prev

Al-Kafirun

next

1 : 109

قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ

Sema, (ewe Mtume), kuwaambia waliomkufuru Allah Mtukufu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Allah Mtukufu!» info
التفاسير: |

2 : 109

لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ

Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo. info
التفاسير: |

3 : 109

وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ

Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa. info
التفاسير: |

4 : 109

وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ

Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo. info
التفاسير: |

5 : 109

وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ

Wala nyinyi si wenye kumuabudu ninayemuabudu mimi siku zijazo, Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Allah Mtukufu Alijua kuwa hawataamini kabisa. info
التفاسير: |

6 : 109

لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ

Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ninayo iamini na sitaki nyingine. info
التفاسير: |
prev

Al-Kafirun

next
:
0:00 0:00