《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 * - 译解目录

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

含义的翻译 章: 盖德尔   段:

Surat Al-Qadr

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.
阿拉伯语经注:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ
Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?
阿拉伯语经注:
لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٞ مِّنۡ أَلۡفِ شَهۡرٖ
Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu, ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.
阿拉伯语经注:
تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ
Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.
阿拉伯语经注:
سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ
Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 盖德尔
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译-阿里·穆哈森·伯瓦尼 - 译解目录

古兰经斯瓦希里语译解,阿里·穆哈森·伯瓦尼翻译

关闭