Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye hai kutoka maiti, naye ni mtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa?
Hakika dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu kufufua, na kuwa ni Yeye pekee anaye stahiki kuabudiwa, na kufufua kwake watu kutoka makaburini, zimeenea na zimo za namna mbali mbali. Kwani ni Yeye peke yake ndiye anaye ipasua mbegu ukachipua mmea, na ni Yeye ndiye anaye ipasua kokwa ukatokeza mti. Na hivyo humfufua aliye hai kutokana na kisicho kuwa hai, kama mtu kutokana na udongo. Na akatoa kisicho kuwa hai kutokana na kilicho hai, kama maziwa kutokana na mnyama. Huyo Muweza Mtukufu ndiye Mungu wa Haki. Basi kisiwepo kitu cha kukugeuzeni mkaacha kumuabudu Yeye mkaviabudu vyenginevyo. Imeunganishwa Aya hii ya kupasua mbegu na kokwa, na Aya ya kupambazua asubuhi ambayo inaashiria kuwepo mwangaza, na kiza, na ya kwamba mwangaza umeshikamana kwa nguvu na kukua kwa mimea na miti. Hayo ni kwa kuwa mbegu na kokwa baada ya kuchipua zinahitajia chakula. Na chakula hichi kinatokana na mbolea maalumu kutokana na ardhi, na pia kutokana na mwangaza wa jua. Kwa hivyo mizizi yao inakwenda chini kutafuta chakula cha ardhi, na vigogo vyake na matawi inapata chakula kutokana na mwako wa jua ambalo ndilo linachomoza asubuhi.
Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na utulivu, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi.
Ni Yeye ndiye anaye toa mwangaza wa mchana kutokana na giza- giza la asubuhi, ili vilivyo hai viende kupata njia za maisha yao. Na akaufanya usiku uwe ni wa mapumziko ya mwili na roho, na akaufanya mwendo wa jua na mwezi wende kwa mpango mzuri kabisa ili watu wajue nyakati za ibada zao na maisha yao. Huo ndio mpango ulio fanywa kwa hikima, ndio tadbiri ya Mwenye uwezo Mwenye kuumiliki ulimwengu, Mwenye kukusanya kila kitu katika ujuzi wake.
Na Yeye ndiye aliye kuwekeeni nyota ili mwongoke kwazo katika kiza cha bara na bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao jua.
Yeye ndiye aliye kufanyieni nyota zikuongozeni kwa zilivyo pangwa mfike mwendako, nanyi mnakwenda kizani usiku, bara au baharini. Hakika Sisi tumezibainisha dalili za rehema yetu, na uwezo wetu, kwa ajili ya watu ambao wanao nufaika kwa ilimu.
Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu.
Yeye ndiye aliye kutoeni kwenye asli moja, nayo ni baba wa watu wote, Adam. Na Adam ametoka kwenye ardhi. Basi ardhi ndio kituo chenu muda wa uhai wenu, na ndipo pahala pa kupaaga baada ya kufa kwenu, na mkapotea chini yake. Na tumezibainisha dalili za uwezo wetu kwa watu wanao zingatia na kufahamu mambo yalivyo.
Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokana na baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake punje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na yakawiva. Hakika katika hayo pana Ishara kwa watu wanao amini.
Naye ndiye anaye teremsha kutoka mawinguni maji, ambayo kwayo akatoa kila namna ya mimea. Kuna mimea inayo toa majani laini kuwa ni mboga, na tunatoa pia mimea ya kuzaa punje nyingi zimepandana wenyewe kwa wenyewe. Na kutokana na makole ya mitende mna mashada yamebeba tende, wepesi kuzipata. Na pia tumetoa kutokana na maji mizabibu, na zaituni, na makomamanga. Katika hiyo yapo matunda yalio fanana kwa sura, na yasiyo fanana kwa utamu, na harufu, na namna ya faida yake. Hebu yaangalieni kwa kupima na kuzingatia matunda yake inapo zaa hiyo miti, na matunda yanapo wiva, vipi yanapo komaa baada ya kupitia hali mbali mbali! Hakika katika haya zipo ishara kwa wanao itafuta Haki na wanaamini na kunyenyekea. Aya hii inafahamisha maana kwa ilimu ya sayansi, nayo ni kuwa maji husaidia mimea kuchipua. Mbegu iliyo kaa tu haitaharaki husisimka kwa kupata maji ikaanza kumea, ikafanya kazi yake ya uhai. Mimea tena hukua na kutoa majani yenye rangi ya kijani, nayo ni madda inayo itwa "Chlorophyl". Hiyo Klorofil ni lazima kuwepo kwa ajili ya kujenga chakula kwa msaada wa mwangaza wa jua, na kuweza kuukuza mmea na kutoa matunda na mbegu nyengine.
Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali Yeye ndiye aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo mbandikiza nayo!.
Juu ya dalili hizi makafiri wamewafanya Malaika na mashetani ni washirika wa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye aliye waumba hao. Haiwafalii kujua hayo wakamuabudu asiye kuwa Yeye, naye ndiye aliye waumba Malaika na mashetani. Haitakikani wawaabudu hao nao wameumbwa kama wao!! Na hawa makafiri wakambunia Mwenyezi Mungu wana. Wakristo wakadai kuwa Masihi ni mwana wa Mungu, na baadhi ya washirikina wa Kiarabu wakadai kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Na huo ni ujinga, kutokuwa na ilimu! Mwenyezi Mungu Mtukufu ameepukana na hayo wanayo muambatisha naye Subhana!
Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.
Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi bila ya kuwa na kiigizo kilicho tangulia, vipi awe na mwana, kama wanavyo dai hawa, na hali Yeye hana mke, naye ndiye aliye umba vitu vyote? Miongoni mwa vitu hivyo ni hao wanao wafanya washirika wake. Naye ni Mjuzi wa kila kitu, na anawahisabia wasemayo na watendayo, na ni Mwenye kuwalipa kwa kauli yao na vitendo vyao.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".