Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់អ៊ីសរ៉ក   អាយ៉ាត់:
وَمَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَلَن تَجِدَ لَهُمۡ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِهِۦۖ وَنَحۡشُرُهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ عُمۡيٗا وَبُكۡمٗا وَصُمّٗاۖ مَّأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ كُلَّمَا خَبَتۡ زِدۡنَٰهُمۡ سَعِيرٗا
Na anaye mhidi (muongoza) Mwenyezi Mungu basi huyo ndiye aliye hidika. Na anaye wapotoa basi huto wapatia walinzi badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.
Waambie: Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa kwa kuwa yu tayari kufuata uwongofu, basi huyo ni mwongofu. Na anaye mpotoa kwa kufisidika khulka yake, hutopata wa kuwanusuru asiye kuwa Yeye wa kuwaongoa duniani. Na Akhera tutawakusanya wakikokotwa juu ya nyuso zao, hawaoni, wala hawasemi, wala hawasikii. Na mahali pao wanapo pelekwa kukaa ni Jahannamu. Kula moto ukipungua ukali wake Mwenyezi Mungu anazidi kuuchochea uwake kwa nguvu zaidi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُم بِأَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَقَالُوٓاْ أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا وَرُفَٰتًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ خَلۡقٗا جَدِيدًا
Hayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa ishara zetu, na wakasema: Hivyo tukisha kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya?
Adhabu hiyo ndiyo malipo yao kwa sababu ya kuzikataa dalili tulizo waletea za kuthibitisha Haki, na kwa ile kauli yao kusema: Hivyo sisi tutafufuliwa kwa umbo jipya baada ya kwisha kuwa mifupa na vumbi?
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
۞ أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يَخۡلُقَ مِثۡلَهُمۡ وَجَعَلَ لَهُمۡ أَجَلٗا لَّا رَيۡبَ فِيهِ فَأَبَى ٱلظَّٰلِمُونَ إِلَّا كُفُورٗا
Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhaalimu hawataki ila ukafiri.
Jee wameghafilika na hawakujua kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, juu ya ukubwa wao, ni Mwenye kuweza kuumba watu na majini kama wao? Na Mwenye kuweza hayo, vipi awe hawezi kuwarejesha wao upya, na hilo ni jepesi zaidi kwake! Na Yeye Subhanahu ameweka muda maalumu wa kuwarejesha tena baada ya kwisha kufa, na huo hauna shaka kuwa. Na muda huo ndio Siku ya Kiyama. Na juu ya hivyo walio zidhulumu nafsi zao kwa ukafiri wanakataa baada ya kuletewa hoja hizi. Na hayo si kwa lolote ila kwa ukafiri tu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قُل لَّوۡ أَنتُمۡ تَمۡلِكُونَ خَزَآئِنَ رَحۡمَةِ رَبِّيٓ إِذٗا لَّأَمۡسَكۡتُمۡ خَشۡيَةَ ٱلۡإِنفَاقِۚ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ قَتُورٗا
Sema: Lau kuwa nyinyi mnazimiliki khazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngeli zuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu. Na mwanaadamu tangu hapo tabia yake ni mchoyo!.
Waambie hawa washirikina: Lau kuwa mnazimiliki riziki za Mola wangu Mlezi, mngeli zifanyia ubakhili kwa kuogopa ufakiri. Kwani ni tabia ya watu kuwa na pupa na ubakhili. Na Mwenyezi Mungu, Mkwasi na Karimu, humpa anacho taka amtakaye, na huteremsha miujiza aitakayo Yeye, sio waitakayo watu. Na Yeye katika yote hayo ni Mwenye hikima na Mjuzi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ تِسۡعَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ فَسۡـَٔلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِذۡ جَآءَهُمۡ فَقَالَ لَهُۥ فِرۡعَوۡنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰمُوسَىٰ مَسۡحُورٗا
Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!.
Na lau hawa watu wangeli letewa hizo ishara wazitakazo, wange zigeuzia uso, wala wasinge ziamini! Na Sisi tulimpa Musa Ishara tisa wazi. Na juu ya hivyo wakakufuru. Na Firauni akasema: Hakika mimi nakuona wewe, Musa, ni mtu uliye rogwa! Hizo ishara tisa ni: 1. Fimbo, 2. Mkono Mweupe, 3. Tufani, 4. Nzige na vyura na chawa na damu, 5. Ukame na upungufu wa mazao, 6. Kupasuka bahari, 7. Kutimbuka maji baharini, 8. Kuning'inia mlima kama kivuli, 9. Kusemezwa na Mola wake Mlezi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قَالَ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَآ أَنزَلَ هَٰٓؤُلَآءِ إِلَّا رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ بَصَآئِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰفِرۡعَوۡنُ مَثۡبُورٗا
Musa akasema: Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia.
Musa akasema: Ewe Firauni! Unajua vyema kuwa aliye ziteremsha Ishara hizi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Kwani ni Yeye ndiye Mwenye kuweza hayo. Nazo Ishara hizo zi wazi, zinakuonyesha ukweli wangu. Lakini wewe unafanya kiburi na inadi tu. Na hakika mimi nakuona wewe, Firauni, kuwa ni mwenye kuangamia ikiwa hutoacha inadi yako.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
فَأَرَادَ أَن يَسۡتَفِزَّهُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ فَأَغۡرَقۡنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ جَمِيعٗا
Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na walio kuwa pamoja naye wote.
Firauni akashikilia uasi wake, akataka kumtoa Musa na Wana wa Israili katika nchi ya Misri. Tukamzamisha yeye na askari wake wote.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَقُلۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِۦ لِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱسۡكُنُواْ ٱلۡأَرۡضَ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأٓخِرَةِ جِئۡنَا بِكُمۡ لَفِيفٗا
Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaeni katika nchi. Itapo kuja ahadi ya Akhera tutakuleteni nyote pamoja.
Tukamvua Musa na kaumu yake, na baada ya kumzamisha Firauni tukasema kuwaambia Wana wa Israili: Kaeni katika nchi takatifu ilioko Sham. Ukija wakati wa uhai wa pili tutakutoeni makaburini kwenu kwa mchanganyiko. Kisha tutakuhukumuni kwa uadilifu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់អ៊ីសរ៉ក
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ