Na yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawatengenekewi. [23]
[23] Na yule bibi aliye kuwa Yusuf anakaa nyumbani kwake, naye anamjua madaraka yake, alitaka kumghuri aache mwendo wake ulio safi. Akawa anajipitisha pitisha mbele yake kuonyesha uzuri wake, na kujitamanisha kwake. Hata mwishoe akamfungia milango, na akamwambia: Njoo kwangu, nimejitoa kwako! Yusuf akasema: Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu, aniepusha na hiyo shari! Na vipi nifanye uchafu huo nawe, na mumeo mheshimiwa ni bwana wangu aliye niweka bora ya makamo? Hakika hawafuzu wanao wadhulumu watu kwa udanganyifu na khiana, wakajitia wenyewe katika maasi ya uzinzi!
Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio safishwa. [24]
[24] Na yule bibi aliazimia aingiane naye, na nafsi ya Yusuf ilimvutia kwake, lau kuwa hakuiona nuru ya Mwenyezi Mungu ya haki imezagaa mbele ya macho yake. Basi hakuufuata mvutio wa nafsi, na akayashinda matamanio, na akajizuilia maasi na khiana. Akathibiti juu ya usafi na kutakasika kwake. Ndio hivi tulivyo mthibitisha Yusuf kwenye usafi na kutakasika, ili tumuepushe na uovu wa khiana na maasi ya uzinzi. Hakika yeye ni miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu walio itakasa dini yao kwa Mwenyezi Mungu.
Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akairarua kanzu yake Yusuf kwa nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hapana malipo ya mwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au kupewa adhabu chungu. [25]
[25] Yusuf akakimbilia mlangoni kutaka kutoka, na yule bibi naye akapiga mbio amtangulie ili amzuie kutoka. Akaivuta kanzu yake kwa nyuma ili kumzuia, akaichana. Hapo wakapambana na mume wa yule bibi mlangoni! Yule bibi akasema kumchongea Yusuf: Hapana malipo ya mwenye kutaka kumfanya mkeo mambo mabaya ila atiwe gerezani, au akutishwe adhabu chungu!
Yusuf akasema: Yeye ndiye aliye nitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliye kuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo. [26]
[26] Yusuf akasema kujitetea: Ni yeye ndiye aliyenitaka, na akajaribu kunikhadaa! Ikawa ni kusutana. Alikata hukumu mmojapo katika jamaa zake mwenyewe yule mwanamke kwa kusema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi huyu bibi kasema kweli katika madai yake, na huyu kijana ni mwongo kwa aliyo yasema.
Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni katika vitimbi vyenu wanawake. Bila ya shaka vitimbi vyenu ni vikuu. [28]
[28] Mume alipoona kuwa kanzu ya Yusuf imechanwa mgongoni alimwambia mkewe: Huku kumtuhumu kwako kijana kwa yaliyo tokea na hali yeye hana makosa, ni katika vitimbi vyenu, enyi wanawake. Hakika vitimbi vyenu ni vikuu mno!
Yusuf! Wachilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Kwa hakika wewe ni katika walio fanya makosa. [29]
[29] Ewe Yusuf wachilia mbali mambo haya, na wewe yafiche wala usiyaseme. Na wewe, mwanamke, omba maghfira kwa dhambi yako. Hapana shaka kuwa wewe ni katika wenye dhambi, wenye kuyakusudia makosa, na kutenda maasi, na kuwasingizia wengine uasi wasio ufanya!
Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake ! Hakika amesalitika kwa mapenzi. Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio dhaahiri. [30]
[30] Khabari zikawafikia baadhi ya wanawake wa mjini, wakazungumza wakisema: Mke wa Mheshimiwa anamzaini mtumishi wake na anamkhadaa amkubalie anayo yataka kwake! Ama kweli amesalitika kwa mahaba hata hajitambui! Hakika sisi tunaamini kuwa kwa mwendo wake huu ameingia kwenye upotovu na makosa yaliyo wazi.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".