Alif Laam Raa.[1] Hizo ni Aya za Kitabu chenye hekima.[1]
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Je, imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemfunulia mwanamume kutokana nao kuwa, “Waonye watu, na wabashirie wale walioamini ya kuwa wana cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi?” Wakasema makafiri, “Hakika huyu ni mchawi aliye dhahiri!”
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, kisha akainuka juu ya Kiti cha Enzi, anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je, hamkumbuki?
Kwake Yeye tu ndiyo marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru, wana vinywaji vya maji ya moto, na adhabu chungu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyakufuru.
Yeye ndiye aliyelifanya jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo isipokuwa kwa haki. Anazipambanua Ishara kwa kaumu wanaojua.
Wito wao humo utakuwa, “Subhanaka Allahumma (Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!)." Na maamkizi yao humo ni "Salama." Na mwisho wa wito wao ni, “Alhamdulillahi Rabbil 'aalamiin (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote)."
Na lau kama Mwenyezi Mungu angeliwafanyia watu haraka kuwaletea maovu kama wanavyojiharakishia kuletewa heri, basi bila ya shaka wangelikwishatimiziwa muda wao. Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao.
Na mtu akiguswa na shida, hutuomba naye ameegesha ubavu, au amekaa au amesimama. Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda.
Na hakika tuliviangamiza vizazi vya kabla yenu walipodhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini. Hivyo ndivyo tunavyowalipa kaumu wahalifu.
Sema, “Mwenyezi Mungu angelitaka, nisingeliwasomea, wala nisingelikuwa mwenye kukijua zaidi yenu. Kwani nilikwishakaa miongoni mwenu umri mzima kabla yake! Kwani, hamtii akilini?”
Nao wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema, “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!” Sema, “Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka mbali na hao wanaomshirikisha nao.”
Na watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu, kisha wakahitilafiana. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, hakuna shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika yale wanayohitilafiana.
Na wanasema, “Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?” Sema, “Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.”
Na tunapowaonjesha watu rehema baada ya shida iliyowagusa, tazama, wanafanya njama katika Ishara zetu. Sema, “Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa kupanga njama. Hakika wajumbe wetu wanayaandika hayo mnayoyapangia njama.”
Yeye ndiye anayewaendesha katika nchi kavu na baharini. Mpaka mnapokuwa katika majahazi na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri na wakaufurahia, upepo mkali ukayajia, na yakawajia mawimbi kutokea kila mahali, na wakaona kwamba wameshazingirwa, basi hapo wanamwomba Mwenyezi Mungu kwa kumpwekeshea yeye tu dini, “Ukituokoa kutokana na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.”
Lakini anapowaokoa, tazama, wanafanya jeuri tena katika ardhi bila ya haki. Enyi watu! Hakika jeuri zenu zitawadhuru nyinyi wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu. Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Hakika mfano wa uhai wa dunia hii ni kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi ikachanganyika nayo miongoni mwa vile wanavyovila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana. Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu kwa kaumu wanaotafakari.
Na wale waliochuma mabaya, malipo ya baya ni kwa mfano wake, na watafunikwa na madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao ni kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni. Wao, humo watadumu.
Na siku tutakapowakusanya wote, kisha tutawaambia wale walioshirikisha, "Simameni mahali penu nyinyi na washirika wenu." Kisha tutatenganisha baina yao. Na hao washirika wao watasema, "Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.
Sema, "Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini? Au ni nani anayemiliki kusikia na kuona? Na ni nani atoaye kilicho hai kutoka kwa maiti, na atoaye maiti kutoka kwa kilicho hai? Na ni nani anayeyaendesha mambo yote?" Basi watasema, "Mwenyezi Mungu." Basi sema, "Je, hamchi?"
Sema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe, kisha akavirejesha? Sema: Mwenyezi Mungu anaanzisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha. Basi ni vipi mnadanganywa?
Sema, "Je, yupo yeyote katika washirika wenu mwenye kuongoa kwenye haki?" Sema, "Mwenyezi Mungu anaongoa kwenye haki." Basi, je, yule anayeongoa kwenye haki anastahiki zaidi kufuatwa au yule asiyeongoka isipokuwa akiongozwa? Basi nyinyi mna nini, mnahukumu namna gani?
Na haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini ni usadikisho wa yale yaliyoitangulia, na ni maelezo ya kina ya Kitabu kisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Bali waliyakadhibisha yale wasiyoyaelewa elimu yake vyema kabla hayajawajia maelezo yake. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao.
Na wakikukadhibisha, basi sema, "Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi mko mbali sana na yale ninayoyatenda, nami niko mbali sana na mnayoyatenda."
Na Siku atakapowakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa isipokuwa saa moja tu katika mchana! Watatambuana. Hakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuongoka.
Na ima tutakuonyesha baadhi ya yale tunayowaahidi, au tukufishe kabla yake, basi marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayoyafanya.
Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao waliowekewa. Ukifika muda wao, hawakawii hata saa moja wala hawatangulii.
Na lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilichomo katika ardhi, basi bila ya shaka ingejikomboa kwavyo. Na watakapoiona adhabu, wataficha majuto. Na itahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa.
Jueni kuwa hakika ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao hawajui.
Sema: Je, mnaonaje yale aliyowateremshia Mwenyezi Mungu katika riziki, basi mkafanya katika hizo nyingine haramu na nyingine halali. Sema, "Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?"
Na ni nini dhana ya wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uongo Siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.
Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani, wala hamtendi kitendo chochote isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kibainifu.
Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na wala hawafuati hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu washirika wowote. Wao hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawasemi isipokuwa uongo.
Walisema, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana." Ametakasika! Yeye ndiye asiyehitajia kitu. Ni vyake vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Je, mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua?
Na wasomee habari za Nuhu alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.
Lakini wakamkadhibisha. Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio waliobakia, na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa.
Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa kaumu zao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake. Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka.
Basi walipotupa, Musa akasema, "Mliyoleta ndiyo uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu ataubatilisha. Hakika Mwenyezi Mungu hayatengenezi matendo ya waharibifu.
Basi hawakumwamini Musa isipokuwa baadhi ya vijana kutoka kwa kaumu yake, kwa kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri katika ardhi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa waliopita kiasi.
Na tukamteremshia ufunuo (wahyi) Musa na ndugu yake kuwa: Watengenezeeni majumba kaumu yenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndimo mahali pa ibada, na mdumishe Swala, na wape habari njema Waumini.
Na Musa akasema: Mola wetu Mlezi! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake mapambo na mali katika uhai wa dunia. Hivyo wanapoteza watu kutoka kwa njia yako. Mola wetu Mlezi! Zifutilie mbali mali hizo na zifunge nyoyo zao, wasiamini mpaka waione adhabu chungu.
Tukawavusha bahari Wana wa Israili, naye Firauni na askari wake wakawafuata kwa dhuluma na uadui. Mpaka kuzama kulipomfikia, akasema: Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu.
Na hakika tuliwaandalia Wana wa Israili makao mema, na tukawaruzuku katika vitu vizuri. Nao hawakuhitilafiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.
Na ikiwa uko katika shaka juu ya yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwishakujia haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Basi kwa nini haukuwepo mji ulioamini, kwa hivyo Imani yake ikaufaa, isipokuwa kaumu ya Yunus? Walipoamini, tukawaondolea adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia, na tukawastarehesha kwa muda.
Basi, je, wanangojea kingine isipokuwa kama yale yaliyotokea siku za watu waliopita kabla yao? Sema: Ngojeni! Nami hakika ni pamoja nanyi katika wanaongoja.
Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mko katika shaka juu ya Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnaowaabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namwabudu Mwenyezi Mungu anayewafisha. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waumini.
Na Mwenyezi Mungu akikugusa kwa madhara, basi hakuna wa kukuondolea isipokuwa Yeye. Na akikutakia heri, basi hakuna wa kurudisha fadhila yake. Humsibu kwayo amtakaye katika waja wake, na Yeye ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Sema: Enyi watu! Haki imekwishawajia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, anayeongoka, basi anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea, basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
搜索结果:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".