《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 段: (19) 章: 艾奈尔姆
قُلۡ أَيُّ شَيۡءٍ أَكۡبَرُ شَهَٰدَةٗۖ قُلِ ٱللَّهُۖ شَهِيدُۢ بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانُ لِأُنذِرَكُم بِهِۦ وَمَنۢ بَلَغَۚ أَئِنَّكُمۡ لَتَشۡهَدُونَ أَنَّ مَعَ ٱللَّهِ ءَالِهَةً أُخۡرَىٰۚ قُل لَّآ أَشۡهَدُۚ قُلۡ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ وَإِنَّنِي بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ
Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha.
Ewe Nabii! Waambie hao wanao kukanusha na wanao taka ushahidi wa Utume wako: Kitu gani chenye ushahidi mkubwa, na chenye kustahiki kusadikiwa kuliko vyote? Kisha uwambie: Hakika Mwenyezi Mungu ndiye shahidi mkubwa kushinda wote wa kushuhudia baina yangu na nyinyi katika ukweli wa haya ninayo kuleteeni. Na Yeye ndiye aliye iteremsha hii Qur'ani ili iwe ni hoja ya ukweli wangu, nipate kukuhadharisheni nyinyi na kila itakayo mfikia khabari yake. Nayo ni hoja ya kukata, inayo shuhudia ukweli wangu. Kwani nyinyi hamwezi kuleta mfano wake! Waulize: Hivyo nyinyi mnaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu ana miungu wenziwe? Kisha uwambie: Mimi sishuhudii hayo, wala sisemi hivyo, wala sikukubalieni kwa hayo. Hapana shaka wa kuabudiwa kwa haki ni Mungu Mmoja. Na mimi ni mbali kabisa na hayo masanamu mnayo mshirikisha Naye.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 段: (19) 章: 艾奈尔姆
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭