Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 杜哈尼   段:

Ad-Dukhan

حمٓ
Ha Mim
阿拉伯语经注:
وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ
Ninaapa kwa Kitabu kinachobainisha.
阿拉伯语经注:
إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
Hakika Sisi tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
阿拉伯语经注:
فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ
Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima.
阿拉伯语经注:
أَمۡرٗا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ
Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
阿拉伯语经注:
رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ
Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
阿拉伯语经注:
رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
阿拉伯语经注:
لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
阿拉伯语经注:
بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ يَلۡعَبُونَ
阿拉伯语经注:
فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٖ مُّبِينٖ
Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri.
阿拉伯语经注:
يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٞ
Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu!
阿拉伯语经注:
رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ
Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
阿拉伯语经注:
أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مُّبِينٞ
Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
阿拉伯语经注:
ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمٞ مَّجۡنُونٌ
Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.'
阿拉伯语经注:
إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ
Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
阿拉伯语经注:
۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٞ كَرِيمٌ
阿拉伯语经注:
أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Akasema: 'Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
阿拉伯语经注:
وَأَن لَّا تَعۡلُواْ عَلَى ٱللَّهِۖ إِنِّيٓ ءَاتِيكُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٖ
Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
阿拉伯语经注:
وَإِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمۡ أَن تَرۡجُمُونِ
Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
阿拉伯语经注:
وَإِن لَّمۡ تُؤۡمِنُواْ لِي فَٱعۡتَزِلُونِ
Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.'
阿拉伯语经注:
فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَٰٓؤُلَآءِ قَوۡمٞ مُّجۡرِمُونَ
Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: 'Hakika watu hawa ni wakosefu.'
阿拉伯语经注:
فَأَسۡرِ بِعِبَادِي لَيۡلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
Mwenyezi Mungu akasema: 'Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
阿拉伯语经注:
وَٱتۡرُكِ ٱلۡبَحۡرَ رَهۡوًاۖ إِنَّهُمۡ جُندٞ مُّغۡرَقُونَ
Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.'
阿拉伯语经注:
كَمۡ تَرَكُواْ مِن جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ
Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha!
阿拉伯语经注:
وَزُرُوعٖ وَمَقَامٖ كَرِيمٖ
Na mimea na vyeo vitukufu!
阿拉伯语经注:
وَنَعۡمَةٖ كَانُواْ فِيهَا فَٰكِهِينَ
Na neema walizokuwa wakijistareheshea!
阿拉伯语经注:
كَذَٰلِكَۖ وَأَوۡرَثۡنَٰهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ
Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.
阿拉伯语经注:
فَمَا بَكَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَا كَانُواْ مُنظَرِينَ
Basi mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ نَجَّيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ
Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,
阿拉伯语经注:
مِن فِرۡعَوۡنَۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيٗا مِّنَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.
阿拉伯语经注:
وَلَقَدِ ٱخۡتَرۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ عِلۡمٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.
阿拉伯语经注:
وَءَاتَيۡنَٰهُم مِّنَ ٱلۡأٓيَٰتِ مَا فِيهِ بَلَٰٓؤٞاْ مُّبِينٌ
Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
阿拉伯语经注:
إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ
Hakika hawa wanasema:
阿拉伯语经注:
إِنۡ هِيَ إِلَّا مَوۡتَتُنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُنشَرِينَ
'Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
阿拉伯语经注:
فَأۡتُواْ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.'
阿拉伯语经注:
أَهُمۡ خَيۡرٌ أَمۡ قَوۡمُ تُبَّعٖ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Je, ni wao bora au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
阿拉伯语经注:
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo.
阿拉伯语经注:
مَا خَلَقۡنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
阿拉伯语经注:
إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ مِيقَٰتُهُمۡ أَجۡمَعِينَ
Hakika siku ya Uamuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ لَا يُغۡنِي مَوۡلًى عَن مَّوۡلٗى شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
阿拉伯语经注:
إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Isipokuwa atakayemrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno.
阿拉伯语经注:
إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ
Hakika Mti wa Zaqqum
阿拉伯语经注:
طَعَامُ ٱلۡأَثِيمِ
Ni chakula cha mwenye dhambi.
阿拉伯语经注:
كَٱلۡمُهۡلِ يَغۡلِي فِي ٱلۡبُطُونِ
Kama shaba iliyoyeyushwa, hutokota matumboni.
阿拉伯语经注:
كَغَلۡيِ ٱلۡحَمِيمِ
Kama kutokota kwa maji ya moto.
阿拉伯语经注:
خُذُوهُ فَٱعۡتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ
(Itasemwa): 'Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
阿拉伯语经注:
ثُمَّ صُبُّواْ فَوۡقَ رَأۡسِهِۦ مِنۡ عَذَابِ ٱلۡحَمِيمِ
Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayochemka.'
阿拉伯语经注:
ذُقۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡكَرِيمُ
Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
阿拉伯语经注:
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمۡتَرُونَ
Hakika haya ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka.
阿拉伯语经注:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٖ
Hakika wacha Mungu watakuwa katika mahali pa amani.
阿拉伯语经注:
فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ
Katika mabustani na chemchemi.
阿拉伯语经注:
يَلۡبَسُونَ مِن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَقَٰبِلِينَ
Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana.
阿拉伯语经注:
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ
Hivi ndivyo itakavyokuwa, na tutawaoza mahurilaini.
阿拉伯语经注:
يَدۡعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ
Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
阿拉伯语经注:
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلۡمَوۡتَ إِلَّا ٱلۡمَوۡتَةَ ٱلۡأُولَىٰۖ وَوَقَىٰهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ
Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu.
阿拉伯语经注:
فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
阿拉伯语经注:
فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ
Basi tumeifanya nyepesi hii Qur-ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
阿拉伯语经注:
فَٱرۡتَقِبۡ إِنَّهُم مُّرۡتَقِبُونَ
Ngoja tu, na wao wangoje pia.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 杜哈尼
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭