Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao hawatambui. [15]
[15] Walipo kwenda naye mbali na baba yake, na wakakubaliana rai yao ya kumtumbukiza ndani ya kisima, walifanya hayo waliyo yaazimia. Sisi tukamtia moyoni mwake Yusuf atulie, na awe na imani ya Mwenyezi Mungu, kuwa bila ya shaka atakuja waeleza haya mambo yao waliyo yapanga na wakayatenda, na wala wao wenyewe hawajui hapo utapo waambia kwamba wewe ndiye Yusuf waliye mfanyia vitimbi, na wakadhani wamekwisha mmaliza na wameepukana naye!
Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli. [17]
[17] Wakasema: Ewe baba yetu! Sisi tulikwenda kushindana kupiga mishale na kwenda mbio, na tukamwacha Yusuf kwenye vitu vyetu avilinde. Mbwa mwitu akamla, na sisi tuko mbali tumeshughulika na mashindano! Na wewe hutusadiki tunayo yasema, ijapokuwa tunasema haki na kweli!
Wakaja na kanzu yake ina damu ya uwongo. Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza. [18]
[18] Wakaileta kanzu yake nayo ina damu, ati kuwa ni ushahidi wa yale madai yao ya kuwa ile ni damu ya Yusuf, apate kusadiki baba yao! Walakini yeye alisema: Hakika huyo mbwa mwitu hakumla kama mnavyo singizia, bali nafsi zenu zimekupelekeeni kufanya jambo kubwa, na mkalitimiza! Langu mimi ni kusubiri subira njema isiyo legalega kwa mliyo nikutisha. Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anaye takiwa msaada kwa huo upotovu mlio uzua na mnao udai.
Ukafika msafara, wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Kheri Inshallah! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayo yatenda. [19]
[19] Wakaja watu upande ule wa kisima katika msafara wao wa kwendea Misri. Wakamtuma mtu kati yao wa kuchota maji kisimani awaletee. Akatumbukiza ndoo yake, akiivuta na Yusuf kang'ang'anilia! Yule mchota maji akapiga kelele za furaha: Kheri! Kheri gani hii na furaha! Huyu ni kijana! Wakamficha katika vitu vyao, wakamfanya ni bidhaa ya biashara! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyazunguka yote wayatendayo kwa ujuzi wake.
. Na wakamuuza kwa thamani duni, kwa akali ya pesa. Wala hawakuwa na haja naye. [20]
[20] Wakamuuza Misri kwa bei ya chini kabisa, si kiasi chake! Thamani yake ilikuwa ni pesa chache tu! Wala hawakuwa wakimtakia Yusuf thamani kubwa, kwa kukhofia wasije watu wake wakamkuta wakamtambua, na wakawapokonya Yusuf.
Na yule aliye mnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makaazi ya hishima huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwenetu. Na kama hivyo tulimweka Yusuf katika nchi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui. [21]
[21] Yule aliye mnunua kule Misri alimwambia mkewe: Mfanyie wema huyu, na umhishimu, ili makao yake hapa nasi yawe mazuri. Huenda akatufaa, au tukamfanya kuwa ni mwenetu. Kama yalivyo kuwa makaazi yake ni mazuri na ya hishima, basi kadhaalika tulimjaalia Yusuf katika nchi ya Misri cheo kingine kikubwa, ili atekeleze uadilifu na mipango mizuri, na ili tumfunze kufasiri mambo na ndoto, ajue yatakayo kuwa kabla hayajwa, ili awe tayari kuyakabili! Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kutimiza kila jambo alitakalo. Kabisa haemewi na kitu. Lakini watu wengi hawajui siri ya hikima yake, na undani wa mipango yake.
Na alipo fikilia utu uzima tulimpa hukumu na ilimu. Na kama hivi tunawalipa wanao tenda mema. [22]
[22] Na Yusuf alipo timia ukomo wa nguvu zake tukampa hukumu yenye kusibu, na ilimu yenye kufaa. Na kama malipo haya tuliyo mpa yeye kwa wema wake, ndio tunavyo wapa wote walio wema kwa vitendo vyao vyema.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
លទ្ធផលស្វែងរក:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".