Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea kuona. Akasema: Je! Sikukwambieni kuwa mimi najua ya Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi? [96]
[96] Akashikilia tamaa yake akingojea rehema ya Mwenyezi Mungu, na ahali zake wakashikilia kumdhania dhana mbovu mpaka alipo fika mtu aliye chukua kanzu na kumbashiria kwamba Yusuf yupo salama salmina. Ilipo wekwa kanzu usoni kwa Yaa'qub akainusa harufu yake, moyo wake ulijaa furaha, macho yake yakarejea kuona. Yule mjumbe alipo msimulia hali ya Yusuf, na kwamba anamtaka yeye asafiri ende pamoja na ahali zake, aliwageukia walio kuwa naye akiwakumbusha ule utabiri wake, na akiwakaripia kwa vile walivyo mkadhibisha. Akawataka wakumbuke yale aliyo wahakikishia pale punde kwamba yeye anaijua rehema ya Mwenyezi Mungu na fadhila yake wasio ijua wao.
Wakasema: ewe baba yetu, tusamehe Dhambi zetu hapana shaka sisi, tulikuwa na Makosa. [97]
[97] Hapo wakamkabili kwa kumtaka msamaha, wakimtaraji awasamehe, na awatakie kwa Mwenyezi Mungu maghfira kwa madhambi yao. Kwani wao walimhakikishia katika kule kutubu kwao kwamba wao walikuwa ni wenye kutenda madhambi.
Akasema: Nitakuja kuombeeni msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kusamehe. [98]
[98] Akasema Yaa'qub nitaendelea kutaka msamaha kwa Mwenyezi Mungu kufutiwa dhambi zenu. Na hakika Yeye peke yake ndiye mwenye maghfira ya milele na rehema ya daima.
Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah, mmo katika amani. [99]
[99] Yaa'qub akasafiri kwenda Misri pamoja na ahali zake mpaka akafika huko. Walipo ingia kwa Yusuf, naye alikuwa kawapokea kwenye milango ya Misr, huruma na shauku ilimpeleka kwa haraka kwa baba na mama yake! Akawakaribisha na akawataka wao na ahali zake wakae Misri kwa amani na salama kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Na Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia wema kunitoa gerezani, na kukuleteni kutoka jangwani baada ya Shet'ani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Bila ya shaka Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima. [100]
[100] Msafara ukenda ndani ya nchi ya Misri mpaka ukafika kwenye nyumba ya Yusuf. Wakaingia, na Yusuf akawatanguliza wazazi wake akawaweka kwenye kochi. Yaa'qub na ahali zake wakajaa furaha kwa uzuri wa mapokezi aliyo watengezea Mwenyezi Mungu katika mikono ya Yusuf. Kwani kwa hayo ukoo wote umekusanyika hapo baada ya mfarakano, na umetukuka makamu makubwa ya utukufu na hishima. Wakamuamkia maamkio yaliyo zowewa na watu tangu zamani ya kuwaamkia maraisi na watawala. Wakaonyesha unyenyekevu kwa utawala wake. Yale yalimkumbusha Yusuf ile ndoto yake ya utotoni. Akamwambia baba yake: Hii ndio tafsiri ya ndoto niliyo iota na nikakusimulia ya kwamba nimeota usingizini kuwa nyota kumi na moja na jua na mwezi zinanisujudia; ni hivi basi Mola wangu Mlezi ameitimiza, na amenitukuza na amenifanyia hisani. Amedhihirisha kuwa sina makosa, na akanitoa kifungoni, na akakuleteni kutoka jangwani tukutane, baada ya Shetani kutufisidi baina yangu na ndugu zangu, akawachochea dhidi yangu. Na haya yote yasinge kuwa bila ya Mwenyezi Mungu kuyafanya. Yeye ndiye wa kupanga na kuyafanya mambo yatimie kama atakavyo. Na Yeye ndiye Mwenye kuzunguka kila kitu kwa ujuzi wake, ambaye hukumu yake ni yenye kushinda katika kila jambo na kadhiya.
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza tafsiri ya mambo. Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema. [101]
[101] Yusuf akamwelekea Mwenyezi Mungu akimshukuru kwa kuzihisabu neema zake juu yake, na akimwomba amzidishie fadhila zake, kwa kusema: Ewe Mola wangu Mlezi! Neema zako kwangu ni nyingi mno, na bora mno! Umenipa utawala, na nakuhimidi kwa hayo. Ukanitunukia ilimu ya kufasiri ndoto kama ulivyo nitunukia! Ewe Muumba mbingu na ardhi! Wewe ndiye uliye miliki mambo yangu yote, na Mtawala wa neema za uhai wangu na baada ya kufa kwangu! Nifungamanishe nawe kwa ulivyo waridhia Manabii wako katika Dini ya Kiislamu, na uniingize katika kundi la ulio waongoa kwenye wema miongoni mwa baba zangu, na waja wako walio wema, walio safika.
Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipo azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua vitimbi. [102]
[102] Ewe Nabii! Haya tuliyo kusimulia ni katika khabari zilizo pita za kale. Hazikukufikia ila kwa wahyi ulio toka kwetu. Wala wewe hukuwapo pale nduguze Yusuf walipo kuwa wakipanga njama. Wala wewe hukuwa unavijua vitimbi vyao ila kwa kusimuliwa nasi.
Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi. [103]
[103] Na wapo wengi ambao tabia zao zina maradhi zinazo wazuia wasisadiki haya unayo funuliwa, hata moyo wako ukiwa una shauku namna gani waamini, au nafsi yako ikafanya juhudi gani waongoke.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".