Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់អ៊ីសរ៉ក   អាយ៉ាត់:
ذَٰلِكَ مِمَّآ أَوۡحَىٰٓ إِلَيۡكَ رَبُّكَ مِنَ ٱلۡحِكۡمَةِۗ وَلَا تَجۡعَلۡ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتُلۡقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومٗا مَّدۡحُورًا
Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na kufurushwa. [39]
[39] Na hayo ni katika aliyo kufunulia Mola wako Mlezi, katika kuijua haki kwa dhati yake, na kheri ipate kutendwa. Wala usimfanyie Mwenyezi Mungu kuwa na mungu mwengine, usije kutupwa katika Jahannamu ukijilaumu na ukilaumiwa, umeangamia na umefurushwa mbali na rehema za Mola wako Mlezi.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
أَفَأَصۡفَىٰكُمۡ رَبُّكُم بِٱلۡبَنِينَ وَٱتَّخَذَ مِنَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنَٰثًاۚ إِنَّكُمۡ لَتَقُولُونَ قَوۡلًا عَظِيمٗا
Je! Mola wenu Mlezi amekuteulieni wavulana, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake? Kwa hakika nyinyi mnasema usemi mkubwa. [40]
[40] Subhanahu anayachukia wayasemayo makafiri kwamba Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Anasema: Mola wenu Mlezi amekufadhilisheni kuliko Mwenyewe kwa kukupeni nyinyi watoto wanaume wenye nguvu, na Yeye akawafanya Malaika ni banati zake kwa mnavyo dai? Kwa maneno yenu haya mnazua matusi makubwa.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَلَقَدۡ صَرَّفۡنَا فِي هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ لِيَذَّكَّرُواْ وَمَا يَزِيدُهُمۡ إِلَّا نُفُورٗا
Na tumekwisha bainisha katika Qur'ani hii ili wapate kukumbuka. Lakini haikuwazidisha ila kuwa mbali nayo. [41]
[41] Sisi tumebainisha katika Qur'ani hii kwa uwazi mzuri, tukipiga mifano na kutoa mawaidha na hukumu, ili wapate kwaidhika hawa washirikina. Lakini nyoyo zao zimekuwa kama mawe. Kubainisha huku hakukuwazidishia ila kuzidi kuwakimbiza na Haki.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
قُل لَّوۡ كَانَ مَعَهُۥٓ ءَالِهَةٞ كَمَا يَقُولُونَ إِذٗا لَّٱبۡتَغَوۡاْ إِلَىٰ ذِي ٱلۡعَرۡشِ سَبِيلٗا
Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi. [42]
[42] Ewe Nabii! Ili kudhihirisha upotovu wa madai yao wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu, sema: Lau kuwa wapo miungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu kama wasemavyo, hao miungu wangeli tafuta njia kumfikilia huyo Mwenye Ufalme wa mwisho ili wapate kushindana naye.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوّٗا كَبِيرٗا
Subhanahu Wa Taa'la, Ametakasika na Ametukuka juu kabisa na hayo wanayo yasema. [43]
[43] Mwenyezi Mungu ametakasika kabisa kama anavyo stahiki, na ametukuka aliye mkuu shani yake na yote wanayo dai kuwa wapo pamoja na Yeye miungu wengine.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
تُسَبِّحُ لَهُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ ٱلسَّبۡعُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِيهِنَّۚ وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمۡدِهِۦ وَلَٰكِن لَّا تَفۡقَهُونَ تَسۡبِيحَهُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورٗا
Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira. [44]
[44] Hakika mbingu saba na ardhi, na viumbe vyote viliomo humo, vinamtakasa na kumtukuza, na vinaonyesha uzuri wa kuumba kwake, na kutakasika kwake Subhanahu na kila upungufu, na kukamilika ufalme wake, na kwamba Yeye hana mshirika na yeyote katika viumbe wa Ufalme wake uliyo enea. Vyote hivyo vinamtakasa na kumsifu. Lakini makafiri hawafahamu hoja hizi kwa kutawaliwa nyoyo zao na mghafala. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwao, na Mwenye kuwasamehe wanao tubu. Kwa hivyo hawafanyii haraka kuwapa adhabu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ جَعَلۡنَا بَيۡنَكَ وَبَيۡنَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ حِجَابٗا مَّسۡتُورٗا
Na unapo soma Qur'ani tunaweka baina yako na wale wasio iamini Akhera pazia linalo wafunika. [45]
[45] Ewe Nabii! Unapo soma Qur'ani inayo taja dalili za Haki, Sisi huweka pazia, lenye kukuficha baina yako na wale wasio amini kufufuliwa na malipo, pale wanapo taka kukushambulia. Kwa hivyo hawakuoni.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَجَعَلۡنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ أَكِنَّةً أَن يَفۡقَهُوهُ وَفِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَقۡرٗاۚ وَإِذَا ذَكَرۡتَ رَبَّكَ فِي ٱلۡقُرۡءَانِ وَحۡدَهُۥ وَلَّوۡاْ عَلَىٰٓ أَدۡبَٰرِهِمۡ نُفُورٗا
Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapo mtaja katika Qur'ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakenda zao. [46]
[46] Na kwa mujibu wa hikima yetu ya kupotoa na kuongoa huweka vifuniko juu ya nyoyo zao, wasipate kuifahamu Qur'ani ilivyo. Na katika masikio yao hutia uziwi basi hawasikii lenye manufaa kwao. Hayo ni kwa sababu ya kupindukia katika inda yao na majivuno yao. Na pale unapo mtaja Mola wako Mlezi katika Qur'ani peke yake bila ya kuwataja miungu yao, wao basi hurejea nyuma wakaacha kukusikiliza.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَسۡتَمِعُونَ بِهِۦٓ إِذۡ يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَ وَإِذۡ هُمۡ نَجۡوَىٰٓ إِذۡ يَقُولُ ٱلظَّٰلِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلٗا مَّسۡحُورًا
Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayo sikilizia wanapo kusikiliza, na wanapo nong'ona. Wanapo sema hao madhaalimu: Nyinyi hamumfuati isipo kuwa mtu aliye rogwa. [47]
[47] Sisi tunajua vyema vile wanavyo isikiliza Qur'ani nao ilhali wanaikejeli na kuifanyia maskhara na huku wanakusikiliza. Nao wanayaficha yaliyo semwa. Na hiyo ndiyo kauli ya wenye kudhulumu katika siri zao, wakisema: Ikiwa mtamfuata huyu basi hamumfuati ila mtu aliye geuzwa akili yake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ٱنظُرۡ كَيۡفَ ضَرَبُواْ لَكَ ٱلۡأَمۡثَالَ فَضَلُّواْ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ سَبِيلٗا
Tazama vipi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea. Kwa hivyo hawawezi kuipata njia. [48]
[48] Hebu angalia vipi walivyo kushabihisha; wamekushabihisha na mtu aliye rogwa, na wakakuita kohani, mtunga mashairi, wakaipotea njia ya hoja. Kwa hivyo wasiweze kupata njia ya kuzua tusi linalo kubalika, au kwa hivyo wakaukosa uwongofu, na wasiipate njia ya kuufikilia.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَقَالُوٓاْ أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا وَرُفَٰتًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ خَلۡقٗا جَدِيدٗا
Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika, tutafufuliwa kwa umbo jipya? [49]
[49] Wanao kataa kuwa watafufuliwa wanasema: Hivyo tutafuliwa baada ya kwisha kuwa mafupa yaliyo bunguliwa, na mapande mbali mbali, tukawa hai na umbo jipya? Haya hayaingii akilini.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់អ៊ីសរ៉ក
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ