《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 章: 塔拉格   段:

Surat Al-Alaq

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba!
Ewe Muhammad! Soma unayo funuliwa kwa kufunguliwa kwa Jina la Mola wako Mlezi ambaye ni Yeye tu peke yake ndiye Mwenye uweza wa kuumba.
阿拉伯语经注:
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu!
Amemuumba mtu kwa ukamilifu wa mwili wake na ilimu kutokana na kipande cha damu ambacho hakina chochote cha kupelekea kujiona bora.
阿拉伯语经注:
ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
Endelea na kusoma, na Mola wako Mlezi aliye Karimu kushinda wote, atakutukuza wala hatakudharau.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ
Ambaye amefundisha kwa kalamu.
Yeye ndiye ambaye aliye mfunza mtu kuandika kwa kalamu, na wala kwanza hakuwa anajua hayo.
阿拉伯语经注:
عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
Amemfunza mtu yasiyo kuwa yanampitia katika mawazo yake.
阿拉伯语经注:
كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ
Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri.
Ni hakika kweli mtu hupindukia mpaka na hupanda kiburi mbele ya Mola wake Mlezi
阿拉伯语经注:
أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ
Akijiona katajirika.
Anapo jiona si mhitaji, katajirika.
阿拉伯语经注:
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ
Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
Ewe Muhammad! Hakika ni kwa Mola wako Mlezi peke yake ndiyo yako marejeo ya wote kwa kufufuliwa na kulipwa.
阿拉伯语经注:
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ
Umemwona yule anaye mkataza.
Je! Umemwona huyu jeuri
阿拉伯语经注:
عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ
Mja anapo sali?
Anaye mzuia mja asisali anapo taka kusali?
阿拉伯语经注:
أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ
Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
Hebu niambie khabari za jeuri huyu kama yeye yumo katika uwongofu katika huku kuzuia kwake,
阿拉伯语经注:
أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ
Au anaamrisha uchamngu?
Au kwamba ndio anaamrisha uchamngu katika hayo anayo amrisha!
阿拉伯语经注:
أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ
Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
Niambie khabari za huyu mwenye kukataza anapo yakadhibisha aliyo kuja nayo Mtume, na akapuuza Imani na vitendo vyema!
阿拉伯语经注:
أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ
Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
Hivyo hajui kwamba Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zake, naye atamlipa kwazo?
阿拉伯语经注:
كَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
Kwa kumkemea huyu mwenye kuzuia, anaambiwa kama hakuacha hayo anayo yafanya, basi hapana shaka tutamkokota kwa nguvu tukimshika kwa shungi lake la nywele mpaka Motoni!
阿拉伯语经注:
نَاصِيَةٖ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٖ
Shungi la uwongo, lenye makosa!
Hilo shungi lilio juu ya uso wake mwenye kuropokwa uwongo na mwenye athari za ukosefu!
阿拉伯语经注:
فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ
Basi na awaite wenzake!
Basi yeye awaite wenziwe na watu wa baraza lake wawe ndio wasaidizi duniani au Akhera.
阿拉伯语经注:
سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ
Nasi tutawaita Mazabania!
Sisi tutawaita askari wetu wamsaidie Muhammad na walio pamoja naye, na wapambane na huyo mwenye kukanya na wasaidizi wawasukume kwenye Jahannamu!
阿拉伯语经注:
كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!
Kumnyamazisha huyu mwenye kuzuia, wewe usimkubalie kwa hayo anayo kukataza nayo, na dumu juu ya Swala zako, na endelea na sijida zako, na jijongeze kwa Mola wako Mlezi kwa hivyo.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 塔拉格
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭