamu na pia ni manufaa kwa wasafiri.
阿拉伯语经注:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi mtakase Mola wako, ewe Nabii, Aliye mtukufu Mwenye ukamilifu wa majina na sifa, Mwingi wa wema na kheri.
阿拉伯语经注:
۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mapomoko ya nyota nyakati za kuzama kwake mbinguni.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ
Nacho ni kiapo kikubwa lau mnajua kadiri yake.
阿拉伯语经注:
إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ
Hakika hii Qur’ani iliyoteremshiwa Muhammad ni Qur’ani yenye manufaa makubwa, yenye kheri nyingi na yenye elimu tele,
阿拉伯语经注:
فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ
iliyo ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa, kilichofichwa na macho ya viumbe, nacho ni Kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika.
阿拉伯语经注:
لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ
Hawaigusi Qur’ani isipokuwa malaika watukufu ambao Mwenyezi Mungu Amewasafisha na aibu na madhambi. Na pia hawaigusi isipokuwa watu waliojitohirisha na ushirikina na janaba na ukosefu wa udhu.
阿拉伯语经注:
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na hii Qur’ani tukufu imeteremshwa kutoka kwa Mola wa viumbe vyote, kwani hiyo ndiyo haki isiyo na shaka ndani yake.
阿拉伯语经注:
أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ
je hii Qur’ani, enyi washirikina, mnaikanusha?
阿拉伯语经注:
وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ
Na je mnaifanya shukrani yenu kwa neema za Mola wenu ni kuwa nyinyi mnazikanusha na kukufuru? Hapa pana makaripio kwa anayedharau amri za Qur’ani na kutojali mwito wake.
阿拉伯语经注:
فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ
Basi je mnaweza pindi roho ya mmoja wenu inapofika kwenye koo katika uchungu wa kifo,
阿拉伯语经注:
وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ
na hali nyinyi mmehudhuria mnamtazama, kuizuia roho yake ndani ya mwili wake? Hamtaweza hilo!
阿拉伯语经注:
وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ
Na sisi tuko karibu na yeye zaidi, kupitia Malaika wetu, kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuwaoni.
阿拉伯语经注:
فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ
Na je mnaweza, iwapo nyinyi si wenye kuhesabiwa wala kulipwa kwa matendo yenu,
阿拉伯语经注:
تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
kuirudisha roho kwenye mwili, iwapo nyinyi ni wakweli? Hamtaweza kuirudisha.
阿拉伯语经注:
فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Basi iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia, atapata rehema kunjufu na furaha,
阿拉伯语经注:
فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ
wakati wa kufa kwake, na kila kinachoifurahisha nafsi yake, Na atapata Pepo ya starehe huko Akhera.
阿拉伯语经注:
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Na iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia,
阿拉伯语经注:
فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
ataambiwa, «Umesalimika na kuwa kwenye amani, kwa kuwa wewe ni miongoni mwa watu wa upande wa kulia.»
阿拉伯语经注:
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ
Na iwapo yule anayekufa ni miongoni mwa wenye kukanusha kufufuliwa, waliopotoka na njia ya uongofu,
阿拉伯语经注:
فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ
basi atapata makaribisho ya kinywaji cha moto wa Jahanamu kilichochemshwa, kilicho na joto hadi ya mwisho,
阿拉伯语经注:
وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ
na atachomwa na Moto na aungulike na adhabu yake kali.
阿拉伯语经注:
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ
Hakika habari hii tumezokuelezea, ewe Mtume, ni ukweli wa yakini usio na shaka.
阿拉伯语经注:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Aliyetukuka na umtakase na yale ambayo madhalimu na wenye kukanusha wanayasema. Mwenyezi Mungu Yuko juu ya yale wanayoyasema ujuu mkubwa sana.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 瓦格尔
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。 - 译解目录

古兰经斯瓦希里文译解,阿布杜拉·穆罕默德·艾布·拜克尔博士和谢赫纳赛尔·哈米斯翻译。

关闭