prev

Az-Zukhruf

next

1 : 43

حمٓ

“Hā, Mĩm” maelezo yametangulia mwanzoni mwa sura ya Al-Baqarah juu ya herufi zilizokatwa na kutengwa. info
التفاسير: |

2 : 43

وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Allah Mtukufu Aliyetukuka Ameapa kwa Qur’ani ambayo matamshi yake na maana yake iko wazi. info
التفاسير: |

3 : 43

إِنَّا جَعَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa lugha ya Kiarabu, huenda nyinyi mkaelewa na mkazingatia maana yake na hoja zake. info
التفاسير: |

4 : 43

وَإِنَّهُۥ فِيٓ أُمِّ ٱلۡكِتَٰبِ لَدَيۡنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ

Nayo, kwa hakika, katika Ubao Uliohifadhiwa kwetu sisi ina cheo na heshima za juu, iko thabiti, haina tafauti ndani yake wala kugongana. info
التفاسير: |

5 : 43

أَفَنَضۡرِبُ عَنكُمُ ٱلذِّكۡرَ صَفۡحًا أَن كُنتُمۡ قَوۡمٗا مُّسۡرِفِينَ

Je tuwape nyinyi mgongo na tuache kuwateremshia Qur’ani kwa ajili ya kupuuza kwenu, kutofuata na kupita mipaka kwenu katika kukataa kuiamini? info
التفاسير: |

6 : 43

وَكَمۡ أَرۡسَلۡنَا مِن نَّبِيّٖ فِي ٱلۡأَوَّلِينَ

Tumewatuma Manabii wengi katika karne za mwanzo zilizopita kabla ya watu wako, ewe Nabii. info
التفاسير: |

7 : 43

وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Hawajiwi na Nabii yoyote isipokuwa huwa wakimcheza shere kama vile watu wako walivyokucheza shere, basi tukawaangamiza wale waliowakanusha Mitume wetu, nao walikuwa ni wenye nguvu kali na ushujaa wa kivita kuliko watu wako, (ewe Mtume). info
التفاسير: |

8 : 43

فَأَهۡلَكۡنَآ أَشَدَّ مِنۡهُم بَطۡشٗا وَمَضَىٰ مَثَلُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na yashapita mateso ya wa mwanzo kwa kuangamizwa kwa sababu ya ukanushaji wao, ujeuri wao na kuwacheza shere Mitume wao. Katika haya pana maliwazo kwa Nabii, (rehema na amani zimshukie). info
التفاسير: |

9 : 43

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡعَلِيمُ

Na unapowauliza, (ewe Mtume), hawa washirikina miongoni mwa watu wako, «Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?» Wanasema, «Aliyeziumba ni Yule Aliye Mshindi katika mamlaka Yake, Aliye Mjuzi wa hizo na vitu vilivyomo ndani yake, hakuna chochote kinachofichika Kwake». info
التفاسير: |

10 : 43

ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مَهۡدٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ فِيهَا سُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Aliyewafanyia ardhi kuwa ni (kama) tandiko na mkeka, Akawasahilishia humo njia za maisha yenu na biashara zenu, ili mjiongoze kwa njia hizo kwenye maslahi yenu ya kidini na ya kidunia. info
التفاسير: |
prev

Az-Zukhruf

next
:
0:00 0:00