Check out the new design

ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី * - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់អ៊ីសរ៉ក   អាយ៉ាត់:
مَّن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡعَاجِلَةَ عَجَّلۡنَا لَهُۥ فِيهَا مَا نَشَآءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلۡنَا لَهُۥ جَهَنَّمَ يَصۡلَىٰهَا مَذۡمُومٗا مَّدۡحُورٗا
Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayo yataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa. [18]
[18] Mwenye kutaka starehe za dunia hii ipitayo na akazitumikia kwa kutafutia kisingizio, wala asiwe na yakini na miadi, na wala asingojee malipo ya Akhera, tutamletea haraka haraka tuyatakayo ya duniani kwa ukunjufu na wasaa. Haya ni kwa tumtakaye kumletea haraka. Kisha tutamuandalia kwa Akhera Jahannamu ahilikike kwa joto lake, naye hali awe ni mwenye kushutumiwa kwa aliyo yatenda, mwenye kutengwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَمَنۡ أَرَادَ ٱلۡأٓخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعۡيَهَا وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ كَانَ سَعۡيُهُم مَّشۡكُورٗا
Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a'mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa. [19]
[19] Na mwenye kuitaka Akhera kwa vitendo vyake, naye akawa navyo hivyo vitendo, na akawa anamuamini Mwenyezi Mungu na malipo yake, basi watu kama hao vitendo vyao vitakubaliwa na Mwenyezi Mungu na watapata malipo kwa ajili yake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
كُلّٗا نُّمِدُّ هَٰٓؤُلَآءِ وَهَٰٓؤُلَآءِ مِنۡ عَطَآءِ رَبِّكَۚ وَمَا كَانَ عَطَآءُ رَبِّكَ مَحۡظُورًا
Wote hao tunawakunjulia - hawa na hao - katika neema za Mola wako Mlezi. Wala neema za Mola wako Mlezi hazizuiliki. [20]
[20] Na Sisi tutawakunjulia neema za Mola wako Mlezi hapa duniani makundi yote mawili, pindi wakichukua khatua ya kufikia hayo. Wala neema za Mola wako Mlezi hatonyimwa yeyote, akiwa Muumini au akiwa kafiri, maadamu wakishika njia za kuzitafuta.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
ٱنظُرۡ كَيۡفَ فَضَّلۡنَا بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۚ وَلَلۡأٓخِرَةُ أَكۡبَرُ دَرَجَٰتٖ وَأَكۡبَرُ تَفۡضِيلٗا
Angalia vipi tulivyo wafadhili baadhi yao kuliko wenginewe. Na hakika Akhera ni yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi. [21]
[21] Hebu angalia kwa kuzingatia vipi tulivyo wafadhilisha baadhi ya waja wetu kuliko wengine, kwa kuwapa mali na vyeo na nafasi, pindi wakishika njia za kuyapata hayo katika dunia. Na hayo ni kwa hikima tunayo ijua Sisi. Na tafauti zao katika Akhera ni kubwa zaidi kuliko tafauti zao za duniani. Kwa hivyo yatakikana waishughulikie Akhera, kwani huko ndiko kwenye kutukuka kwa kweli na kuzidiana kwa hakika.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
لَّا تَجۡعَلۡ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَقۡعُدَ مَذۡمُومٗا مَّخۡذُولٗا
Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, usije ukawa wa kulaumiwa uliye tupika. [22]
[22] Ewe mwenye jukumu! Usimfanyie Mwenyezi Mungu kuwa na mshirika, utakuja fedheheka kwa kudharauliwa, na utajaaliwa uwe mwenye kutupika.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
۞ وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنًاۚ إِمَّا يَبۡلُغَنَّ عِندَكَ ٱلۡكِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوۡ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفّٖ وَلَا تَنۡهَرۡهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوۡلٗا كَرِيمٗا
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. [23]
[23] Na Mola wako Mlezi amehukumu kuwa msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye. Na pia muwafanyie wema kwa ukamilifu wazazi wenu wawili. Na hao, au mmoja wao, wakifikilia kwako hali ya unyonge na mwisho wa umri wao, basi lisikutoke tamko la kuchoka nao au kuudhika kwa yanayo kupata kutokana nao. Wala usiwahamakie. Na nena nao maneno mazuri, laini, yenye kuwaonyesha ihsani na kuwahishimu.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَٱخۡفِضۡ لَهُمَا جَنَاحَ ٱلذُّلِّ مِنَ ٱلرَّحۡمَةِ وَقُل رَّبِّ ٱرۡحَمۡهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرٗا
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni. [24]
[24] Na wafanyie upole, na wanyenyekee kwa kuwaonea huruma, na uwaombee: Ewe Mola Mlezi! Warehemu wote wawili, kama walivyo nifanyia huruma walipo nilea utotoni.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمۡۚ إِن تَكُونُواْ صَٰلِحِينَ فَإِنَّهُۥ كَانَ لِلۡأَوَّٰبِينَ غَفُورٗا
Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanao tubia kwake. [25]
[25] Enyi watu! Mola wenu Mlezi anajua kuliko nyinyi yaliyomo katika dhamiri zenu, na atakuhasibuni kwayo kwa thawabu na i'kabu. Na mkiwa mnakusudia wema na mkautenda, tena mkatokea baadhi yenu mkateleza, na kisha mkarejea kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Subhanahu atakusameheni. Kwani Yeye ni Mwenye kusamehe daima kwa wale wanao rejea kwake.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
وَءَاتِ ذَا ٱلۡقُرۡبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلۡمِسۡكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرۡ تَبۡذِيرًا
Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. [26]
[26] Na wape jamaa zako haki yao kwa kuwafanyia wema na kuwaunga; na kadhaalika masikini mwenye haja, na msafiri aliye katikana na mali yake. Wape hao haki yao katika Zaka na sadaka, wala usiyavuruge mali yako kwa utumiaji ovyo usio na maslaha.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
إِنَّ ٱلۡمُبَذِّرِينَ كَانُوٓاْ إِخۡوَٰنَ ٱلشَّيَٰطِينِۖ وَكَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ لِرَبِّهِۦ كَفُورٗا
Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. Na Shet'ani ni mwenye kumkufuru Mola wake Mlezi. [27]
[27] Kwani wabadhirifu (watumiaji ovyo) wenzao ni Mashetani, wanapokea minong'ono yao wanapo wachochea wafanye ufisadi na watumie kwa uharibifu. Na ni mtindo wa Shetani daima kukufuru neema ya Mola wake Mlezi. Na sahibu yake ni hali kadhaalika.
តាហ្វសៀរជាភាសា​អារ៉ាប់ជាច្រេីន:
 
ការបកប្រែអត្ថន័យ ជំពូក​: អាល់អ៊ីសរ៉ក
សន្ទស្សន៍នៃជំពូក លេខ​ទំព័រ
 
ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី - សន្ទស្សន៍នៃការបកប្រែ

បកប្រែដោយលោកអាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

បិទ