Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់ម៉ាអារិច   អាយ៉ាត់:
يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ
Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, [11]
[11] Watakuwa wakijuulishana wao kwa wao mpaka wajuane baraabara, na ilhali hapana amuulizae mwenzie kitu. Kafiri atatamani lau ange pata kujikomboa nafsi yake na adhabu hiyo Siku ya Kiyama kwa kumtoa mwanawe awe ni fidia yake,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ
Na mkewe, na nduguye, [12]
[12] Au mkewe, au nduguye,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ
Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, [13]
[13] Au jamaa zake aliyo khusiana nao,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ يُنجِيهِ
Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. [14]
[14] Na wote waliomo duniani, apate kuokoka yeye tu!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
كَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ
La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, [15]
[15] Ewe mkosefu! Wacha hayo unayo yatamani ya kutaka kujikomboa kwa fidia! Hakika huo moto, unawaka kweli!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
نَزَّاعَةٗ لِّلشَّوَىٰ
Unao babua ngozi ya kichwa! [16]
[16] Utakubabua mikono yako, na miguu yako, na viungo vyako vyote,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ
Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. [17]
[17] Utanadi kwa jina la huyo aliye iacha Haki, na akaacha ut'iifu,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ
Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. [18]
[18] Na akakusanya mali akayaweka katika mabweta yake, wala hakutoa haki ya Mwenyezi Mungu iliomo katika hayo mali!
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
۞ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا
Hakika mtu ameumbwa na papara. [19]
[19] Hakika tabia ya binaadamu ni papara, mwingi wa kupapatika,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعٗا
Inapo mgusa shari hupapatika. [20]
[20] Na kutoridhika akifikiwa na lolote la karaha na uzito,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا
Na inapo mgusa kheri huizuilia. [21]
[21] Na ni mwingi wa kuzuia na kunyima akipata kheri na neema.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ
Isipo kuwa wanao swali, [22]
[22] Isipo kuwa wanao swali,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ
Ambao wanadumisha Sala zao, [23]
[23] Ambao wanadumisha Swala zao, hawakikosi hata kipindi kimoja.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ مَّعۡلُومٞ
Na ambao katika mali yao iko haki maalumu [24]
[24] Na wale ambao katika mali yao ipo haki iliyo ainiwa
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; [25]
[25] iliyo wekwa kwa ajili ya masikini mwenye kuomba kutaka msaada, na anaye jizuilia kuomba pia. (Katika wanao zuilika kuomba wanaingia si wenye kustahi na kuona vibaya tu, bali pia wasio weza kuomba kama watoto wachanga, wagonjwa, na wanyama pia.)
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, [26]
[26] Na wale wanao isadiki Siku ya Malipo, basi wanajitayarisha kwa ajili yake;
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ
Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. [27]
[27] Na wale wanao iogopa adhabu ya Mola wao Mlezi basi wanajikinga nayo wala hawajitii katika jambo la kuwaletea adhabu hiyo.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونٖ
Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. [28]
[28] Kwani hakika adhabu ya Mola wao Mlezi hapana hata mmoja anaye weza kuaminika nayo isimpate.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ
Na ambao wanahifadhi tupu zao. [29]
[29] Na ambao wanazihifadhi tupu zao hata hawaemewi na matamanio yao.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ
Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi [30]
[30] Lakini kwa wake zao na masuria wao hawazihifadhi; kwa sababu hapo hawalaumiwi kuifuata tabia ya maumbile.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ
Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. [31]
[31] Basi mwenye kutafuta starehe ya maingiliano kwa wasio kuwa wake na masuria, basi hao tena ni wenye kuikiuka halali na kuingia katika haramu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, [32]
[32] Na hao wenye kuzihifadhi amana za sharia na amana za waja wa Mwenyezi Mungu, na walio lazimika nayo kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu bila ya kukhuni wala kupunja,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ
Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, [33]
[33] Na ambao kwa shahada zao wamesimama sawa sawa kwa haki bila ya kuficha wanalo lijua,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ
Na ambao wanazihifadhi Sala zao. [34]
[34] Na wanao hifadhi Swala zao wakizisali sawasawa kwa ukamilifu -
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
أُوْلَٰٓئِكَ فِي جَنَّٰتٖ مُّكۡرَمُونَ
Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. [35]
[35] Watu wenye sifa kama hizo nzuri watakuwa ni wenye kuhishimiwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu huko Peponi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ
Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? [36]
[36] Kitu gani kinawapelekea hao walio kufuru kukujia mbio mbio ?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ
Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! [37]
[37] Kutoka kuliani na kushotoni kwa makundi?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٖ
Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? [38]
[38] Je, kwani kila mmoja wao ana tamaa ya kuingia kwenye Pepo yenye neema, baada ya kusikia kuwa Mwenyezi Mungu amemuahidi Mtume wake na Waumini kuwatia Peponi?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
كَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ
La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. [39]
[39] Basi nawaache hiyo tamaa yao ya kuingia Peponi. Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na maji ya kudharauliwa.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza [40]
[40] Naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote, na magharibi zote za siku, na sayari na hidaya, kwamba hakika bila ya shaka Sisi tuna uweza wa kuwaangamiza,
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់ម៉ាអារិច
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ