《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 阿布杜拉·穆罕默德和纳赛尔·海米斯。

页码:close

52 : 15

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمٗا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ

Pindi walipoingia kwake na wakamuamkia kwa kusema, «Amani.» Hapo naye akawarudishia maamkizi ya amani. Kisha akawaletea chakula wakakataa kukila, na hapo akasema, «Sisi ni wenye hofu na nyinyi». info
التفاسير: |

53 : 15

قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٖ

Malaika wakamwambia, «Usiwe na hofu. Sisi tumekuja kukupa habari njema kwamba utapata mtoto atakayekuwa na ujuzi mwingi wa Dini, naye ni Is’hãq». info
التفاسير: |

54 : 15

قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ

Ibrãhîm akasema, huku yuwaona ajabu, «Mnanipa habari njema za kupata mtoto na mimi nishakuwa mtu mzima, na mke wangu pia, ni kwa njia gani mnanipa habari njema hizo za kushangaza?». info
التفاسير: |

55 : 15

قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ

Wakasema, «Tunakupa habari njema kwa kweli ambayo Allah Mtukufu Ametujulisha nayo. Basi usiwe miongoni mwa waliokata tamaa ya wewe kupata mtoto». info
التفاسير: |

56 : 15

قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ

Ibrăhīm akasema, «Hakika hawakati tamaa na rehema za Mola wao isipokuwa walio na makosa waliojitenga na njia ya haki». info
التفاسير: |

57 : 15

قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Na akasema, «Ni jambo gani kubwa mlilolijia, enyi mliotumwa, kutoka kwa Allah Mtukufu?» info
التفاسير: |

58 : 15

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٖ مُّجۡرِمِينَ

Wakasema, «Hakika Allah Mtukufu Ametutuma kuwaangamiza watu wa Lût walio washirikina wapotofu». info
التفاسير: |

59 : 15

إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Isipokuwa Lūṭ na watu wake waliomuamini, hao hatutawaangamiza na tutawaokoa wote. info
التفاسير: |

60 : 15

إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Ama yule mke wake aliye kafiri, tumepitisha kwa amri ya Allah Mtukufu kumwangamiza pamoja na watakaosalia kwenye adhabu. info
التفاسير: |

61 : 15

فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Basi walipofika kwa Lût Malaika waliotumwa. info
التفاسير: |

62 : 15

قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ مُّنكَرُونَ

Aliwaambia, «Kwa kweli, nyinyi ni watu msiojulikana na mimi». info
التفاسير: |

63 : 15

قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ

Wakasema, «Usiogope. Kwani hakika yetu sisi tumekujilia na adhabu ambayo jamaa zako walikuwa na shaka nayo na hawakuwa wakiikubali kuwa ni kweli». info
التفاسير: |

64 : 15

وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na tumekujia na haki kutoka kwa Allah Mtukufu, na kwa hakika sisi ni wasema kweli. info
التفاسير: |

65 : 15

فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعٖ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدٞ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ

Kwa hivyo, toka pamoja na watu wako waumini, baada ya kupita sehemu ya usiku. Na wewe nenda nyuma yao isije mmoja wao akasalia nyuma ikampata adhabu. Na jichungeni asije mmoja wenu akageuka na akatazama nyuma asije akaona adhabu na pia naye ikampata. Na kimbilieni kule ambako Amewaamrisha Allah Mtukufu, ili mpate kuwa mahali salama penye amani. info
التفاسير: |

66 : 15

وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعٞ مُّصۡبِحِينَ

Na tukampelekea wahyi Lût kwamba watu wako(waliokukanusha) wataangamizwa wote, hakuna atakayesalia, pindi kutakapoanza kupambazuka. info
التفاسير: |

67 : 15

وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na wakaja wakazi wa mji wa Lût mpaka kwa Lût pindi walipojua kwamba kwake kuna wageni, huku wana furaha na nderemo kwa wageni wake, ili wawachukue wafanye nao machafu. info
التفاسير: |

68 : 15

قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ

Lût akawaambia, «Hawa ni wageni wangu, na wako kwenye himaya yangu, basi msinifedheheshe». info
التفاسير: |

69 : 15

وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ

Na yaogopeni mateso ya Allah Mtukufu, wala msiwasumbue mkaniingiza kwenye unyonge na madharau kwa kuwaudhi wageni wangu. info
التفاسير: |

70 : 15

قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Watu wake wakasema, «Kwani sisi si tulikukataza kumkaribisha mgeni yoyote miongoni mwa walimwengu – na walikuwa wakiwakatia njia wasafiri - kwa kuwa sisi tunataka kufanya machafu na wao?» info
التفاسير: |
prev

Al-hijr

next
:
0:00 0:00