የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የ እስዋሂሊ ቋንቋ ትርጉም - በአብደላህ ሙሀመድ ናስር ከሚስ * - የትርጉሞች ማዉጫ


የይዘት ትርጉም ምዕራፍ: ሱረቱ ሙሀመድ   አንቀጽ:

Surat Muhammad

ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ أَضَلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Wale waliokataa kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Peke Yake Mungu wa kweli Asiye na mshirika, na wakawazuia watu na Dini Yake, Mwenyezi Mungu Atazifuta amali zao na kuzipomosha na Atawapa usumbufu kwa sababu ya amali zao hizo.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٖ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡ كَفَّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ
Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakafuata Sheria Zake na wakaamini Kitabu Alichomteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, nacho ndio ukweli usiokuwa na shaka kutoka kwa Mola wao, Mwenyezi Mungu Atawasamehe na Atawafinikia maovu waliyoyafanya na hatawatesa kwa maovu hayo na Atawatengezea mambo yao duniani na Akhera.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡبَٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡحَقَّ مِن رَّبِّهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمۡثَٰلَهُمۡ
Kupoteza huko na kuongoza, sababu yake ni kwamba wale waliokufuru wamemfuata Shetani wakamtii, na kwamba wale walioamini walimfuata Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo ya mwangaza na uongofu. Kama Alivyobainisha Mwenyezi Mungu vile Anavyoyafanya mapote mawili ya watu wa ukafiri na watu wa Imani kwa wanavyostahili, vilevile Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Anawapigia watu mifano yao, ili kila watu wanaofanana wa aina moja wakutamane na wale wanaonasibiana nao.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَإِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَضَرۡبَ ٱلرِّقَابِ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَثۡخَنتُمُوهُمۡ فَشُدُّواْ ٱلۡوَثَاقَ فَإِمَّا مَنَّۢا بَعۡدُ وَإِمَّا فِدَآءً حَتَّىٰ تَضَعَ ٱلۡحَرۡبُ أَوۡزَارَهَاۚ ذَٰلِكَۖ وَلَوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَٱنتَصَرَ مِنۡهُمۡ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَاْ بَعۡضَكُم بِبَعۡضٖۗ وَٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Basi mkipambana, enyi Waumini, na wale waliokufuru katika viwanja vya vita, piganeni nao kidhati na mzipige shingo zao. Hata mtakapowadhoofisha kwa kuwaua kwa wingi na mkazivunja nguvu zao, wafungeni kisawasawa wale mnaowateka. Kisha basi ima muwasamehe kwa kuwafungua na kuwaacha bila kutoa fidia badala yake, au wajikomboe kwa kutoa fidia, au watiwe utumwani au wauawe. Na endeleeni kufanya hivyo mpaka vita vimalizike. Hiyo ndiyo hukumu iliyotajwa ya kuwatahini Waumini kwa makafiri na ushindi kuzunguka baina yao. Na lau Mwenyezi Mungu Angalitaka wangalipata ushindi Waumini bila ya vita, lakini Mwenyezi Mungu Amejaalia mateso yao yawe mikononi mwenu ndipo Akaweka sheria ya jihadi ili Awajaribu nyinyi kwa wao na Ainusuru kwa sababu yenu Dini Yake. Na wale Waumini waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, Hatayapomosha Mwenyezi Mungu malipo mema ya matendo yao.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
سَيَهۡدِيهِمۡ وَيُصۡلِحُ بَالَهُمۡ
Atawaafikia siku za uhai wao duniani wawe watiifu Kwake na wafanye matendo ya kumridhi, Awatengeze hali zao, mambo yao na malipo mema yao duniani na Akhera,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَيُدۡخِلُهُمُ ٱلۡجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمۡ
na Awatie Peponi ambayo Aliwajulisha na Akawasifia, na Akawaafikia kusimama kuyafanya yale Ailyowaamrisha, na miongoni mwayo ni kufa shahidi katika njia Yake, kisha atawajulisha wao mashukio yao huko Peponi watakapoingia humo.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَنصُرُواْ ٱللَّهَ يَنصُرۡكُمۡ وَيُثَبِّتۡ أَقۡدَامَكُمۡ
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, mkiinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kuhukumu kwa Kitabu Chake na kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, Mwenyezi Mungu Atawapa ushindi juu ya maadui zenu na Atazithibitisha nyayo zenu wakati wa kupigana.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَتَعۡسٗا لَّهُمۡ وَأَضَلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Na wale waliokanusha, basi maangamivu ni yao, na Mwenyezi Mungu Atazifuta thawabu za matendo yao mema.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَرِهُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Hayo ni kwa sababu wao walikichukia Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilichoteremshwa kwa Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakakikanusha, na Mwenyezi Mungu akayatangua matendo yao kwa kuwa yalikuwa katika kumtii Shetani.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
۞ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ دَمَّرَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۖ وَلِلۡكَٰفِرِينَ أَمۡثَٰلُهَا
Kwani hawakwenda makafiri hawa kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu wakayazingatia yale yaliyowapata ummah waliopita ya mateso? Mwenyezi Mungu Aliyavunjavunja majumba yao. Na makafiri hawa watakuwa na mwisho kama huo uliowafikia ummah hao.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ مَوۡلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَأَنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ لَا مَوۡلَىٰ لَهُمۡ
Hilo tulilowafanyia watu wa mapote mawili: pote la Imani na pote la ukafiri, ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Msimamizi wa Waumini na mwenye kuwanusuru, na kuwa makafiri hawana mwenye kuwasimamia wala kuwanusuru.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
إِنَّ ٱللَّهَ يُدۡخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يَتَمَتَّعُونَ وَيَأۡكُلُونَ كَمَا تَأۡكُلُ ٱلۡأَنۡعَٰمُ وَٱلنَّارُ مَثۡوٗى لَّهُمۡ
Hakika Mwenyezi Mungu Atawatia, wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, kwenye mabustani ya Pepo ambayo inapita mito chini ya miti yake ikiwa ni takrima kwao. Na mfano wa wale waliokanusha katika kula kwao na kujistarehesha kwao na ulimwengu, ni kama mfano wa mifugo miongoni mwa wanyama ambao hawana hamu isipokuwa kula nyasi, hawafikirii lingine. Na Moto wa Jahanamu ndio makao yao na maskani.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَكَأَيِّن مِّن قَرۡيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةٗ مِّن قَرۡيَتِكَ ٱلَّتِيٓ أَخۡرَجَتۡكَ أَهۡلَكۡنَٰهُمۡ فَلَا نَاصِرَ لَهُمۡ
Na wengi miongoni mwa watu wa mijini walikuwa wana nguvu zaidi kuliko watu wa mji wako, ewe Mtume, ambao ni Makkah, waliokutoa watu wake humo. Watu wa miji hiyo tuliwaangamiza kwa adhabu za aina mbalimbali. Hawakuwa na msaidizi wa kuwanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ كَمَن زُيِّنَ لَهُۥ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُم
Je yule aliyekuwa na ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ujuzi kuwa Yeye ni Mmoja, ni kama yule ambaye Shetani amempambia matendo yake maovu na akafuata yale ambayo nafsi yake ilimuita iyafuate ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kumuabudu asiyekuwa Yeye bila ya hoja wala ushahidi? Hawalingani.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
مَّثَلُ ٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِي وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۖ فِيهَآ أَنۡهَٰرٞ مِّن مَّآءٍ غَيۡرِ ءَاسِنٖ وَأَنۡهَٰرٞ مِّن لَّبَنٖ لَّمۡ يَتَغَيَّرۡ طَعۡمُهُۥ وَأَنۡهَٰرٞ مِّنۡ خَمۡرٖ لَّذَّةٖ لِّلشَّٰرِبِينَ وَأَنۡهَٰرٞ مِّنۡ عَسَلٖ مُّصَفّٗىۖ وَلَهُمۡ فِيهَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ وَمَغۡفِرَةٞ مِّن رَّبِّهِمۡۖ كَمَنۡ هُوَ خَٰلِدٞ فِي ٱلنَّارِ وَسُقُواْ مَآءً حَمِيمٗا فَقَطَّعَ أَمۡعَآءَهُمۡ
Sifa ya Pepo ambayo Mwenyezi Mungu Amewaahidi wachamungu: ndani yake kuna mito mikubwa ya maji yasiyobadilika, na mito ya maziwa yasyogeuka tamu yake, na mito ya shizi ambayo wanaionea ladha wenye kuinywa, na mito ya asali iliyosafishwa isiyo na taka. Na wachamungu hawa watapata ndani ya hiyo pepo matunda yote ya aina tafauti na mengineyo. Na kubwa kuliko hayo ni kule kusitiriwa na kusamehewa dhambi zao. Basi je, wale watakaokuwa ndani ya Pepo hiyo ni kama wale watakaokaa Motoni bila kutoka humo na wakanyweshwa maji yaliyo moto sana hadi ya mwisho yakawakata tumbo zao?
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُ إِلَيۡكَ حَتَّىٰٓ إِذَا خَرَجُواْ مِنۡ عِندِكَ قَالُواْ لِلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مَاذَا قَالَ ءَانِفًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡ
Miongoni mwa hawa wanafiki kuna wanaokusikiliza bila ya kuelewa, kwa madharau na kupuuza, mpaka wanapoondoka kutoka kwenye kikao chako, huwa wakisema wakiwaambia wale waliohudhuria kikao chako kati ya wale wenye ujuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa njia ya shere, «Amesema nini Muhammad hivi sasa?» Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amezipiga muhuri nyoyo zao, zikawa haziielewi haki wala hawaongokei kuifikia, na wakayafuata matamanio yao katika ukafiri na upotevu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَٱلَّذِينَ ٱهۡتَدَوۡاْ زَادَهُمۡ هُدٗى وَءَاتَىٰهُمۡ تَقۡوَىٰهُمۡ
Na wale walioongoka kuifuata haki, Mwenyezi Mungu Aliwaongezea uongofu , na kwa hivyo uongofu wao ukapata nguvu na Akawaafikia kwenye uchamungu na akaufanya sahali kwao.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَهَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأۡتِيَهُم بَغۡتَةٗۖ فَقَدۡ جَآءَ أَشۡرَاطُهَاۚ فَأَنَّىٰ لَهُمۡ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ ذِكۡرَىٰهُمۡ
Wakanushaji hawa hawangojei isipokuwa wakati wa Kiyama ambao wameahidiwa kuwa utawajia kwa ghafla. Kwani alama zake zishajitokeza na wao hawakunufaika nazo. Basi watapata wapi kukumbuka wakati wa Kiyama utakapowajia?
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَٱعۡلَمۡ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لِذَنۢبِكَ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مُتَقَلَّبَكُمۡ وَمَثۡوَىٰكُمۡ
Basi jua, ewe Nabii, kwamba hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na utake msamaha wa dhambi zako, na uwaombee msamaha Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Mwenyezi Mungu anazijua harakati zenu mnapoangaza mchana na mahali pa kutulia kwenu mnapolala usiku.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَوۡلَا نُزِّلَتۡ سُورَةٞۖ فَإِذَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ مُّحۡكَمَةٞ وَذُكِرَ فِيهَا ٱلۡقِتَالُ رَأَيۡتَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ نَظَرَ ٱلۡمَغۡشِيِّ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡمَوۡتِۖ فَأَوۡلَىٰ لَهُمۡ
Na wale wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanasema, «Basi si iteremshwe sura kutoka kwa Mwenyezi Mungu ituamrishe kupigana jihadi na wakanushaji.» Na inapoteremshwa sura iliyoimarika kwa maelezo na mambo ya lazima na ikatajwa jihadi ndani yake, utawaona wale ambao mna shaka ndani ya nyoyo zao juu ya Dini ya Mwenyezi Mungu na unafiki wanakuangalia, ewe Nabii, maangalizi ya mtu ambaye amefinikwa na kicho cha kufa.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
طَاعَةٞ وَقَوۡلٞ مَّعۡرُوفٞۚ فَإِذَا عَزَمَ ٱلۡأَمۡرُ فَلَوۡ صَدَقُواْ ٱللَّهَ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ
Basi lililo bora kwa hawa ambao ndani ya nyoyo zao mna maradhi wamtii Mwenyezi Mungu na wasema neno linaoafikiana na Sheria. Vita vinapopasa na ikaja amri ya Mwenyezi Mungu kuilazimisha, hawa wanafiki wanachukia hilo. Na lau wao wangalikuwa wakweli kwa Mwenyezi Mungu katika kuamini na kutenda mema, hilo lingalikuwa bora kwao kuliko kufanya maasia na kuenda kinyume.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَهَلۡ عَسَيۡتُمۡ إِن تَوَلَّيۡتُمۡ أَن تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَتُقَطِّعُوٓاْ أَرۡحَامَكُمۡ
Huenda nyinyi mkikipa mgongo Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Mwenendo wa Nabii wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, mkaja kumuasi Mwenyezi Mungu katika ardhi, mkamkanusha Yeye, mkamwaga damu na mkakata vizazi vyenu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فَأَصَمَّهُمۡ وَأَعۡمَىٰٓ أَبۡصَٰرَهُمۡ
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaepusha na rehema Yake Akawafanya wasiyasikie yanayowanufaisha wala wasiyaone na zisiwafunukie hoja za Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa ni nyingi.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلۡقُرۡءَانَ أَمۡ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقۡفَالُهَآ
Je, si wayazingatie mawaidha ya Qur’ani wanafiki hawa na wazifikirie hoja zake? Lakini nyoyo hizi zimefungwa, hakuna kitu cha hii Qur’ani kinachozifikia, hivyo basi haziyatii akilini mawaidha ya Mwenyezi Mungu na mazingatio yake.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱرۡتَدُّواْ عَلَىٰٓ أَدۡبَٰرِهِم مِّنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡهُدَى ٱلشَّيۡطَٰنُ سَوَّلَ لَهُمۡ وَأَمۡلَىٰ لَهُمۡ
Hakika ya wale waliyorudi nyuma wakaacha uongofu na Imani na wakageuka kwa visigino vyao wakimkanusha Mwenyezi Mungu baada ya haki kuwafunukia, (hao) Shetani amewapambia makosa yao na akawanyoshea matumaini ya kuishi duniani.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُواْ لِلَّذِينَ كَرِهُواْ مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ سَنُطِيعُكُمۡ فِي بَعۡضِ ٱلۡأَمۡرِۖ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِسۡرَارَهُمۡ
Kule kuwanyoshea wao mpaka wakolee kwenye ukafiri, ni kwa kuwa wao walisema kuwaambia Mayahudi waliokanusha Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, «Tutawatii katika baadhi ya mambo ambayo yako kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu na amri ya Mtume Wake.» Na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anayajua wanayoyaficha na wanayoydhihirisha. Basi Muislamu ajihadhari na kumtii asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyo kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, na amri ya Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَكَيۡفَ إِذَا تَوَفَّتۡهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَضۡرِبُونَ وُجُوهَهُمۡ وَأَدۡبَٰرَهُمۡ
Basi itakuwa vipi hali yao watakapozikamata Malaika roho zao na huku wanawapiga nyuso zao na migongo yao?
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱتَّبَعُواْ مَآ أَسۡخَطَ ٱللَّهَ وَكَرِهُواْ رِضۡوَٰنَهُۥ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Adhabu hiyo waliyostahili na wakaipata ni kwa kuwa wao waliyafuata mambo yanayomfanya Mwenyezi Mungu Awakasirikie ya kumtii Shetani na wakayachukia yale yanayomfanya Awe radhi nao ya matendo mema, na miongoni mwayo ni kupigana na wakanushaji, baada ya kulifanya hilo ni lazima juu yao, ndipo Mwenyezi Mungu Akazibatilisha thawabu za matendo yao, miongoni mwa sadaka, kuunga kizazi na yasiyokuwa hayo.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَمۡ حَسِبَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخۡرِجَ ٱللَّهُ أَضۡغَٰنَهُمۡ
Au kwani wanadhani hao wanafiki kuwa Mwenyezi Mungu Hatovitoa vile vilivyomo ndani ya nyoyo zao vya uhasidi na kuuchukia Uislamu na wafuasi wake? Ndio, Mwenyezi Mungu Atamtenganisha mkweli kutokana na mrongo.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَلَوۡ نَشَآءُ لَأَرَيۡنَٰكَهُمۡ فَلَعَرَفۡتَهُم بِسِيمَٰهُمۡۚ وَلَتَعۡرِفَنَّهُمۡ فِي لَحۡنِ ٱلۡقَوۡلِۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Na lau tungalitaka, ewe Nabii, tungalikuonesha hao watu wenyewe, ukawatambua kwa alama zilizo wazi kwao. Na kwa hakika utawajua kutokana na maneno yao yaliyodhihirika yenye kuonyesha malengo yao. Na kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, hakuna chochote kinachofichamana cha matendo ya wanaomtii wala matendo ya wanaomuasi, na Atamlipa kila mmoja kwa anachostahili.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَلَنَبۡلُوَنَّكُمۡ حَتَّىٰ نَعۡلَمَ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ مِنكُمۡ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَنَبۡلُوَاْ أَخۡبَارَكُمۡ
Na tutawatahini nyinyi, tena tutawatahini, enyi Waumini, kwa kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu na kupigana nao jihadi mpaka yajitokeze yale Aliyoyajua Mwenyezi Mungu tangu kale, ili tuwatenge watu wa jihadi kati yenu na uvumilivu wa kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu na tuyatahini maneno yenu na matendo yenu, na hapo adhihirike mkweli miongoni mwenu kutokana na mrongo.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَشَآقُّواْ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡهُدَىٰ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗا وَسَيُحۡبِطُ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Hakika ya wale waliokataa kuwa Menyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, wakawazuia watu na Dini Yake, wakaenda kinyume na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wakampiga vita baada ya wao kujiwa na hoja na alama za kuwa yeye ni Nabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hawataidhuru Dini ya Mwenyezi Mungu kitu chochote na Atayatangua malipo ya matendo yao waliyoyafanya duniani, kwa kuwa wao hawakutaka kwa matendo hayo radhi za Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَلَا تُبۡطِلُوٓاْ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Enyi wale mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakafuata Sheria Zake kivitendo! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume katika maamrisho yao na makatazo yao, na msiyatangue malipo ya matendo yenu kwa kukanusha na kufanya maasia.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ مَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٞ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡ
Hakika ya wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika na wakawazuia watu na Dini Yake, kisha wakafa wakiwa katika hali hiyo, Mwenyezi Mungu Hatawasamehe, na Atawapa adhabu ikiwa ndio mateso yao kwa ukanushaji wao, na Atawafedhehesha mbele ya halaiki ya watu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَلَا تَهِنُواْ وَتَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱلسَّلۡمِ وَأَنتُمُ ٱلۡأَعۡلَوۡنَ وَٱللَّهُ مَعَكُمۡ وَلَن يَتِرَكُمۡ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Basi msiwe wanyonge, enyi wenye kumuamini Mwenyezi Mugu na Mtume Wake, wa kujiepusha na kupambana na washirikina, mkaogopa kupigana nao na mkawaita kwenye suluhu na masikilizano na hali ya kuwa nyinyi ndio wenye ushindi na nguvu juu yao, na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Yuko pamoja na nyinyi kwa kuwanusuru na kuwapa nguvu. Hapa kuna bishara kubwa ya kupatiwa ushindi na kusaidiwa juu ya maadui. Na Mwenyezi Mungu Hatawapunguzia nyinyi malipo mema ya matendo yenu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
إِنَّمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا لَعِبٞ وَلَهۡوٞۚ وَإِن تُؤۡمِنُواْ وَتَتَّقُواْ يُؤۡتِكُمۡ أُجُورَكُمۡ وَلَا يَسۡـَٔلۡكُمۡ أَمۡوَٰلَكُمۡ
Hakika uhai wa duniani ni mchezo na udanganyifu. Na mtakapomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkamuogopa Mwenyezi Mungu kwa kutekeleza mambo Aliyoyafanya ni ya lazima na kujiepusha na mambo ya kumuasi, Atawapa malipo mema ya matendo yenu, na Hatawataka myatoe mali yenu yote katika Zaka, Anachowataka mfanye ni mtoe sehemo ya hayo mali.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
إِن يَسۡـَٔلۡكُمُوهَا فَيُحۡفِكُمۡ تَبۡخَلُواْ وَيُخۡرِجۡ أَضۡغَٰنَكُمۡ
Akiwa Atawataka myatoe mali yenu na Akawa Atawakariria na kuwasumbua, mtayafanyia uchoyo na mtakataa kuyatoa, na hapo Atakapowataka myatoe mali yenu Atayatoa nje machukivu yaliyo ndani ya nyoyo zenu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ تُدۡعَوۡنَ لِتُنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبۡخَلُۖ وَمَن يَبۡخَلۡ فَإِنَّمَا يَبۡخَلُ عَن نَّفۡسِهِۦۚ وَٱللَّهُ ٱلۡغَنِيُّ وَأَنتُمُ ٱلۡفُقَرَآءُۚ وَإِن تَتَوَلَّوۡاْ يَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓاْ أَمۡثَٰلَكُم
Haya nyini, enyi Waumini, mnaitwa kutoa kwenye kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuinusuru Dini Yake. Basi miongoni mwenu kuna anayefanya uchoyo kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kufanya uchoyo huwa anajifanyia uchoyo nafsi yake. Na Mwenyezi Munmgu, Aliyetukuka, Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia nyinyi, na nyinyi ndio mnaomhitajia Yeye. Na mkipa mgongo mkaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na kufuata amri Zake, Atawaangamiza na Atawaleta watu wengine, na kisha wasiwe ni kama nyinyi katika kuzipa mgongo amri za Mwenyzi Mungu, bali wao watamtii Yeye na kumtii Mtume Wake na watapigana jihadi katika njia Yake kwa mali yao na nafsi zao.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
 
የይዘት ትርጉም ምዕራፍ: ሱረቱ ሙሀመድ
የምዕራፎች ማውጫ የገፅ ቁጥር
 
የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - የ እስዋሂሊ ቋንቋ ትርጉም - በአብደላህ ሙሀመድ ናስር ከሚስ - የትርጉሞች ማዉጫ

የተከበረው ቁርአን ስዋሂሊኛ መልዕክተ ትርጉም - በዶ/ር ሙሐመድ ዓብደሏህ አቡ በክር እና ሸይኽ ናሲር ኸሚስ

መዝጋት