Check out the new design

Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs * - Lexique des traductions


Traduction des sens Sourate: Muhammad   Verset:

Muhammad

ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ أَضَلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Wale waliokataa kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Peke Yake Mungu wa kweli Asiye na mshirika, na wakawazuia watu na Dini Yake, Mwenyezi Mungu Atazifuta amali zao na kuzipomosha na Atawapa usumbufu kwa sababu ya amali zao hizo.
Les exégèses en arabe:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٖ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡ كَفَّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ
Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakafuata Sheria Zake na wakaamini Kitabu Alichomteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, nacho ndio ukweli usiokuwa na shaka kutoka kwa Mola wao, Mwenyezi Mungu Atawasamehe na Atawafinikia maovu waliyoyafanya na hatawatesa kwa maovu hayo na Atawatengezea mambo yao duniani na Akhera.
Les exégèses en arabe:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡبَٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡحَقَّ مِن رَّبِّهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمۡثَٰلَهُمۡ
Kupoteza huko na kuongoza, sababu yake ni kwamba wale waliokufuru wamemfuata Shetani wakamtii, na kwamba wale walioamini walimfuata Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo ya mwangaza na uongofu. Kama Alivyobainisha Mwenyezi Mungu vile Anavyoyafanya mapote mawili ya watu wa ukafiri na watu wa Imani kwa wanavyostahili, vilevile Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Anawapigia watu mifano yao, ili kila watu wanaofanana wa aina moja wakutamane na wale wanaonasibiana nao.
Les exégèses en arabe:
فَإِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَضَرۡبَ ٱلرِّقَابِ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَثۡخَنتُمُوهُمۡ فَشُدُّواْ ٱلۡوَثَاقَ فَإِمَّا مَنَّۢا بَعۡدُ وَإِمَّا فِدَآءً حَتَّىٰ تَضَعَ ٱلۡحَرۡبُ أَوۡزَارَهَاۚ ذَٰلِكَۖ وَلَوۡ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَٱنتَصَرَ مِنۡهُمۡ وَلَٰكِن لِّيَبۡلُوَاْ بَعۡضَكُم بِبَعۡضٖۗ وَٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Basi mkipambana, enyi Waumini, na wale waliokufuru katika viwanja vya vita, piganeni nao kidhati na mzipige shingo zao. Hata mtakapowadhoofisha kwa kuwaua kwa wingi na mkazivunja nguvu zao, wafungeni kisawasawa wale mnaowateka. Kisha basi ima muwasamehe kwa kuwafungua na kuwaacha bila kutoa fidia badala yake, au wajikomboe kwa kutoa fidia, au watiwe utumwani au wauawe. Na endeleeni kufanya hivyo mpaka vita vimalizike. Hiyo ndiyo hukumu iliyotajwa ya kuwatahini Waumini kwa makafiri na ushindi kuzunguka baina yao. Na lau Mwenyezi Mungu Angalitaka wangalipata ushindi Waumini bila ya vita, lakini Mwenyezi Mungu Amejaalia mateso yao yawe mikononi mwenu ndipo Akaweka sheria ya jihadi ili Awajaribu nyinyi kwa wao na Ainusuru kwa sababu yenu Dini Yake. Na wale Waumini waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, Hatayapomosha Mwenyezi Mungu malipo mema ya matendo yao.
Les exégèses en arabe:
سَيَهۡدِيهِمۡ وَيُصۡلِحُ بَالَهُمۡ
Atawaafikia siku za uhai wao duniani wawe watiifu Kwake na wafanye matendo ya kumridhi, Awatengeze hali zao, mambo yao na malipo mema yao duniani na Akhera,
Les exégèses en arabe:
وَيُدۡخِلُهُمُ ٱلۡجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمۡ
na Awatie Peponi ambayo Aliwajulisha na Akawasifia, na Akawaafikia kusimama kuyafanya yale Ailyowaamrisha, na miongoni mwayo ni kufa shahidi katika njia Yake, kisha atawajulisha wao mashukio yao huko Peponi watakapoingia humo.
Les exégèses en arabe:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَنصُرُواْ ٱللَّهَ يَنصُرۡكُمۡ وَيُثَبِّتۡ أَقۡدَامَكُمۡ
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, mkiinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kuhukumu kwa Kitabu Chake na kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, Mwenyezi Mungu Atawapa ushindi juu ya maadui zenu na Atazithibitisha nyayo zenu wakati wa kupigana.
Les exégèses en arabe:
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فَتَعۡسٗا لَّهُمۡ وَأَضَلَّ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Na wale waliokanusha, basi maangamivu ni yao, na Mwenyezi Mungu Atazifuta thawabu za matendo yao mema.
Les exégèses en arabe:
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَرِهُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأَحۡبَطَ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Hayo ni kwa sababu wao walikichukia Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilichoteremshwa kwa Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakakikanusha, na Mwenyezi Mungu akayatangua matendo yao kwa kuwa yalikuwa katika kumtii Shetani.
Les exégèses en arabe:
۞ أَفَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ دَمَّرَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۖ وَلِلۡكَٰفِرِينَ أَمۡثَٰلُهَا
Kwani hawakwenda makafiri hawa kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu wakayazingatia yale yaliyowapata ummah waliopita ya mateso? Mwenyezi Mungu Aliyavunjavunja majumba yao. Na makafiri hawa watakuwa na mwisho kama huo uliowafikia ummah hao.
Les exégèses en arabe:
ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ مَوۡلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَأَنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ لَا مَوۡلَىٰ لَهُمۡ
Hilo tulilowafanyia watu wa mapote mawili: pote la Imani na pote la ukafiri, ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Msimamizi wa Waumini na mwenye kuwanusuru, na kuwa makafiri hawana mwenye kuwasimamia wala kuwanusuru.
Les exégèses en arabe:
 
Traduction des sens Sourate: Muhammad
Lexique des sourates Numéro de la page
 
Traduction des sens du Noble Coran - La traduction swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs - Lexique des traductions

Traduit par le Dr. 'Abd Allah Muhammad Abû Bakr et Cheikh Nâsir Khamîs.

Fermeture