Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: យូសុហ្វ   អាយ៉ាត់:
۞ وَمَآ أُبَرِّئُ نَفۡسِيٓۚ إِنَّ ٱلنَّفۡسَ لَأَمَّارَةُۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّيٓۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٞ رَّحِيمٞ
NAmi sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu, isipo kuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu. [53]
[53] Wala sidai kuwa nafsi yangu haitelezi; kwani ni tabia ya nafsi kumili kwenye matamanio, na kupendelea maovu na shari. Isipo kuwa nafsi aliyo ilinda Mwenyezi Mungu na akaiweka mbali na maovu. Na hakika mimi ninatumai rehema ya Mwenyezi Mungu na msamaha wake, kwani Yeye ni Mkunjufu wa kusamehe dhambi za wenye kutubu, na yu karibu wa kuwarehemu waja wake walio kosa.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦٓ أَسۡتَخۡلِصۡهُ لِنَفۡسِيۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُۥ قَالَ إِنَّكَ ٱلۡيَوۡمَ لَدَيۡنَا مَكِينٌ أَمِينٞ
Basi mfalme akasema: Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa. Basi alipo msemeza alinena: Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na umeaminika. [54]
[54] Usafi wa Yusuf ulipo dhihiri kwa mfalme, aliazimu amwite. Akawatuma watu wake wamlete awe wake yeye mwenyewe wa kumsafia niya. Basi alipo hudhuria na yakapita baina yao mazungumzo, mfalme akaathirika na utukufu wa Yusuf kwa usafi wa nafsi yake, na ubora wa rai zake! Akamwambia: Sasa wewe kwangu utakuwa na cheo cha hishima kilicho thibiti. Na wewe ni muaminifu kwangu ninaye kuamini.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ ٱجۡعَلۡنِي عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلۡأَرۡضِۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٞ
Yusuf akasema: Nifanye mshika khazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mjuzi. [55]
[55] Mfalme akajua kwake Yusuf kuwa yeye ni muangalizi mwema na mweza wa kazi yake. Na Yusuf akahisi hayo. Hapo akataka amfanye waziri akamwambia: Nitawalishe juu ya khazina zote za mamlaka yako, na ghala za nchi yako. Kwani mimi kama ulivyo yakinika mwenyewe naweza kuendesha mambo ya serikali, nami ni mlinzi, na najua kupanga na kuendesha mambo.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ يَتَبَوَّأُ مِنۡهَا حَيۡثُ يَشَآءُۚ نُصِيبُ بِرَحۡمَتِنَا مَن نَّشَآءُۖ وَلَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Basi namna hivi tukampa Yusuf cheo katika nchi; anakaa humo popote anapo penda. Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupuuzi malipo ya wafanyao mema. [56]
[56] Mfalme alilikubali ombi lake, akamfanya waziri wake. Hivyo basi Mwenyezi Mungu alimneemesha Yusuf kwa neema nzuri, akampa madaraka na uwezo katika nchi ya Misri, akienda humo atakapo. Na hii ndiyo shani yake Mwenyezi Mungu kwa waja wake, humpa neema yake amtakaye katika wao, wala hawanyimi thawabu zao, bali huwapa ujira wao wa wema wautendao kwa kuwalipa mema hapa hapa duniani.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَكَانُواْ يَتَّقُونَ
Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa walio amini na wakawa wachamungu. [57]
[57] Na malipo yao ya Akhera ni bora zaidi na yanalingana zaidi na hao wanao msadiki Yeye na Mitume wake, na ikawa wanaingojea Siku ya Hisabu na wanaikhofu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَجَآءَ إِخۡوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَعَرَفَهُمۡ وَهُمۡ لَهُۥ مُنكِرُونَ
Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia kwake. Yeye akawajua na wao hawakumjua. [58]
[58] Ukame ukazidi kushtadi katika nchi jirani na Misri. Ikawapata watu wa Yaa'qub shida vile vile kama ilivyo wapata wengineo. Watu walikwenda Misri kutoka kila pande baada ya kujua matengenezo ya Yusuf ya kuweka akiba chakula, na kujitayarisha kwake kwa miaka ya ukame. Yaa'qub aliwatuma wanawe wende kutafuta chakula, lakini akabaki naye nduguye Yusuf kwa mama kwa kumkhofia. Wale watoto wake walipo fika Misri wakenda moja kwa moja kwa Yusuf, naye akawatambua, lakini wao hawakumjua.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ قَالَ ٱئۡتُونِي بِأَخٖ لَّكُم مِّنۡ أَبِيكُمۡۚ أَلَا تَرَوۡنَ أَنِّيٓ أُوفِي ٱلۡكَيۡلَ وَأَنَا۠ خَيۡرُ ٱلۡمُنزِلِينَ
Na alipo watengenezea tayari haja yao alisema: Nileteeni ndugu yenu kwa baba. Je! Hamwoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa kukirimu? [59]
[59] Yusuf akaamrisha wakaribishwe ugeni, na wapewe mahitaji wanayo yataka. Wakapewa hayo. Akaingia kuzungumza nao na kuwauliza hali zao kama mtu asiye wajua! Naye anawajua vyema. Nao wakamwambia kuwa wamemwacha ndugu yao mmoja kwa baba yao, kwani hapendi kuachana naye. Naye huyo ni Bin-yamini nduguye Yusuf kwa baba na mama. Basi yeye akasema: Mwacheni ndugu yenu aje nanyi, wala msiogope chochote. Nyinyi mmekwisha ona vipi ninavyo kutimizieni vipimo vyenu, na ninavyo kukirimuni.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَإِن لَّمۡ تَأۡتُونِي بِهِۦ فَلَا كَيۡلَ لَكُمۡ عِندِي وَلَا تَقۡرَبُونِ
Na msipo niletea basi hampati kipimo chochote kwangu, wala msinikurubie. [60]
[60] Mkitomleta ndugu yenu huyu, basi hampati chakula kwangu, wala msijaribu kunijia tena.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالُواْ سَنُرَٰوِدُ عَنۡهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَٰعِلُونَ
Wakasema: Sisi tutamrairai baba yake; na bila ya shaka tutafanya hayo. [61]
[61] Nduguze wakasema: Tutajaribu kusema na baba yake ageuze rai yake, iondoke khofu yake juu ya mwanawe. Na sisi tunakuhakikishia kuwa hatutokasiri wala kulegalega katika hayo.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَقَالَ لِفِتۡيَٰنِهِ ٱجۡعَلُواْ بِضَٰعَتَهُمۡ فِي رِحَالِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَعۡرِفُونَهَآ إِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili wazione watakapo rudi kwa watu wao wapate kurejea tena. [62]
[62] Walipo taka kuondoka aliwaambia wafwasi wake: Watilieni thamani ya bidhaa yao waliyo kuja nayo humo humo pamoja na mizigo yao, ili waione watakapo rudi kwa watu wao, wapate kurejea tena kwa kutumai kupewa chakula kwa kuamini kuwa tunatimiza ahadi, na wawe na imani ya usalama wa ndugu yao, na baba yao azidi kutua nafsi yake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَلَمَّا رَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَبِيهِمۡ قَالُواْ يَٰٓأَبَانَا مُنِعَ مِنَّا ٱلۡكَيۡلُ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَآ أَخَانَا نَكۡتَلۡ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ
Basi walipo rejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula zaidi, basi mpeleke nasi ndugu yetu ili tupate kupimiwa; na yakini sisi tutamlinda. [63]
[63] Walipo rejea kwa baba yao walimsimulia kisa chao na Mheshimiwa wa Misri, na upole wake kwao, na kwamba amewaonya kuwa atawanyima kuwapimia chakula baadae ikiwa hatokuwa nao Bin-yamini; na kwamba amewaahidi kuwatimizia kipimo na atawatukuza pindi wakirudi na ndugu yao. Wakamwambia baba yao: Mwache ende nasi ndugu yetu, kwani ukimpeleka yeye tutapimiwa chakula cha kutosha tunacho kihitajia. Nasi tunakuahidi ahadi ya nguvu ya kwamba tutafanya juhudi kumlinda.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: យូសុហ្វ
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ