Check out the new design

വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് വിവർത്തന കേന്ദ്രം * - വിവർത്തനങ്ങളുടെ സൂചിക


പരിഭാഷ അദ്ധ്യായം: ഫാത്തിഹ   ആയത്ത്:

Al-Fatihah

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
[1] Bismillaahi inamaanisha, ninaanza "kwa jina la Mwenyezi Mungu." Nayo ipo mwanzoni mwa kila Sura ya Qur-ani isipokuwa Surat Tawba. (Tafsir Aayat Al-Ahkam cha Muhammad bin Ali Assaayis).
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.[1]
[1] Mola Mlezi ni yule anayewalea walimwengu wote. Nao walimwengu ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu. Na ulezi wake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa viumbe wake ni wa aina mbili: Wa kiujumla na wa mahususi. Ama wa kiujumla ni kuumba kwake viumbe, kuwapa riziki, na kuwaongoza katika yale yaliyo na masilahi yao. Nao ulezi wake mahususi ni kulea kwake vipenzi wake kwa imani, na kuwawezesha kuifikia, na kuwakamilishia imani hiyo. (Tafsir Assa'dii)
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.[1]
[1] Katika misingi waliyokubaliana juu yake watangulizi wema wa umma huu na maimamu wake ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ana majina na sifa nzuri. (Tafsir Assa'di)
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ
Mmiliki wa Siku ya Malipo.[1]
[1] Kuanzia aya ya kwanza hadi aya hii, ni kana kwamba Mwenyezi Mungu aliyetakasika anasema: "Enyi waja wangu, ikiwa mnanisifu na mnanitukuza kwa sababu ya ukamilifu wa dhati yangu na sifa zangu, basi nisifuni, kwani Mimi kwa hakika ni “Mwenyezi Mungu.” Na ikiwa ni kwa sababu ya wema wangu, na ulezi wangu, na neema zangu, basi Mimi kwa hakika ndiye “Mola Mlezi wa walimwengu.” Na ikiwa ni kwa sababu ya matarajio na matumaini yenu katika siku zijazo, basi mimi kwa hakika ndiye “Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.” Na ikiwa ni kwa sababu ya hofu, basi mimi kwa hakika ndiye "Mmiliki wa Siku ya Kiyama." (Tafsiri ya Al-Alusi)
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ
Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.[1]
[1] Mwenyezi Mungu alitaja kuomba msaada baada ya kutaja ibada ijapokuwa kuomba msaada kunaingia humo (katika ibada); kwa sababu mja katika ibada zake zote anahitaji kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani, Mwenyezi Mungu asipomsaidia, hatapata anachokitaka kama vile kutekeleza maamrisho na kuacha makatazo. (Tafsir Assa'dii)
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
Tuongoe njia iliyonyooka.[1]
[1] Aya hii inajumuisha kubainisha kuwa mja hana njia ya kupata furaha yake (mafanikio) isipokuwa kwa kudumu kwenye njia iliyonyooka. Na kwamba hana njia yoyote ya kumfanya anyooke isipokuwa kwa kuongolewa na Mola wake Mlezi kuifikia; kama vile hana njia yoyote ya kumuabudu isipokuwa kwa msaada wake. Kwa hivyo, hana njia ya kunyooka kwenye njia hiyo (ya uwongofu) isipokuwa kwa uwongofu wake (Mwenyezi Mungu). (Tafsiri ya Ibn al-Qayyim)
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ
Njia ya wale uliowaneemesha. Siyo ya wale waliokasirikiwa, wala waliopotea.[1]
[1] Kisha (Mwenyezi Mungu) akaeleza kuwa njia ya watu wa uwongofu huu ni tofauti na njia ya watu wa waliokasirikiwa na watu wa upotovu. Hivyo basi, viumbe wakagawanyika katika makundi matatu kuhusiana na uwongofu huu: Aliyeneemeshwa kwa kuupata kisha bahati yake katika neema hiyo ikaendelea kulingana na bahati yake katika maelezo yake na migawanyiko yake. Na (kundi la pili) mpotevu ambaye hakupewa uwongofu huu, na wala hakufanikiwa kuupata. Na (kundi la tatu) aliyekasirikiwa; ambaye aliujua (uwongofu) lakini hakuwezeshwa kutenda kama (uwongofu )unavyohitaji. (Tafsiri ya Ibn al-Qayyim)
അറബി ഖുർആൻ വിവരണങ്ങൾ:
 
പരിഭാഷ അദ്ധ്യായം: ഫാത്തിഹ
സൂറത്തുകളുടെ സൂചിക പേജ് നമ്പർ
 
വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് വിവർത്തന കേന്ദ്രം - വിവർത്തനങ്ങളുടെ സൂചിക

റബ്‌വ ഇസ്‌ലാമിക് ദഅ്'വാ ആൻഡ് ഗൈഡൻസ് സെൻററിൻ്റെയും കോൺടെന്റ് ഇൻ ലാംഗ്വേജസ് സർവീസ് അസോസിയേഷൻ്റെയും സഹകരണത്തോടെ മർകസ് റുവാദ് തർജമ വിഭാഗം വിവർത്തനം ചെയ്തതാണ്.

അടക്കുക