《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 章: 奈扎尔提   段:

Surat An-Nazi'at

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا
Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu!
Ninaapa kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuving'oa vitu kutokana na pahala pao kwa nguvu,
阿拉伯语经注:
وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا
Na kwa wanao toa kwa upole!
Na kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuvitoa vitu kwa utaratibu na ulaini,
阿拉伯语经注:
وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا
Na wanao ogelea!
Na kwa kila kilicho pewa mbio za kutekeleza kazi yake kwa sahala na wepesi.
阿拉伯语经注:
فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا
Wakishindana mbio!
Na kwa vinavyo shindania kutimiza waajibu ulio twikwa juu yao kushindania kwa juhudi,
阿拉伯语经注:
فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا
Wakidabiri mambo.
Na vinavyo dabiri, kupanga, mambo na kuyaendesha kwa mujibu wa vilivyo khusishwa,
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ
Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka!
Bila ya shaka Saa ya Kiyama itafika; hiyo siku ambayo mpulizo wa mwanzo wa barugumu utavitikisa viumbe vyote,
阿拉伯语经注:
تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ
Kifuate cha kufuatia.
Na mpulizo huo utafuatiwa na wa pili ambao ndio utakao kuwa wa kufufuliwa watu.
阿拉伯语经注:
قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ
Siku hiyo nyoyo zitapiga piga!
Siku hiyo nyoyo zitapapatika kwa khofu.
阿拉伯语经注:
أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ
Macho yatainama chini!
Macho ya watu yatakuwa na huzuni, manyonge.
阿拉伯语经注:
يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ
Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza?
Watu hawa husema duniani kwa kukanya kufufuliwa: Ati tutarudishwa sisi baada ya kwisha kufa, tuumbwe tena kama tulivyo kuwa?
阿拉伯语经注:
أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ
Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa?
Tukisha kuwa mafupa yaliyo chakaa, ati tutarejeshwa tufufuliwe upya?
阿拉伯语经注:
قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ
Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara!
Wanasema, kwa kukanya na kejeli: Kurejea huko kama kukitokea basi ni marejeo ya khasara, na sisi si watu wa kukhasiri.
阿拉伯语经注:
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ
Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu,
Msidhani kurejea huko ni kuzito. Kwani hayo ni ukelele mmoja tu,
阿拉伯语经注:
فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ
Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano!
Mara maiti wote watahudhurishwa kwenye ardhi ya mkusanyiko!
阿拉伯语经注:
هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Je! Imekufikia hadithi ya Musa?
Ewe Muhammad! Imekufikilia hadithi ya Musa,
阿拉伯语经注:
إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى
Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia:
Alipo mwita Mola wake Mlezi katika bonde lilio takaswa, linalo itwa "T'uwa"?
阿拉伯语经注:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri
Akaambiwa: Nenda kwa Firauni aliye pindukia mpaka katika udhalimu.
阿拉伯语经注:
فَقُلۡ هَل لَّكَ إِلَىٰٓ أَن تَزَكَّىٰ
Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa?
Umwambie: Je! Huelekei kut'ahirika?
阿拉伯语经注:
وَأَهۡدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخۡشَىٰ
Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha.
Na mimi nikuongoze upate kumjua Mola wako Mlezi, umwogope.
阿拉伯语经注:
فَأَرَىٰهُ ٱلۡأٓيَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi alimwonyesha Ishara kubwa.
Musa akamwonyesha Firauni miujiza mikubwa.
阿拉伯语经注:
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ
Lakini aliikadhibisha na akaasi.
Lakini Firauni alimkadhibisha Musa kwa aliyo kuja nayo, na akamuasi kwa aliyo mwitia.
阿拉伯语经注:
ثُمَّ أَدۡبَرَ يَسۡعَىٰ
Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi.
Kisha akamgeuzia mgongo, akenda kujitahidi kumpinga.
阿拉伯语经注:
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ
Akakusanya watu akanadi.
Akawakusanya wachawi, na akawaita watu,
阿拉伯语经注:
فَقَالَ أَنَا۠ رَبُّكُمُ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa.
Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi aliye mkubwa kabisa.
阿拉伯语经注:
فَأَخَذَهُ ٱللَّهُ نَكَالَ ٱلۡأٓخِرَةِ وَٱلۡأُولَىٰٓ
Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo.
Mwenyezi Mungu akampa adhabu kwa kauli yake ya mwisho, nayo ni vile kusema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi aliye mkubwa kabisa. Na akampa adhabu kwa kauli yake ya mwanzo, nayo ni kumkadhibisha Musa a.s.
阿拉伯语经注:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰٓ
Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa.
Hakika katika hadithi hiyo yapo mawaidha kwa mwenye kumkhofu Mwenyezi Mungu.
阿拉伯语经注:
ءَأَنتُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَمِ ٱلسَّمَآءُۚ بَنَىٰهَا
Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga!
Enyi mnao kanya kufufuliwa! Kukuumbeni nyinyi ni taabu zaidi au kuziumba mbingu, kuzikusanya sehemu zake zilio tawanyika mbali mbali,
阿拉伯语经注:
رَفَعَ سَمۡكَهَا فَسَوَّىٰهَا
Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri.
Na kunyanyua kimo chake, na zikakaa sawa hazina tafauti wala ila?
阿拉伯语经注:
وَأَغۡطَشَ لَيۡلَهَا وَأَخۡرَجَ ضُحَىٰهَا
Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake
Na akatia kiza katika usiku wake, na akautokeza mchana wake ukawa na mwangaza?
阿拉伯语经注:
وَٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ ذَٰلِكَ دَحَىٰهَآ
Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi.
Na ardhi baada ya hayo akaikunjua, na akaisawazisha, ikasilihi kukaliwa na watu wake?
阿拉伯语经注:
أَخۡرَجَ مِنۡهَا مَآءَهَا وَمَرۡعَىٰهَا
Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake,
Akatoa ndani yake maji yake yanayo tibuka katika chemchem zake, na ikamiminika mito yake, na ikawa na mimea yake ya chakula kwa ajili ya watu na wanyama;
阿拉伯语经注:
وَٱلۡجِبَالَ أَرۡسَىٰهَا
Na milima akaisimamisha,
Na milima akaithibitisha imara
阿拉伯语经注:
مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Kwa nafuu yenu na mifugo yenu.
Kwa ajili ya manufaa yenu na wanyama wenu mnao wafuga!
阿拉伯语经注:
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلطَّآمَّةُ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
Kitakapo fika Kiyama ambacho vitisho vyake vitaenea kote,
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا سَعَىٰ
Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya,
Siku atakapo kumbuka mtu vitendo vyake vya kheri au shari,
阿拉伯语经注:
وَبُرِّزَتِ ٱلۡجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ
Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona,
Na Jahannamu ikadhihirishwa wazi, akaiona kila mwenye macho kuwa ndio malipo,
阿拉伯语经注:
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ
Basi ama yule aliye zidi ujeuri,
Basi ama mwenye kupita mpaka kwa maasi yake,
阿拉伯语经注:
وَءَاثَرَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Na akakhiari maisha ya dunia,
Na akajichagulia nafsi yake maisha yanayo pita njia,
阿拉伯语经注:
فَإِنَّ ٱلۡجَحِيمَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake!
Basi Moto wa Jahannamu unao babua upepo wake ndio makaazi yake wala hana mengineyo.
阿拉伯语经注:
وَأَمَّا مَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ وَنَهَى ٱلنَّفۡسَ عَنِ ٱلۡهَوَىٰ
Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio,
Na ama mwenye kukhofu ukubwa na utukufu wa Mola wake Mlezi, na akaizuia nafsi yake na matamanio ya kumpumbaza,
阿拉伯语经注:
فَإِنَّ ٱلۡجَنَّةَ هِيَ ٱلۡمَأۡوَىٰ
Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!
Basi huyo nyumba ya neema ya Peponi ndio makaazi yake, wala hana penginepo.
阿拉伯语经注:
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَا
Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini?
Ewe Muhammad! Wanakuuliza, ati, khabari za Saa ya Kiyama, itakuwa lini?
阿拉伯语经注:
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكۡرَىٰهَآ
Una nini wewe hata uitaje?
Ujuzi wa hayo hauko kwako hata uwatajie.
阿拉伯语经注:
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَىٰهَآ
Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake.
Ujuzi wa hayo uko kwa Mola wako Mlezi tu, si kwa mwenginewe. (Nabii Isa a.s. ambaye Wakristo wanasema ni Mwana wa Mungu, au ndiye Mungu, pia anasimuliwa katika Biblia kuwa hakuijua Saa na Siku ya Kiyama. Injili ya Mathayo inanukulu maneno ya Yesu: "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.")
阿拉伯语经注:
إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخۡشَىٰهَا
Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu.
Kwani waajibu wako ni kuwaonya wanao khofu si kuwatangazia wakati wake.
阿拉伯语经注:
كَأَنَّهُمۡ يَوۡمَ يَرَوۡنَهَا لَمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا عَشِيَّةً أَوۡ ضُحَىٰهَا
Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake.
Na wao siku watakayo iona hiyo Saa ya Kiyama ni kama kwamba hawakuishi duniani zaidi kuliko jioni moja tu, au mchana wake.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 奈扎尔提
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭