Basi kwa sababu ya kuvunja kwao agano zao, na kuzikufuru kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu ameziziba kwa kufuru zao, basi hawaamini isipokuwa kidogo tu.
Na kusema kwao: Hakika, sisi tulimuua Masihi Isa, mwana wa Maryam, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nao hawakumuua wala hawakumsulubisha, bali walifananishiwa tu. Na hakika wale waliohitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana elimu yoyote nayo isipokuwa ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuua kwa yakini.
Na hawi katika Watu wa Kitabu isipokuwa hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Qiyama atakuwa shahidi juu yao.[1]
[1] Aya hii inamaanisha kwamba kila mtu miongoni mwa Watu waliopewa Kitabu kama vile Wayahudi na Wakristo kabla ya kufa kwake humwamini Isa (Yesu) kwamba ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kwamba ni Mungu wala mototo wa Mungu. Kwani wakati anapokufa, huonyeshwa uhakika wa jambo hili. Kisha Siku ya Kiyama, Isa (Yesu) atakuwa shahidi dhidi yao kwamba aliwafikishia wito wa Mola wao Mlezi, lakini wakaupuuza na kwamba Wakristo waliubadilisha. (Tafsir At-Tahriir wat-Tanwiir, cha Ibn 'Aashuur)
Basi kwa sababu ya dhuluma ya wale waliotubu na kumrudia Mwenyezi Mungu (yani Mayahudi), tuliwaharimishia vitu vizuri walivyohalalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu.
Lakini waliobobea katika elimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini yale yaliyoteremshwa juu yako, na yale yaliyoteremshwa kabla yako. Na wanaosimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, hao tutawapa malipo makubwa.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
搜索结果:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".