《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

页码:close

32 : 15

قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Allah Mtukufu Akasema kumwambia Iblisi, «Una nini wewe kutosujudu pamoja na Malaika?» info
التفاسير: |

33 : 15

قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلٖ مِّنۡ حَمَإٖ مَّسۡنُونٖ

Iblisi akasema akionyesha kiburi chake na uhasidi wake, «Hainasibiani na mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kutokana na udongo mkavu, uliokuwa mweusi na uliogeuka». info
التفاسير: |

34 : 15

قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٞ

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Akamwambia, Basi toka Peponi, wewe ushafukuzwa na umeepushwa na kila jema. info
التفاسير: |

35 : 15

وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Umeshukiwa na laana na umewekwa mbali na rehema yangu mpaka Siku ya kufufuliwa watu ili wahesabiwe na walipwe. info
التفاسير: |

36 : 15

قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Iblisi akasema, «Ewe Mola wangu! Nipatie muda mpaka siku ya wewe kuwafufua waja wako, nayo ni Siku ya Kiyama». info
التفاسير: |

37 : 15

قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

Allah Mtukufu Akamwambia, Wewe ni miongoni mwa wale niliowapa muda na kuchelewesha kuwaangamiza mpaka siku ambayo viumbe wote watakufa baada ya Mpulizo wa kwanza. info
التفاسير: |

38 : 15

إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ

Nayo ni siku na muda maalumu. Na alikubaliwa hilo kwa njia ya kulegezewa na kuachiliwa, na ni mtihani kwa binadamu na majini. info
التفاسير: |

39 : 15

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Akasema Iblisi, Mola wangu, kwa sababu ya vile ulivyonipoteza na kunipotosha nitawapambia vizazi vya Ãdam kukuasi katika ardhi na nitawapoteza wote wasiione njia ya uongofu. info
التفاسير: |

40 : 15

إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

Isipokuwa waja wako ambao umewaongoa wakakutakasia ibada peke yako pasi na viumbe wako wengine. info
التفاسير: |

41 : 15

قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ

Akasema Allah Mtukufu, Hii ni njia nyofu iliyolingana inayofikisha kwangu na kwenye Nyumba ya ukarimu wangu. info
التفاسير: |

42 : 15

إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ

Kwa kweli, wale waja wangu ambao wamenitakasia mimi sitakupatia uwezo juu ya nyoyo zao ili uwapoteze kwa uwezo huo na njia iliyonyoka. Lakini uwezo wako utakuwa ni juu ya yule aliyekufuata miongoni mwa wapotofu washirikina ambao wameukubali usimamizi wako na kukutii badala ya kunitii mimi. info
التفاسير: |

43 : 15

وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Hakika Moto mkali ndio agizo la Iblisi na wafuasi wake wote. info
التفاسير: |

44 : 15

لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبٖ لِّكُلِّ بَابٖ مِّنۡهُمۡ جُزۡءٞ مَّقۡسُومٌ

Una milango saba, kila mlango uko chini ya mwingine. Kila mlango utakuwa na fungu na sehemu ya wafuasi wa Iblisi kulingana na matendo yao. info
التفاسير: |

45 : 15

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٍ

Hakika wale waliomcha Allah Mtukufu, kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kujiepusha na aliyoyakataza, watakua kwenye mabustani ya Pepo na mito ipitayo. info
التفاسير: |

46 : 15

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ

Wataambiwa, «Ingieni Mabustani haya mkiwa watulivu mumesalimika na kila ovu mmesalimika na kila adhabu». info
التفاسير: |

47 : 15

وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٖ مُّتَقَٰبِلِينَ

Na tutawaondolea yaliyomo ndani ya nyoyo zao ya chuki na uadui, wataishi Peponi wakiwa ndugu wapendanao, watakaa kwenye vitanda vikubwa na nyuso zao zitaelekeana katika hali ya kuungana na kupendana. info
التفاسير: |

48 : 15

لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبٞ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ

Haitawapata humo tabu wala uchovu. Na wao ni wenye kusalia humo milele. info
التفاسير: |

49 : 15

۞ نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Wapashe habari, ewe Mtume, waja wangu kwamba mimi ni mwenye kuwasamehe Waumini wenye kutubia, ni mwenye huruma kwao. info
التفاسير: |

50 : 15

وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ

Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iumizayo yenye kutia uchungu kwa wasiotubia. info
التفاسير: |

51 : 15

وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ

Na wapashe habari, ewe Mtume, kuhusu wageni wa Ibrãhîm miongoni mwa Malaika ambao walimpa habari njema za kupata mtoto na za kuangamia kwa jamaa wa Lûṭ. info
التفاسير: |
prev

Al-hijr

next
:
0:00 0:00