Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Ash-Sharh   Ayah:

Surat Ash-Sharh

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ
Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri,
Arabic explanations of the Qur’an:
وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ
Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ
na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha,
Arabic explanations of the Qur’an:
وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ
kwenye cheo cha juu?
Arabic explanations of the Qur’an:
فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا
Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرٗا
Hakika kwenye dhiki kuna faraji.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ
Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب
Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako.
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Ash-Sharh
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close