Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 图勒   段:

At-Tur

وَٱلطُّورِ
Ninaapa kwa mlima wa T'ur.
阿拉伯语经注:
وَكِتَٰبٖ مَّسۡطُورٖ
Na Kitabu kilichoandikwa.
阿拉伯语经注:
فِي رَقّٖ مَّنشُورٖ
Katika ngozi iliyokunjuliwa.
阿拉伯语经注:
وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ
Na kwa Nyumba iliyojengwa.
阿拉伯语经注:
وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ
Na kwa dari iliyonyanyuliwa.
阿拉伯语经注:
وَٱلۡبَحۡرِ ٱلۡمَسۡجُورِ
Na kwa bahari iliyojazwa.
阿拉伯语经注:
إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٞ
Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea.
阿拉伯语经注:
مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٖ
Hapana wa kuizuia.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوۡرٗا
Siku zitakapotikisika mbingu kwa mtikiso.
阿拉伯语经注:
وَتَسِيرُ ٱلۡجِبَالُ سَيۡرٗا
Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa.
阿拉伯语经注:
فَوَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Basi ole wao siku hiyo hao wanaokadhibisha.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي خَوۡضٖ يَلۡعَبُونَ
Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا
Siku watakaposukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu.
阿拉伯语经注:
هَٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
(Waambiwe): Huu ndio ule Moto mliokuwa mkiukadhibisha!
阿拉伯语经注:
أَفَسِحۡرٌ هَٰذَآ أَمۡ أَنتُمۡ لَا تُبۡصِرُونَ
Je, huu ni uchawi, au hamwoni tu?
阿拉伯语经注:
ٱصۡلَوۡهَا فَٱصۡبِرُوٓاْ أَوۡ لَا تَصۡبِرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡۖ إِنَّمَا تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyokuwa mkiyatenda.
阿拉伯语经注:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَنَعِيمٖ
Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na neema.
阿拉伯语经注:
فَٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ وَوَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ
Wakifurahi kwa yale aliyowapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
阿拉伯语经注:
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyokuwa mkiyatenda.
阿拉伯语经注:
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٖ مَّصۡفُوفَةٖۖ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ
Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyopangwa kwa safu. Na tutawaoza mahurulaini.
阿拉伯语经注:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱتَّبَعَتۡهُمۡ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلۡحَقۡنَا بِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَمَآ أَلَتۡنَٰهُم مِّنۡ عَمَلِهِم مِّن شَيۡءٖۚ كُلُّ ٱمۡرِيِٕۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٞ
Na wale walioamini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani, tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alichokichuma.
阿拉伯语经注:
وَأَمۡدَدۡنَٰهُم بِفَٰكِهَةٖ وَلَحۡمٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
Na tutawapa matunda, na nyama kama watakavyopenda.
阿拉伯语经注:
يَتَنَٰزَعُونَ فِيهَا كَأۡسٗا لَّا لَغۡوٞ فِيهَا وَلَا تَأۡثِيمٞ
Watapeana humo bilauri zisizo na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.
阿拉伯语经注:
۞ وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ غِلۡمَانٞ لَّهُمۡ كَأَنَّهُمۡ لُؤۡلُؤٞ مَّكۡنُونٞ
Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza.
阿拉伯语经注:
وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَسَآءَلُونَ
Wataelekeana wakiulizana.
阿拉伯语经注:
قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا قَبۡلُ فِيٓ أَهۡلِنَا مُشۡفِقِينَ
Waseme: Hakika tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa mno.
阿拉伯语经注:
فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ
Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda mbali adhabu ya upepo wa Moto.
阿拉伯语经注:
إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلُ نَدۡعُوهُۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡبَرُّ ٱلرَّحِيمُ
Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwingi wa kurehemu.
阿拉伯语经注:
فَذَكِّرۡ فَمَآ أَنتَ بِنِعۡمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٖ وَلَا مَجۡنُونٍ
Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu.
阿拉伯语经注:
أَمۡ يَقُولُونَ شَاعِرٞ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيۡبَ ٱلۡمَنُونِ
Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari.
阿拉伯语经注:
قُلۡ تَرَبَّصُواْ فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُتَرَبِّصِينَ
Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia.
阿拉伯语经注:
أَمۡ تَأۡمُرُهُمۡ أَحۡلَٰمُهُم بِهَٰذَآۚ أَمۡ هُمۡ قَوۡمٞ طَاغُونَ
Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?
阿拉伯语经注:
أَمۡ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥۚ بَل لَّا يُؤۡمِنُونَ
Au ndiyo wanasema: 'Ameitunga hii!' Bali basi tu hawaamini!
阿拉伯语经注:
فَلۡيَأۡتُواْ بِحَدِيثٖ مِّثۡلِهِۦٓ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ
Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.
阿拉伯语经注:
أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
阿拉伯语经注:
أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ
Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana yakini.
阿拉伯语经注:
أَمۡ عِندَهُمۡ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمۡ هُمُ ٱلۡمُصَۜيۡطِرُونَ
Au wanazo hazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
阿拉伯语经注:
أَمۡ لَهُمۡ سُلَّمٞ يَسۡتَمِعُونَ فِيهِۖ فَلۡيَأۡتِ مُسۡتَمِعُهُم بِسُلۡطَٰنٖ مُّبِينٍ
Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja iliyo wazi!
阿拉伯语经注:
أَمۡ لَهُ ٱلۡبَنَٰتُ وَلَكُمُ ٱلۡبَنُونَ
Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?
阿拉伯语经注:
أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ
Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?
阿拉伯语经注:
أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ
Au wanayo elimu ya ghaibu, nao wameandika?
阿拉伯语经注:
أَمۡ يُرِيدُونَ كَيۡدٗاۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ هُمُ ٱلۡمَكِيدُونَ
Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao waliokufuru ndio watakaotegeka.
阿拉伯语经注:
أَمۡ لَهُمۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Au wanaye mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ametaksika Mwenyezi Mungu mbali na hao wanaowashirikisha naye.
阿拉伯语经注:
وَإِن يَرَوۡاْ كِسۡفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطٗا يَقُولُواْ سَحَابٞ مَّرۡكُومٞ
Na hata wangeona pande linatoka mbinguni linaanguka wangesema: Ni mawingu yaliyobebana.
阿拉伯语经注:
فَذَرۡهُمۡ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي فِيهِ يُصۡعَقُونَ
Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapohilikishwa.
阿拉伯语经注:
يَوۡمَ لَا يُغۡنِي عَنۡهُمۡ كَيۡدُهُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ
Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
阿拉伯语经注:
وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ عَذَابٗا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Na hakika wale waliodhulumu watapata adhabu nyingine isiyokuwa hii, lakini wengi wao hawajui.
阿拉伯语经注:
وَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعۡيُنِنَاۖ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ
Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu,
阿拉伯语经注:
وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَإِدۡبَٰرَ ٱلنُّجُومِ
Na usiku pia mtakase, na zinapokuchwa nyota.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 图勒
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭