Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់ម៉ាអារិច   អាយ៉ាត់:

Al-Ma'arij

سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٖ وَاقِعٖ
Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea! [1]
[1] Ameita, mwenye kuita, kuhimiza kama kufanya kejeli, iletwe upesi adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo hapana shaka itawashukia makafiri.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٞ
Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia . [2]
[2] Wala hapana chochote cha kuzuia adhabu hiyo,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ
Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. [3]
[3] Kwani hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu, ambako huko ndiko zinatoka nguvu zinazo simama, na hukumu inayo tekelezwa.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ
Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! [4]
[4] Malaika na Jibrili wanapanda kwenda kunako toka amri yake kwa siku ambayo urefu wake ni miaka khamsini elfu kwa mujibu wa hisabu ya miaka ya duniani.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَٱصۡبِرۡ صَبۡرٗا جَمِيلًا
Basi subiri kwa subira njema.Hakika wao wanaiona iko mbali! [5]
[5] Basi, ewe Muhammad! Subiri uwastahamilie hizo kejeli zao, na kuhimiza kwao adhabu, kwa subira isiyo kuwa na mbabaiko ndani yake wala mashtaka.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدٗا
Hakika wao wanaiona iko mbali! [6]
[6] Hakika hao makafiri wanaiona hiyo Siku ya Kiyama ni kitu cha muhali kutokea.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَنَرَىٰهُ قَرِيبٗا
Na Sisi tunaiona iko karibu. [7]
[7] Na Sisi tunaona kuwa ni jambo jepesi katika uweza wetu, wala halina uzito wowote.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ
Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. [8]
[8] Siku mbingu itakapo kuwa kama fedha iliyo yayuka,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ
Na milima itakuwa kama sufi. [9]
[9] Na milima itakapo kuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na ikapigwa,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمٗا
Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. [10]
[10] Wala jamaa hamuulizi jamaa yake: Nini hali yako? Kwa sababu kila mmoja kajishughulikia nafsi yake!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់ម៉ាអារិច
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ