prev

Al-Qalam

next

1 : 68

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ

«Nūn» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwakatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al- Baqarah. Anaapa Allah Mtukufu kwa Kalamu ambayo kwayo Malaika na watu wanaandikia, na kwa kile wanachokiandika cha kheri, manufaa na aina za elimu. info
التفاسير: |

2 : 68

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ

Hukuwa wewe, (ewe Mtume), kwa sababu ya neema ya Allah Mtukufu kwako, ya unabii na utume, ni mchache wa akili wala mwenye uduni wa maoni. info
التفاسير: |

3 : 68

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ

Na wewe una malipo makubwa yasiyopunguzwa wala kukatwa kwa yale matatizo unayopambana nayo katika ufikishaji ujumbe. info
التفاسير: |

4 : 68

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ

Na hakika wewe, (ewe Mtume), uko juu kwa tabia nzuri, nazo ni zile tabia njema zilizomo kwenye Qur’ani. Kwani kuifuata Qur’ani ilikua ni sifa yake, kwani alikua akitekeleza amri zake na kukomeka na yale yanayokatazwa. info
التفاسير: |

5 : 68

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ

Kwa kipindi cha karibu kijacho, utaona ewe Mtume, na wataona makafiri. info
التفاسير: |

6 : 68

بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ

Wataona (makafiri) ugonjwa wa akili na wazimu viko kwa nani miongoni mwenu? info
التفاسير: |

7 : 68

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Hakika Mola wako, kutakasika ni Kwake, Ndiye Mjuzi zaidi wa kumjua mpotofu aliyeenda kinyume na Dini ya Allah Mtukufu na njia ya uongofu, na Yeye Ndiye Mjuzi zaidi wa kumjua mchamungu aliyeongoka kwenye njia ya haki. info
التفاسير: |

8 : 68

فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Basi jikite kwenye msimamo ulionao, (ewe Mtume), wa kuenda kinyume na wakanushaji, na wala usiwatii. info
التفاسير: |

9 : 68

وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ

Wanatamani uwe laini kwao na kuwakubalia baadhi ya misimamo waliyonayo, na wao wawe laini kwako. info
التفاسير: |

10 : 68

وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ

Usimkubalie, (ewe Mtume), kila mtu mweye kuapa mara kwa mara. info
التفاسير: |

11 : 68

هَمَّازٖ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٖ

Muongo sana, dhalili, msengenyaji watu, anayetembea baina yao kwa kuchochea ugomvi na kuchukua maneno ya baadhi yao kuwapelekea wengine kwa lengo la kuwachonganisha, bahili wa mali, mwenye uchoyo wa kuitumia katika njia ya haki. info
التفاسير: |

12 : 68

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Mwenye kuzuia sana ufanyaji wema, anayevuka mpaka wake katika kuwafanyia watu uadui na kutumia yaliyoharamishwa, mwingi wa madhambi. info
التفاسير: |

13 : 68

عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ

Mshupavu katika ukafiri wake, mchafu na muovu na anayenasibishwa na baba asiye wake. info
التفاسير: |

14 : 68

أَن كَانَ ذَا مَالٖ وَبَنِينَ

Na kwa kuwa yeye ni mwenye mali na watoto ndipo akakiuka mipaka na akaifanyia kiburi haki. info
التفاسير: |

15 : 68

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Ikawa akisomewa aya za Qur’ani na mtu yoyote huzikanusha na kusema kuwa hizo ni maneno ya urongo na itikadi za watu waliopita. Aya hizi, ingawa zimeteremka kwa baadhi ya washirikina, kama vile al-Walīd bin al-Mughīrah, zina onyo ndani yake kwa Muislamu kuwa asikubaliane na anayesifika kwa sifa hizi zenye kutukanika. info
التفاسير: |

16 : 68

سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ

Tutaweka alama ya kudumu juu ya pua yake, ili afedheheke mbele za watu. info
التفاسير: |
prev

Al-Qalam

next
:
0:00 0:00