បកប្រែអត្ថន័យគម្ពីរគួរអាន - បកប្រែជាភាសាស្វាហ៊ីលី - អាប់ទុលឡោះ មូហាំម៉ាត់ និង ណាសៀរ ខមីស

លេខ​ទំព័រ:close

17 : 68

إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ

Sisi tumewatahini watu wa Makkah kwa njaa na ukame, kama tulivyowatahini wenye shamba walipoapa wakiwa pamoja, kwamba watakwenda kuvuna matunda ya shamba lao asubuhi mapema, ili wasiokuwa wao, kati ya masikini na mfano wao, wasipate kula katika mavuno hayo. info
التفاسير: |

18 : 68

وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ

Na hawakusema walipopanga hayo, «Allah Mtukufu Akitaka». info
التفاسير: |

19 : 68

فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٞ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ

Allah Mtukufu akaliteremshia shamba hilo moto ukaliteketeza kipindi cha usiku hali wakiwa wamelala. info
التفاسير: |

20 : 68

فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ

Likapambaukiwa likiwa lishachomeka na kuwa leusi kama usiku wa giza. info
التفاسير: |

21 : 68

فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ

Hapo wakaitana kipindi cha asubuhi. info
التفاسير: |

22 : 68

أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ

Haya tokeni mapema mwende kwenye shamba lenu iwapo bado mnataka kuvuna matunda! info
التفاسير: |

23 : 68

فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ

Wakatoka kwa haraka, huku wakinong’onezana. info
التفاسير: |

24 : 68

أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٞ

Leo msimpe nafasi masikini yoyote kuingia shamba lenu. info
التفاسير: |

25 : 68

وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٖ قَٰدِرِينَ

Wakaenda kipindi cha mwanzo wa mchana kuelekea kwenye shamba lao wakiwa na lengo baya la kuwanyima masikini matunda ya shamba, wakiwa wana uwezo kamili wa kulitekeleza hilo kulingana na madai yao. info
التفاسير: |

26 : 68

فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ

Walipolishuhudia shamba lao limechomeka walilikataa na wakasema, ‘Kwa hakika tumepotea njia ya kulifikia! info
التفاسير: |

27 : 68

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ

Na walipojua kuwa hilo ndilo shamba lao walisema, Bali sisi tumekoseshwa mazao yake kwa sababu ya nia yetu ya uchoyo na kuwanyima masikini. info
التفاسير: |

28 : 68

قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ

Akasema muadilifu zaidi miongoni mwao, «Kwani sikuwaambia myafunge maneno yenu na matakwa ya Allah Mtukufu kwa kusema ‘Allah Mtukufu Akitaka’?» info
التفاسير: |

29 : 68

قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Hapo wakasema, baada ya kurudi kwenye fahamu za uongofu, «Allah Mtukufu Mola wetu Ametakasika na udhalimu katika haya yaliyotupata, lakini ni sisi ndio tuliojidhulumu nafsi zetu kwa kuacha kuyafunga maneno yetu na matakwa ya Allah Mtukufu na kwa lengo letu baya». info
التفاسير: |

30 : 68

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ

Wakageukiana wao kwa wao wakilaumiana kwa kuacha kuyafunga maneno yao na matakwa ya Allah Mtukufu na kwa lengo lao baya. info
التفاسير: |

31 : 68

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ

Wakasema, «Ewe ole wetu! Sisi tulikuwa tumekiuka mpaka kwa kuwanyima masikini na kuenda kinyume na amri ya Allah Mtukufu». info
التفاسير: |

32 : 68

عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ

Tunatarajia kwa Mola wetu kuwa Atatupa kilicho bora zaidi kuliko shamba letu, kwa kuwa tumetubia na tumekubali makosa yetu. Sisi tuna matumaini mema kwa Mola wetu, tunatarajia msamaha na tunaomba kheri. Mfano wa mateso hayo tuliyowatesa nayo wenye shamba, ndivyo yanavyokuwa mateso yetu duniani kwa kila anayeenda kinyume na amri ya Allah Mtukufu, na akazifanyia uchoyo neema za Allah Mtukufu Alizompa, kwa kutotekeleza haki ya Allah Mtukufu katika neema hizo. info
التفاسير: |

33 : 68

كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Na kwa hakika adhabu ya Allah Mtukufu ni kubwa zaidi na ni kali zaidi kuliko adhabu ya duniani. Lau wangejua wangejiepusha na kila jambo lenye kusababisha kupata mateso hayo. info
التفاسير: |

34 : 68

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Hakika wale waliojikinga na mateso ya Allah Mtukufu kwa kufanya yale Aliyowaamrisha na kuacha yale Aliyoyakataza, watapata kwa Mola wao huko Akhera, mabustani ya Peponi ambayo ndani yake kuna starehe za daima. info
التفاسير: |

35 : 68

أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ

Hivi tuwalinganishe wale wanaomnyenyekea Allah Mtukufu kwa kumtii na wale waliokufuru? info
التفاسير: |

36 : 68

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Mna nini nyinyi? Vipi mnatoa uamuzi huu wa kidhalimu, mkalinganisha baina yao katika malipo? info
التفاسير: |

37 : 68

أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٞ فِيهِ تَدۡرُسُونَ

Au nyinyi mna kitabu kilichoteremshwa kutoka mbinguni, ambacho mnakuta ndani yake kuwa mtiifu ni kama muasi, mkawa mnayasoma hayo mnayoyasema? info
التفاسير: |

38 : 68

إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ

Mkawa ndani ya kitabu hicho mna kila mnachokitamani? kwa hakika hilo nyinyi hamnalo. info
التفاسير: |

39 : 68

أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ

Au nyinyi mna ahadi na mapatano ya lazima juu yetu mpaka siku ya kiama kuwa mtapata mnayoyataka na kuyatamani? info
التفاسير: |

40 : 68

سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ

Waulize washirikina, (ewe Mtume), «Ni yupi katika wao anayeichukulia hukumu hiyo dhamana na ahadi kwamba atayapata hayo?» info
التفاسير: |

41 : 68

أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Au wana waungu wanaowachukulia dhamana kwa wanayoyasema na kuwasaidia kuyafikia hayo wanayoyataka? Basi na wawalete iwapo wao ni wakweli katika madai yao. info
التفاسير: |

42 : 68

يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٖ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ

Siku ya Kiyama, mambo yatakuwa magumu na kitisho chake kitakuwa kikubwa, na hapo Allah Mtukufu atakuja ili kutoa uamuzi baina ya viumbe, atafunua muundi Wake usiofanana na kitu chochote. Amesema mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), «Atafunua Mola wetu muundi Wake, hapo amsujudie kila mwanamume aliyeamini na mwanamke aliyeamini, na atasalia yule aliyekuwa akisujudu duniani kwa kujionesha na kusikika, mgongo wake ukigeuka na ukiwa mfupa mmoja.» Imepokewa na Bukhari na Muslim. info
التفاسير: |
prev

Al-Qalam

next
:
0:00 0:00