Check out the new design

قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - علی محسن البروانی * - ترجمے کی لسٹ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

معانی کا ترجمہ سورت: عبَسْ   آیت:

Abasa

عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ
Alikunja kipaji na akageuka! [1]
[1] Uso wake ulitaghayari kwa kuchukia na akageuka,
عربی تفاسیر:
أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ
Kwa sababu alimjia kipofu! [2]
[2] Kwa sababu kamjia kipofu anamuuliza khabari ya Dini yake.
عربی تفاسیر:
وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? [3]
[3] Na wewe unajuaje, pengine huyo kipofu atatakasika kwa atayo yapata kwako,
عربی تفاسیر:
أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? [4]
[4] Au atawaidhika na mawaidha yamfae.
عربی تفاسیر:
أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ
Ama ajionaye hana haja! [5]
[5] Ama yule anaye jiona ametosheka kwa mali yake na nguvu zake,
عربی تفاسیر:
فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ
Wewe ndio unamshughulikia? [6]
[6] Wewe ndio unamkabili na unamshughulikia kumfikishia wito wako.
عربی تفاسیر:
وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
Na si juu yako kama hakutakasika. [7]
[7] Na wewe una lawama gani ikiwa yeye hakutakasika kwa Imani?
عربی تفاسیر:
وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ
Ama anaye kujia kwa juhudi . [8]
[8] Ama anaye kukimbilia kutafuta ilimu na uwongofu,
عربی تفاسیر:
وَهُوَ يَخۡشَىٰ
Naye anaogopa! [9]
[9] Naye anamkhofu Mwenyezi Mungu .
عربی تفاسیر:
فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ
Ndio wewe unampuuza? [10]
[10] Wewe unampuuza.
عربی تفاسیر:
كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةٞ
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. [11]
[11] Hakika Aya hizi ni mawaidha.
عربی تفاسیر:
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Basi anaye penda akumbuke. [12]
[12] Mwenye kutaka atawaidhika kwa Qur'ani.
عربی تفاسیر:
فِي صُحُفٖ مُّكَرَّمَةٖ
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, [13]
[13] Nayo Qur'ani imo katika kurasa zilizo tukuzwa kwa Mwenyezi Mungu,
عربی تفاسیر:
مَّرۡفُوعَةٖ مُّطَهَّرَةِۭ
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. [14]
[14] Zina cheo cha juu, na pahala palipo tukuka, zimetakasika na kila upungufu.
عربی تفاسیر:
بِأَيۡدِي سَفَرَةٖ
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, [15]
[15] Katika mikono ya Malaika ambao Mwenyezi Mungu amewafanya ndio mabalozi baina yake na Mitume wake;
عربی تفاسیر:
كِرَامِۭ بَرَرَةٖ
Watukufu, wema. [16]
[16] Walio bora, wema.
عربی تفاسیر:
قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? [17]
[17] Ameangamia mwanaadamu! Nini kilicho mfanya akufuru na hali Mwenyezi Mungu amemfanyia hisani zote hizi?
عربی تفاسیر:
مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ
Kwa kitu gani amemuumba? [18]
[18] Hakumbuki yeye kaumbwa kutokana na nini?
عربی تفاسیر:
مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. [19]
[19] Kutokana na maji ya kudharauliwa Yeye Mwenyezi Mungu alimwanzisha kumuumba akamjaalia apitie daraja mbali mbali za kukua.
عربی تفاسیر:
ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ
Kisha akamsahilishia njia. [20]
[20] Kisha akamfanyia nyepesi njia ya kufikia Imani, na akamfunza njia hiyo.
عربی تفاسیر:
ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ
Kisha akamfisha, akamtia kaburini. [21]
[21] Kisha akamfisha na akamtukuza kwa kumtia kaburini.
عربی تفاسیر:
ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ
Kisha apendapo atamfufua. [22]
[22] Na tena akipenda atamhuisha baada ya kufa kwake.
عربی تفاسیر:
كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ
La! Hajamaliza aliyo muamuru. [23]
[23] Ni kweli mwanaadamu, juu ya kuwa umri wake mrefu duniani, hakutimiza aliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu katika mambo ya Imani na ut'iifu.
عربی تفاسیر:
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ
Hebu mtu na atazame chakula chake. [24]
[24] Hebu mtu na aangalie shani ya chakula chake - vipi tulivyo kipanga na kumsahilishia!
عربی تفاسیر:
أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبّٗا
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, [25]
[25] Ni Sisi tumeiteremsha mvua kutoka mbinguni, ikateremka.
عربی تفاسیر:
ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقّٗا
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, [26]
[26] Tena tukaipasua pasua ardhi kwa ajili ya mimea.
عربی تفاسیر:
فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبّٗا
Kisha tukaotesha humo nafaka, [27]
[27] Tukaotesha humo nafaka ambazo watu huzila na huweka akiba.
عربی تفاسیر:
وَعِنَبٗا وَقَضۡبٗا
Na zabibu, na mimea ya majani, [28]
[28] Na mizabibu na mimea ya majani inayo liwa mibichi.
عربی تفاسیر:
وَزَيۡتُونٗا وَنَخۡلٗا
Na mizaituni, na mitende, [29]
[29] Na mizaituni mizuri, na mitende yenye kuzaa,
عربی تفاسیر:
وَحَدَآئِقَ غُلۡبٗا
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, [30]
[30] Na mabustani yaliyo songamana matawi ya miti yake,
عربی تفاسیر:
وَفَٰكِهَةٗ وَأَبّٗا
Na matunda, na malisho ya wanyama; [31]
[31] Na matunda ya kustaladhi nayo, na malisha ya kula nyama hoa (mifugo).
عربی تفاسیر:
مَّتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. [32]
[32] Tumeotesha yote hayo kwa ajili ya faida yenu na wanyama wenu wa kufuga.
عربی تفاسیر:
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ
Basi utakapo kuja ukelele, [33]
[33] Basi utakapo kuja ukelele wa Kiyama utakao tia uziwi masikio,
عربی تفاسیر:
يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, [34]
[34] Siku mtu atakapo mkimbia ndugu yake,
عربی تفاسیر:
وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ
Na mamaye na babaye, [35]
[35] Na mama yake, na baba yake,
عربی تفاسیر:
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ
Na mkewe na wanawe. [36]
[36] Na mkewe, na wanawe!
عربی تفاسیر:
لِكُلِّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذٖ شَأۡنٞ يُغۡنِيهِ
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha [37]
[37] Kila mmojapo katika hawa atakuwa na jambo lake la kumshughulisha!
عربی تفاسیر:
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ مُّسۡفِرَةٞ
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, [38]
[38] Zipo nyuso siku hii zenye mwangaza,
عربی تفاسیر:
ضَاحِكَةٞ مُّسۡتَبۡشِرَةٞ
Zitacheka, zitachangamka; [39]
[39] Zenye kung'ara na kufurahi kwa neema za Mwenyezi Mungu.
عربی تفاسیر:
وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةٞ
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, [40]
[40] Na nyuso nyengine siku hii zina vumbi zimesawijika.
عربی تفاسیر:
تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ
Giza totoro litazifunika, [41]
[41] Zimegubikwa na kiza na weusi.
عربی تفاسیر:
أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ
Hao ndio makafiri watenda maovu [42]
[42] Wenye nyuso hizi ni makafiri wapotovu, ambao walio kuwa hawabali maasi waliyo kuwa wakiyatenda.
عربی تفاسیر:
 
معانی کا ترجمہ سورت: عبَسْ
سورتوں کی لسٹ صفحہ نمبر
 
قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - علی محسن البروانی - ترجمے کی لسٹ

علی محسن البروانی نے ترجمہ کیا ہے۔

بند کریں