85 : 43

وَتَبَارَكَ ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Ni nyingi mno baraka za Allah Mtukufu na kheri Zake na ni mkubwa mno ufalme Wake, Ambaye ni Yake Peke Yake, mamlaka ya mbingu saba na ardhi saba na vitu vilivyoko baina yake, na Kwake Yeye Ndiko uliko ujuzi wa Wakati ambapo Kiyama kitasimama, na viumbe wafufuliwe kutoka makaburini mwao wapelekwe kwenye Kisimamo cha Hesabu, na Kwake Yeye mtarudishwa, enyi watu, baada ya kufa kwenu, na hapo alipwe kila mmoja kwa anayostahiki. info
التفاسير: |
prev

Az-Zukhruf

next
:
0:00 0:00