የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - ስዋሂሊኛ ትርጉም - በዓሊይ ሙሕሲን አል-በርዋሊይ * - የትርጉሞች ማዉጫ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

የይዘት ትርጉም ምዕራፍ: ሱረቱ ዐበሰ   አንቀጽ:

Surat Abasa

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ
Alikunja kipaji na akageuka!
Uso wake ulitaghayari kwa kuchukia na akageuka,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ
Kwa sababu alimjia kipofu!
Kwa sababu kamjia kipofu anamuuliza khabari ya Dini yake.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
Na wewe unajuaje, pengine huyo kipofu atatakasika kwa atayo yapata kwako,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
Au atawaidhika na mawaidha yamfae.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ
Ama ajionaye hana haja!
Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ
Wewe ndio unamshughulikia?
Wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
Na si juu yako kama hakutakasika.
Na wewe una lawama gani ikiwa yeye hakutakasika kwa Imani?
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ
Ama anaye kujia kwa juhudi .
Ama anaye kukimbilia kutafuta ilimu na uwongofu,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَهُوَ يَخۡشَىٰ
Naye anaogopa!
Naye anamkhofu Mwenyezi Mungu .
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ
Ndio wewe unampuuza?
Wewe unampuuza.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٞ
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
Hakika Aya hizi ni mawaidha.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Basi anaye penda akumbuke.
Mwenye kutaka atawaidhika kwa Qur'ani.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فِي صُحُفٖ مُّكَرَّمَةٖ
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
Nayo Qur'ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa kwa Mwenyezi Mungu,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
مَّرۡفُوعَةٖ مُّطَهَّرَةِۭ
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
Zina cheo cha juu, na pahala palipo tukuka, zimetakasika na kila upungufu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
بِأَيۡدِي سَفَرَةٖ
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
Katika mikono ya Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewafanya ndio mabalozi baina yake na Mitume wake;
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
كِرَامِۭ بَرَرَةٖ
Watukufu, wema.
Walio bora, wema.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
Ameangamia mwanaadamu! Nini kilicho mfanya akufuru na hali Mwenyezi Mungu amemfanyia hisani zote hizi?
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ
Kwa kitu gani amemuumba?
Hakumbuki yeye kaumbwa kutokana na nini?
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
Kutokana na maji ya kudharauliwa Yeye Mwenyezi Mungu alimwanzisha kumuumba akamjaalia apitie daraja mbali mbali za kukua.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ
Kisha akamsahilishia njia.
Kisha akamfanyia nyepesi njia ya kufikia Imani, na akamfunza njia hiyo.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ
Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
Kisha akamfisha na akamtukuza kwa kumtia kaburini.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ
Kisha apendapo atamfufua.
Na tena akipenda atamhuisha baada ya kufa kwake.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ
La! Hajamaliza aliyo muamuru.
Ni kweli mwanaadamu, juu ya kuwa umri wake mrefu duniani, hakutimiza aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika mambo ya Imani na ut'iifu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ
Hebu mtu na atazame chakula chake.
Hebu mtu na aangalie shani ya chakula chake - vipi tulivyo kipanga na kumsahilishia!
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبّٗا
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
Ni Sisi tumeiteremsha mvua kutoka mbinguni, ikateremka.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa ajili ya mimea.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا
Kisha tukaotesha humo nafaka,
Tukaotesha humo nafaka ambazo watu huzila na huweka akiba.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا
Na zabibu, na mimea ya majani,
Na mizabibu na mimea ya majani inayo liwa mibichi.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا
Na mizaituni, na mitende,
Na mizaituni mizuri, na mitende yenye kuzaa,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
Na mabustani yaliyo songamana matawi ya miti yake,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَفَٰكِهَةٗ وَأَبّٗا
Na matunda, na malisho ya wanyama;
Na matunda ya kustaladhi nayo, na malisha ya kula nyama hoa (mifugo).
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
مَّتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
Tumeotesha yote hayo kwa ajili ya faida yenu na wanyama wenu wa kufuga.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ
Basi utakapo kuja ukelele,
Basi utakapo kuja ukelele wa Kiyama utakao tia uziwi masikio,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ
Na mamaye na babaye,
Na mama yake, na baba yake,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ
Na mkewe na wanawe.
Na mkewe, na wanawe!
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٖ شَأۡنٞ يُغۡنِيهِ
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha
Kila mmojapo katika hawa atakuwa na jambo lake la kumshughulisha!
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ مُّسۡفِرَةٞ
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza,
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
ضَاحِكَةٞ مُّسۡتَبۡشِرَةٞ
Zitacheka, zitachangamka;
Zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٞ
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
Na nyuso nyengine siku hii zina vumbi zimesawijika.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ
Giza totoro litazifunika,
Zimegubikwa na kiza na weusi.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ
Hao ndio makafiri watenda maovu
Wenye nyuso hizi ni makafiri wapotovu, ambao walio kuwa hawabali maasi waliyo kuwa wakiyatenda.
የአረብኛ ቁርኣን ማብራሪያ:
 
የይዘት ትርጉም ምዕራፍ: ሱረቱ ዐበሰ
የምዕራፎች ማውጫ የገፅ ቁጥር
 
የቅዱስ ቁርዓን ይዘት ትርጉም - ስዋሂሊኛ ትርጉም - በዓሊይ ሙሕሲን አል-በርዋሊይ - የትርጉሞች ማዉጫ

የተከበረው ቁርአን ስዋሂሊኛ መልዕክተ ትርጉም - በዓሊይ ሙሕሲን አል-በርዋሊይ

መዝጋት