next

Al-Qadr

prev

1 : 97

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ

Sisi Tumeiteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu, nao ni miongoni mwa masiku ya mwezi wa Ramdhani. info
التفاسير: |

2 : 97

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ

Na nilipi liliokujulisha, (ewe Mtume), ni upi usiku wa cheo na utukufu? info
التفاسير: |

3 : 97

لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٞ مِّنۡ أَلۡفِ شَهۡرٖ

Usiku wa cheo na utukufu ni bora fadhila zake kuliko fadhila za miezi elfu moja isiyokuwa usiku huo. info
التفاسير: |

4 : 97

تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ

Usiku huo hushuka Malaika na Jibrili, amani iwashukie, kwa ruhusa ya Mola wao na kila amri ya kila jambo Alilolikadiria liwe kwa mwaka mzima. info
التفاسير: |

5 : 97

سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ

Usiku huo wote ni amani, hakuna shari, mpaka kuchomoza alfajiri. info
التفاسير: |
next

Al-Qadr

prev
:
0:00 0:00