Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu.
Huyo aliye sifika kwa sifa za ukamilifu ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye, Muumba wa kila kitu vilivyo kuweko, na vitavyo kuwa. Basi ni Yeye tu Mwenye kustahiki kuabudiwa. Basi muabuduni Yeye, na Yeye peke yake ndiye Mwenye kutawala kila kitu na kila jambo. Marejeo yote ni kwake tu.
Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu.
Ewe Nabii! Waambie watu: Zimekwisha kujieni kutoka kwa Muumba wenu na Mwenye kumiliki mambo yenu yote, hoja na maelezo wazi katika hii Qur'ani. Hizo zinakuangazieni Njia ya Haki. Basi mwenye kunafiika kwazo, manufaa ni yake mwenyewe. Na mwenye kujitenga nazo, basi amejidhuru mwenyewe! Wala mimi si mlinzi wenu, bali mimi ni Mjumbe ninakufikishieni niliyo tumwa kwenu.
Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanao jua.
Na mfano wa uchambuzi kama huu wa pekee katika kueleza dalili za maumbile, ndivyo tunavyo eleza Ishara zetu katika Qur'ani kwa njia namna kwa namna na kwa mbali mbali, ili kusimamisha hoja za kuwashinda hao wapingao. Kwa hivyo wao hawapati ila kuzua uwongo, wakakutuhumu kuwa haya umejifunza kwa watu, wala hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Nasi tunabainisha haya uliyo teremshiwa, nayo ni Haki isiyo athirika na kipendacho moyo, kwa ajili ya watu ambao wanayo ielewa Haki na wanainyenyekea.
Fuata uliyo funuliwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hapana mungu ila Yeye. Na jitenge na washirikina.
Ewe Nabii! Fuata wahyi ulio kujia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye kumiliki na kuendesha mambo yako. Hakika Yeye peke yake ndiye Mungu anaye stahiki kut'iiwa na kunyenyekewa. Basi shikamana na ut'iifu wake, wala usibali inadi za washirikina.
Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao.
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka wamuabudu Yeye peke yake angeli walazimisha kwa nguvu na kwa uweza wake. Lakini Yeye amewaachilia watumie khiari yao. Na Sisi hatukukufanya wewe kuwa ni muangalizi wao, ukiwahisabia vitendo vyao. Wala wewe hukulazimishwa kuwa usimamie kuwapangia na kuwatengenezea mambo yao.
Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.
Enyi Waumini! Msiyatukane masanamu ya washirikina wanayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, isije chuki yao kwa hayo ikawapelekea hasira ya kumtukana Mwenyezi Mungu kwa uadui na ujinga. Kama tulivyo wapambia hawa kupenda masanamu yao, kila umma una a'mali yake kwa mujibu wa makdara yao. Na marejeo ya wote ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake Siku ya Kiyama. Naye atawaeleza khabari ya vitendo vyao, na atawalipa kwavyo.
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara wataiamini. Sema: Ishara ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa zitapo kuja hawato amini.
Na washirikina waliapa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwajia Ishara ya kuiona katika Ishara walizo zitaka, basi yakini hiyo itakuwa ni sababu ya kuamini kwao. Sema ewe Nabii: Ishara hizi ziko kwa Mwenyezi Mungu. Yeye peke yake ndiye Mwenye madaraka juu yake hizo ishara. Mimi sina uweza wa hayo. Nyinyi Waumini, hamjui ninayo yajua Mimi. Hata zikiwajia Ishara hizi hawataamini.
Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyo kuwa hawakuamini mara ya kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga.
Na nyinyi pia hamjui kuwa Sisi tumezigeuza nyoyo zao zinapo kuja Ishara huzitafutia visababu na tafsiri, na tunayageuza macho yao kwa mambo ya dhana na mawazo tu. Kwa hivyo baada ya kuja Ishara hali yao inakuwa kama mwanzo. Nasi tunawawacha wakipotea katika dhulma yao na inadi yao.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".