prev

Al-hijr

next

1 : 15

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ وَقُرۡءَانٖ مُّبِينٖ

(Alif, Lâm, Râ) Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa. hizo ni aya tukufu miongoni mwa aya za Kitabu kitukufu kilichoteremshwa kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Nazo ni aya za Qur’ani zenye kufafanua kweli kwa matamko mazuri zaidi na yaliyo wazi zaidi na yenye kuonyesha zaidi makusudio. Kitabu na Qur’ani ni kitu kimoja; na hapa Allah Mtukufu Ameyakusanya pamoja majina mawili. info
التفاسير: |

2 : 15

رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ كَانُواْ مُسۡلِمِينَ

Makafiri watatamani, watakapowaona Waumini walioasi wakitoka Motoni, lau wao wangekuwa ni wenye kumpwekesha Allah Mtukufu wakawa ni wenye kutoka kama wao. info
التفاسير: |

3 : 15

ذَرۡهُمۡ يَأۡكُلُواْ وَيَتَمَتَّعُواْ وَيُلۡهِهِمُ ٱلۡأَمَلُۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Waache, ewe Mtume, hao makafiri wapate kula na wastarehe na ulimwengu wao na iwashughulishe tamaa ya huo ulimwengu wasimtii Allah Mtukufu, watakuja kujua mwisho wa mambo yao ambayo ni hasara ya duniani na Akhera. info
التفاسير: |

4 : 15

وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٞ مَّعۡلُومٞ

Na wakiomba kuteremshiwa adhabu, kwa kukukanusha, ewe Mtume, basi sisi hatuuangamizi mji, isipokuwa uwapo wakati wa kuangamizwa umeshapangwa; hatutawaangamiza mpaka waufikie mfano wa wale waliowatangulia. info
التفاسير: |

5 : 15

مَّا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ

Hakuna watu wowote watakaoupita muda wao uliowekwa wakauzidisha wala kuutangulia wakaupunguza. info
التفاسير: |

6 : 15

وَقَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِي نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ إِنَّكَ لَمَجۡنُونٞ

Na wenye kumkanusha Muhammad, rehema na amani zimshukie, walisema kwa njia ya shere, «Ewe uliyeteremshiwa Qur’ani, wewe umerukwa na akili». info
التفاسير: |

7 : 15

لَّوۡمَا تَأۡتِينَا بِٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Si utuletee Malaika iwapo wewe ni mkweli wapate kutoa ushahidi kwamba Allah Mtukufu Amekutumiliza. info
التفاسير: |

8 : 15

مَا نُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَمَا كَانُوٓاْ إِذٗا مُّنظَرِينَ

Na Allah Mtukufu Akawajibu: Sisi hatuwateremshi Malaika isipokuwa kwa adhabu ambayo haina kucheleweshwa kwa asiyeamini na hawakuwa ni wenye kuachwa wakati Malaika watakapoteremka. info
التفاسير: |

9 : 15

إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Nabii Muhammad, (rehema na amani zimshukie), na hakika sisi tunachukua ahadi kuitunza isiongezwe, isipunguzwe wala sehemu yoyote katika hiyo isipotee. info
التفاسير: |

10 : 15

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ فِي شِيَعِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na kwa hakika tulitumiliza kabla yako, ewe Mtume, Wajumbe kati ya makundi ya wa mwanzo. info
التفاسير: |

11 : 15

وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Hakuna Mjumbe yoyote aliwajia wao isipokuwa walikuwa wakimfanyia shere. Katika haya pana kumliwaza Mtume, (rehema na amani zimshukie). Na kama walivyokufanyia hawa, hivyo ndivyo walivyofanyiwa Mitume kabla yako. info
التفاسير: |

12 : 15

كَذَٰلِكَ نَسۡلُكُهُۥ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Kama tulivyoutia ukafiri kwenye nyoyo za ummah waliotangulia kwa sababu ya kuwafanyia shere Mitume na kuwakanusha, hivyo ndivyo tunavyofanya kwenye nyoyo za washirikina miongoni mwa watu wako waliofanya uhalifu wa kumkanusha Allah Mtukufu na kuwakanusha Mitume Wake. info
التفاسير: |

13 : 15

لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَقَدۡ خَلَتۡ سُنَّةُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Hawauamini Ukumbusho ulioteremshwa kwako. Na umeshapita mwendo wa wamwanzo wa kuwaangamiza wakanushaji. Na hawa ni kama wao, wataangamizwa wenye kuendelea na ukafiri na ukanushaji miongoni mwao. info
التفاسير: |

14 : 15

وَلَوۡ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَابٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّواْ فِيهِ يَعۡرُجُونَ

Na lau tungewafungulia makafiri wa Makkah mlango wa mbingu, wakaendelea kupanda kuingia ndani wapate kuyashuhudia yaliyomo mbinguni ya ajabu za ufalme wa Allah Mtukufu, hawangaliamini. info
التفاسير: |

15 : 15

لَقَالُوٓاْ إِنَّمَا سُكِّرَتۡ أَبۡصَٰرُنَا بَلۡ نَحۡنُ قَوۡمٞ مَّسۡحُورُونَ

Na wangalisema, «Macho yetu yamerogwa mpaka tumekuwa tunaona tusiyoyaona. Sisi tumerogwa tu na Muhammad kwenye akili zetu». info
التفاسير: |
prev

Al-hijr

next
:
0:00 0:00