Check out the new design

《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 * - 译解目录


含义的翻译 章: 奈智姆   段:

An-Najm

وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ
Ninaapa kwa nyota inapotua.
阿拉伯语经注:
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
阿拉伯语经注:
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ
Wala hatamki kwa matamanio.
阿拉伯语经注:
إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ
Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa.
阿拉伯语经注:
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ
Amemfundisha aliye Mwingi wa nguvu.
阿拉伯语经注:
ذُو مِرَّةٖ فَٱسۡتَوَىٰ
Mwenye kutua, akatulia.
阿拉伯语经注:
وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.
阿拉伯语经注:
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ
Kisha akakaribia na akateremka.
阿拉伯语经注:
فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.
阿拉伯语经注:
فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alichomfunulia.
阿拉伯语经注:
مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ
Moyo haukusema uongo uliyoyaona.
阿拉伯语经注:
أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
Je, mnabishana naye kwa aliyoyaona?
阿拉伯语经注:
وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ
Na akamwona mara nyingine.
阿拉伯语经注:
عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Penye Mkunazi wa mwisho.
阿拉伯语经注:
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ
Karibu yake ndiyo ipo Bustani ya mbinguni inayokaliwa.
阿拉伯语经注:
إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ
Kilipoufunika huo Mkunazi hicho kilichoufunika.
阿拉伯语经注:
مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
阿拉伯语经注:
لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ
Je, mmemuona Lata na Uzza?
阿拉伯语经注:
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ
Na Manaat, mwingine wa tatu?
阿拉伯语经注:
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ
Je, nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?
阿拉伯语经注:
تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ
Huo ni mgawanyo wa dhuluma!
阿拉伯语经注:
إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.
阿拉伯语经注:
أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ
Ati mtu anakipata kila anachokitamani?
阿拉伯语经注:
فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
阿拉伯语经注:
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipokuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.
阿拉伯语经注:
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ
Hakika wale wasioamini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
阿拉伯语经注:
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا
Nao hawana elimu yoyote kwa hayo isipokuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.
阿拉伯语经注:
فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Basi mwachilie mbali anayeupa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.
阿拉伯语经注:
ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ
Huo ndio mwisho wao wa elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anayemjua zaidi mwenye kuongoka.
阿拉伯语经注:
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, ili awalipe wale waliotenda ubaya kwa waliyoyatenda, na wale waliotenda mema awalipe mema.
阿拉伯语经注:
ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ
Ambao wanajiweka mbali na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa hafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipokuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijione watakatifu. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga akawa mbali na maovu.
阿拉伯语经注:
أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ
Je, umemwona yule aliyegeuka akaenda zake?
阿拉伯语经注:
وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ
Na akapeana kidogo, kisha akajizuia?
阿拉伯语经注:
أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ
Je, anayo huyo elimu ya ghaibu, basi ndiyo anaona?
阿拉伯语经注:
أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?
阿拉伯语经注:
وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ
Na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi?
阿拉伯语经注:
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ
Ya kwamba hakika nafsi iliyobeba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?
阿拉伯语经注:
وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyoyafanya mwenyewe?
阿拉伯语经注:
وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?
阿拉伯语经注:
ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa hayo kwa ukamilifu.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Na kwamba kwa Mola wako Mlezi ndiyo mwisho.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye anayeleta kicheko na kilio.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا
Na kwamba Yeye ndiye anayefisha na kuhuisha.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye aliyeumba jozi, dume na jike
阿拉伯语经注:
مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ
Kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ
Na kwamba ni Yeye ndiye anayetosheleza na kukinaisha.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.
阿拉伯语经注:
وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye aliyewaangamiza 'Adi wa kwanza.
阿拉伯语经注:
وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ
Na Thamudi hakuwabakisha.
阿拉伯语经注:
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhalimu zaidi, na waovu zaidi.
阿拉伯语经注:
وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ
Na miji iliyopinduliwa, ni Yeye aliyeipindua.
阿拉伯语经注:
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ
Vikaifunika vilivyofunika.
阿拉伯语经注:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayoifanyia shaka?
阿拉伯语经注:
هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ
Hili ni onyo katika maonyo yale yale ya zamani.
阿拉伯语经注:
أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ
Kiyama kimekaribia!
阿拉伯语经注:
لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ
Hapana wa kukifichua isipokuwa Mwenyezi Mungu.
阿拉伯语经注:
أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ
Je, mnayastaajabia maneno haya?
阿拉伯语经注:
وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ
Na mnacheka, wala hamlii?
阿拉伯语经注:
وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ
Nanyi mmeghafilika?
阿拉伯语经注:
فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ۩
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.
阿拉伯语经注:
 
含义的翻译 章: 奈智姆
章节目录 页码
 
《古兰经》译解 - 斯瓦希里语翻译 - 拉瓦德翻译中心。 - 译解目录

由拉瓦德翻译中心团队与拉布瓦 الدعوة协会和伊斯兰内容服务协会合作翻译。

关闭