《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 段: (125) 章: 艾奈尔姆
فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهۡدِيَهُۥ يَشۡرَحۡ صَدۡرَهُۥ لِلۡإِسۡلَٰمِۖ وَمَن يُرِدۡ أَن يُضِلَّهُۥ يَجۡعَلۡ صَدۡرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجٗا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي ٱلسَّمَآءِۚ كَذَٰلِكَ يَجۡعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجۡسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumhidi humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na anaye taka apotee hukifanya kifua chake kina dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda mbinguni. Namna hivi Mwenyezi Mungu anajaalia uchafu juu ya wasio amini.
Ikiwa hao wamepotea, na nyinyi mkaongoka, basi ni kwa kutaka Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa hukumu yake. Aliye muandikia hidaya humkunjulia kifua chake kwa nuru ya Uislamu. Na aliye muandikia kupotea kifua chake huwa na dhiki ya kweli kweli, kama kinavyo mbana kifua mwenye kupanda pahala pa juu, kama vile mbinguni. Pumzi humpaa, asiweze kitu! Na kwa hivi Mwenyezi Mungu huwaandikia ufisadi na kukatika tamaa hao ambao hawakujaaliwa kuwa na Imani katika shani yao. Masomo ya ilimu za sayansi yamethibitisha kuwa mwanaadamu kila akipanda juu kunadhoofika kuvuta pumzi kwake kwa pua. Mpaka akifika mnyanyuka wa futi 12,000 huwa hawezi kuvuta kwa pua, na huvuta pumzi kwa mdomo. Na hivyo huvuta kwa shida, na akifanya juhudi yoyote ya nguvu huzidi taabu ya kuvuta pumzi. Na hata kusema humletea shida katika pumzi.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 段: (125) 章: 艾奈尔姆
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭