ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: البلد   آية:

سورة البلد - Surat Al-Balad

لَآ أُقۡسِمُ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Naapa kwa Mji huu!
Naapa kiapo cha mkazo kwa mji wa Makka, mji mtakatifu;
التفاسير العربية:
وَأَنتَ حِلُّۢ بِهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ
Nawe unaukaa Mji huu.
Na wewe unaishi katika mji huu, unauzidisha utukufu wake na cheo chake.
التفاسير العربية:
وَوَالِدٖ وَمَا وَلَدَ
Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa.
Na naapa kwa mzazi na anacho kizaa, na kwa hao wawili ndio jinsi inahifadhika na maendeleo yanabakia.
التفاسير العربية:
لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِي كَبَدٍ
Hakika tumemuumba mtu katika taabu.
Hakika Sisi tumemuumba mtu katika mashaka na taabu tangu mwanzo wake mpaka kumalizika mambo yake.
التفاسير العربية:
أَيَحۡسَبُ أَن لَّن يَقۡدِرَ عَلَيۡهِ أَحَدٞ
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
Je! Anadhani mtu aliye umbwa katika mashaka haya kuwa hapana awezae kumdhalilisha?
التفاسير العربية:
يَقُولُ أَهۡلَكۡتُ مَالٗا لُّبَدًا
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
Anasema: Nimetumia katika kupambana na Muhammad s.a.w. na kuupinga wito wake mali mengi ukiyakusanya pamoja.
التفاسير العربية:
أَيَحۡسَبُ أَن لَّمۡ يَرَهُۥٓ أَحَدٌ
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
Ati anadhani kwamba mambo yake hayo yamefichikana, hayajui yeyote hata huyo aliye muumba?
التفاسير العربية:
أَلَمۡ نَجۡعَل لَّهُۥ عَيۡنَيۡنِ
Kwani hatukumpa macho mawili?
Kwani Sisi hatukumuumba na macho mawili ya kutazamia,?
التفاسير العربية:
وَلِسَانٗا وَشَفَتَيۡنِ
Na ulimi, na midomo miwili?
Na ulimi na midomo miwili ili aweze kutamka na kusema sawa?
التفاسير العربية:
وَهَدَيۡنَٰهُ ٱلنَّجۡدَيۡنِ
Na tukambainishia zote njia mbili?
Na tukamwonyesha njia ya kheri na ya shari, na tukamtengenezea aweze kuchagua mojawapo?
التفاسير العربية:
فَلَا ٱقۡتَحَمَ ٱلۡعَقَبَةَ
Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
Basi huyo hakunafiika kwa tuliyo mtengenezea, wala hakuivuka njia ya milimani inayo mzuia asifikie uwokovu, nayo ni choyo wa nafsi yake.
التفاسير العربية:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡعَقَبَةُ
Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?
Na kitu gani kitakufunza nini huko kujitoma kwenye njia ya milimani?
التفاسير العربية:
فَكُّ رَقَبَةٍ
Kumkomboa mtumwa;
Kumkomboa mtu kutokana na utumwa,
التفاسير العربية:
أَوۡ إِطۡعَٰمٞ فِي يَوۡمٖ ذِي مَسۡغَبَةٖ
Au kumlisha siku ya njaa
Au kumlisha siku ya njaa
التفاسير العربية:
يَتِيمٗا ذَا مَقۡرَبَةٍ
Yatima aliye jamaa,
Yatima aliye jamaa wa kumliwaza kwa ujamaa na ufakiri.
التفاسير العربية:
أَوۡ مِسۡكِينٗا ذَا مَتۡرَبَةٖ
Au masikini aliye vumbini.
Au masikini mwingi wa haja na kufakirika.
التفاسير العربية:
ثُمَّ كَانَ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلصَّبۡرِ وَتَوَاصَوۡاْ بِٱلۡمَرۡحَمَةِ
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
Tena awe pamoja na hayo miongoni mwa wenye Imani wanao usiana na wenzao kwa subira na kuoneana huruma.
التفاسير العربية:
أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.
Hao wanao sifika kwa sifa hizi, ndio watu wa kheri, wa mkono wa kulia.
التفاسير العربية:
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni.
Na walio zikataa dalili tulizo zisimamisha kuthibitisha Haki kutoka na Kitabu na hoja zake, hao ndio wapotovu watu waovu walio kosa kheri na watapata adhabu.
التفاسير العربية:
عَلَيۡهِمۡ نَارٞ مُّؤۡصَدَةُۢ
Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.
Juu yao utakuwa Moto ulio bebeana na milango yake ikafungwa.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: البلد
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق