prev

Al-Bayyinah

next

external-link copy
1 : 98

لَمۡ يَكُنِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡبَيِّنَةُ

Hawakuwa wenye kukufuru miongoni mwa Mayhudi na Wanaswara na washirikina ni wenye kuacha ukafiri wao mpaka uwajilie wao ushahidi walioahidiwa katika vitabu vilivyopita. info
التفاسير: |

external-link copy
2 : 98

رَسُولٞ مِّنَ ٱللَّهِ يَتۡلُواْ صُحُفٗا مُّطَهَّرَةٗ

Nao ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, atakayewasomea Qur’ani iliyomo kwenye kurasa safi. info
التفاسير: |

external-link copy
3 : 98

فِيهَا كُتُبٞ قَيِّمَةٞ

Ndani ya kurasa hizo mna habari za kweli na amri za uadilifu zenye kuongoza kwenye haki na kwenye njia ilionyoka. info
التفاسير: |

external-link copy
4 : 98

وَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَةُ

Na hawakutofautiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara, juu ya kuwa Muhammad , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni Mtume wa kweli, kwa sifa zake waliokuwa wakiziona katika vtabu vyao isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabii waliyoahidiwa katika Taurati na Injili. Walikuwa wanakubali , kwa umoja wao, kuwa unabii wake ni wa kweli. Lakini alipotumilizwa waliukanusha na wakatofautiana. info
التفاسير: |

external-link copy
5 : 98

وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلۡقَيِّمَةِ

Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa ni wamuabudu Mwenyezi Mungu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada yao kupata Radhi Zake, hali ya kuepuka upande wa ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka. Kufanya hayo ndio Dini iliyolingana , nayo ni Uislamu. info
التفاسير: |
prev

Al-Bayyinah

next